Lissu: Nitarejea Tanzania endapo yafuatayo yatafanyika


..Lissu ni mwanasheria, na maamuzi yake mengi huyafanya kwa jicho la kisheria. wakati wa uchaguzi sheria zetu zinalaelekeza kwamba wagombea wote wa Uraisi ni lazima wapewe ulinzi wa jeshi la Polisi. Lissu alirejea kwasababu alijua hakuna namna serikali ingeweza kukwepa jukumu la kumlinda wakati akiwa mgombea Uraisi.

..kuhusu tishio la kutaka kuuwawa baada ya uchaguzi mkuu, sidhani kama ni sahihi kumlaumu kwamba halina ushahidi. kwa upande mwingine tunapaswa kuilaumu serikali kwa kutokuchunguza tukio la mauaji dhidi ya Tundu Lissu ambalo lina ushahidi wa wazi kabisa. Labda tungejiuliza, ni nchi gani nyingine ambayo kiongozi mwandamizi wa kisiasa anashambuliwa halafu serikali inapuuzia kufanya uchunguzi?

..kuhusu kufanya siasa ktk mtandao nakuomba ufanye utafiti mpya. kama madai yako kuwa watumiaji wa mitandao Tz ni watu milioni 8 ni ya kweli, basi bila shaka mitandao ni uwanja muhimu wa kufanya siasa. ripoti za tume ya uchaguzi zinasema waTz takriban million 15+ walipiga kura ktk uchaguzi wa 2020, hivyo basi zaidi ya nusu ya Watz hao huenda wanatumia mitandao. Kwa msingi huo mwanasiasa yeyote makini hapa Tz lazima ajishughulishe ktk mitandao ya kijamii.
 
Kwani ye Lissu ndio nani mpaka apangie nchi masharti ya kurudi unyankindi kwao, kama hataki kurudi aendelee na mumewe huko
 
mkuu nashukuru kwa maelezo mazuri pia

Ila nimesema maada hii ni outdated now

CDM wanajua kila kitu na waweke wazi sasa kila kitu ...kuna demokrasia sasa sio? issue ya mwaka juzi tu

Ninaposema wanajua, sitanii waanike
1. Let me believe that, unaposema CDM una maana ya CHADEMA, right...?

2. Kama una maana ya CHADEMA, basi, hebu na wewe tusaidie kidogo.

Una maana gani unaposema CHADEMA "wanajua" na "hutanii..?"
å Na wanajua nini..?

å Je, una maana ya kuwa wanawajua waliompiga Tundu Lissu risasi 38 na 16 kuingia mwilini mwake?

√• Je, una maàna ya kuwa, CHADEMA wanawajua waliotoa CCTV camera na walinzi kwenye makazi ya viongozi wakubwa serikalini Area "D" akiwemo Naibu Spika Tulia, Waziri wa Nishati Kalemani nk nk? Wanawajua? Really? Kwa hiyo unawaambia CHADEMA wafanye kazi ya uPolisi..?

NA WEWE WABEROYA HEBU JIBU MASWALI HAYA:

1. Wewe unadhani ni kwanini polisi hawafanyii kazi jinai hii ya jaribio la kuuwawa kwa TL..?

2. Kama unadhani CHADEMA wanaweza kuwa na taarifa muhimu sana juu ya sakata zima la jaribio la kuuwawa kwa TL mwaka 2017, kwanini polisi wasifanye kazi yao? Hata kama wanazo "hizo taarifa na hutanii" wampe nani sasa maana polisi wamezuiwa au hawataki kabisa kuchunguza..?

3. Kwa scenario hii, hivi unategemea mimi na wewe tuielewe vipi serikali kupitia Jeshi la polisi..? There is no other way zaidi ya kusema kuwa, kumbe ni halali kabisa kwa serikali kupitia Jeshi la polisi kushutumiwa kuwa inalinda wahalifu waliohusika ktk unyama huu...!

Na hapa naomba unielewe kuwa, ninaposema, inalinda wahalifu basi nina maanisha wahalifu kweli bila kujali ni kina nani aidha wawe ni CHADEMA, CCM au wewe mwenyewe Waberoya. Polisi wafanye kazi yao. That's all...!!

4. Na Je, wewe nawe Waberoya unaamini kuwa serikali kupitia Jeshi la polisi linashindwa kufanya upelelezi wa tukio/kesi hii kwa sababu ya assumption ya kuwa eti "CHADEMA wamemficha Ubelgiji" aliyekuwa dereva wa Tundu Lissu..??

Kama unaamini ujinga huu, basi wewe hufai kuitwa GT...!!
 
Hayo mambo yanatekelezeka maccm yanaona shida gani kurudisha gari ,stahiki za kibunge na kufuta kesi za kubambikizwa za kisiasa
 
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hayo mambo yanatekelezeka maccm yanaona shida gani kurudisha gari ,stahiki za kibunge na kufuta kesi za kubambikizwa za kisiasa
Abaki huko huko huku hatumtaki, kwanza aliowatapeli na kumfanyizia bado wako mtaani, akae huko huko kwa usalama wake...
 
Bana abaki huko huko, mbona kuna raha kule za kufa mtu, vipi anafuata makorona, mbu, uchafu, miundo mbinu hovyo, huduma za afya hovyo na nini na nini?
Kumbe nyumbani kutamu eeehhhh?!
 
Anataka tumsamehe na ile aliyomwambia Shaka Ssali wa VOA kuwa mlinzi wa Rais alifariki kwa Corona akijua anasema uongo?
 
Tundu Lisu, pamoja na mengine yote, usilotakiwa kulisahau kunena wakati wote, ni ukuu na uweza wa Mungu:

Mtu anaamua kukuua, unashambuliwa kwa risasi 16, yaani kuhakikisha kwa vyovyote iwavyo ufe, halafu hufi. Anaamua kukunyima matibabu ili ufe, hufi. Anaamua kukunyima pesa stahiki yako ili ushindwe kuishi, lakini unaishi.

Mwishowe, yule aliyeamua kukua, aliyeamua wewe usiishi, anakufa yeye, nawe unashuhudia na kutangaza kifo chake kabla hata ya watu wake wa karibu, wewe unaendelea kuishi. Fumbo hili ni kubwa sana katika maisha ya kiimani.
 
Nini lengo la Tundu Lissu hasa? Tujaalie Serikali imepuuza kabisa kuhusu suala lake la kwamba lazima ahakikishiwe ulinzi ndio arejee nchini au mpaka stahiki zake apewe za matibabu na maposho yake pamoja na kiinua mgongo cha ubunge aliokuwa nao, Je nini atafanya Tundu Lissu atasalia belgium maisha yake?

Tija ya Tundu Lissu kufanya siasa kwa twitter na youtube itasaidia nini mpaka lini ilhali hawezi kuja kwa kugombea wala chochote, au unafikiri Tundu Lissu mara hii atachukua form za kugombea urais online na kurejesha online akiwa kule kule na kampeni zake atafanyia online? pia akichaguliwa ataongoza Tanzania kwa online?

Ndio mana nasema Lissu amefeli kisiasa.

Kwanini Lissu baada ya mwendazake kufariki hakushauriwa kukaa kimya kidogo ili kuleta ulaini fulani na kupata muda kufanya mazungumzo na Rais mama Samia akarudi nchini na baada ya kufika kwanza akaangalia hali halisi ya mazingira ya kurudi kwenye siasa tena? Unajua siasa ni kila kitu kinahitaji siasa., maalim seif ni kiongozi wa kuigwa siku zote, maalim alikuwa mvumilivu sana ni kiongozi ambaye hakuwahi kushindwa kufanya siasa kwa njia zozote zile
 
..mama samia amesema tufungue ukurasa mpya.

..siasa za kupigana risasi, kubambikiana kesi , na kudhulumiana,zikome.
 
Sijui kama kuna anayemhitaji. Muache akichoka atarudi. Kwani kuna aliyemtuma huko? Mbona alipokuja kufanya kampeni aliishi vizuri hadi akatengeneza mazingira ya kurejea kwa mabwana zake bila kupigwa hata kofi?
 
Kwani wakati amerudi wakati wa kampeni alihakikishiwa ulinzi na nani?
 
Amri hizo za Lissu hazitekelezeki kama anataka kurudi arudi na kama hataki abaki huko huko huwezi kumuamrisha Rais achie wafungwa ndio wewe uludi kwani wewe ni nani katika Nchi hii.
Good
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…