Mimi nilikuwa shabiki mkubwa wa Tundu Lissu lakini lazima niseme ukweli ulio moyoni mwangu huyu jamaa amefeli kisiasa kabisa hakuwa na mipango mizuri wala mshauri mzuri., Kwa sababu kama haya anayodai sasa kuhakikishiwa usalama wake ndio aje swali ni mbona uchaguzi alikuja hivyo hivyo kugombea hakujali kuhakikishiwa usalama wala chochote alikuja tu,
Ulipomaliza uchaguzi akadai anataka kuuliwa na mtu aliyemtumia sms akakimbilia ubalozi lakini mbona hakukua na na chochote ule mpango kama ulipita na upepo tu wala hakuna anayezungumza tena sio nje huko aliko wala Tz ni kama vile alijaribu kutaka kutengeneza issue lakini haikuwa na vidhibiti angalau vimuweke katika mazingira mazuri zaidi, alifeli
Umemaliza uchaguzi hakuvumilia ata wiki moja kuonyesha wapiga kura wake kote alikotembelea angalau kuwambia chochote, alienda ubalozi na kutimkia belgium na hata alipofika kule belgum hakuwambia chochote wanachadema ni kama vile alikuja kwa shida ya kusaka urais tu bas ndio iliyokuwa shida yake hakujali wananchi wake., sijuwi alifeli wapi angalau angemsoma maalim seif na vitisho alivyofanyiwa lakini hakuwa mbali na wazanzibari.
Ile kupigwa risasi ilitokea lakini je kwa dunia ilivyoliona lile kweli angepigwa tena marisasi kiongozi aliyetoka kugombea urais?
Huko youtube na twitter anaona ndio jukwaa lake la kisiasa anadhan inatosha? Watanzania wangap hawaelewi twitter wala youtube, jana tumeambiwa watu milioni 8 tu tanzania ndio wanaotumia internet hawa watu wengi waliobaki atawafikia vipi kwa twitter na youtube?
Ndio mana nimesema amefeli sana
..Lissu ni mwanasheria, na maamuzi yake mengi huyafanya kwa jicho la kisheria. wakati wa uchaguzi sheria zetu zinalaelekeza kwamba wagombea wote wa Uraisi ni lazima wapewe ulinzi wa jeshi la Polisi. Lissu alirejea kwasababu alijua hakuna namna serikali ingeweza kukwepa jukumu la kumlinda wakati akiwa mgombea Uraisi.
..kuhusu tishio la kutaka kuuwawa baada ya uchaguzi mkuu, sidhani kama ni sahihi kumlaumu kwamba halina ushahidi. kwa upande mwingine tunapaswa kuilaumu serikali kwa kutokuchunguza tukio la mauaji dhidi ya Tundu Lissu ambalo lina ushahidi wa wazi kabisa. Labda tungejiuliza, ni nchi gani nyingine ambayo kiongozi mwandamizi wa kisiasa anashambuliwa halafu serikali inapuuzia kufanya uchunguzi?
..kuhusu kufanya siasa ktk mtandao nakuomba ufanye utafiti mpya. kama madai yako kuwa watumiaji wa mitandao Tz ni watu milioni 8 ni ya kweli, basi bila shaka mitandao ni uwanja muhimu wa kufanya siasa. ripoti za tume ya uchaguzi zinasema waTz takriban million 15+ walipiga kura ktk uchaguzi wa 2020, hivyo basi zaidi ya nusu ya Watz hao huenda wanatumia mitandao. Kwa msingi huo mwanasiasa yeyote makini hapa Tz lazima ajishughulishe ktk mitandao ya kijamii.