Lissu: Polisi hawana uwezo wa kukaa na Mbowe muda mrefu gerezani. Mbowe na CHADEMA hatutatoa ushirikiano

Lissu: Polisi hawana uwezo wa kukaa na Mbowe muda mrefu gerezani. Mbowe na CHADEMA hatutatoa ushirikiano

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akiwa katika mtandao wa Kijamii wa “Club House” katika chumba kilichofunguliwa na CHADEMA cha “Mashtaka ya Ugaidi ya Mbowe na Katiba Mpya” amesema CHADEMA haitashiriki katika kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe

Amesema “Hatutaandika barua ya kuomba dhamana, wala yeye hataomba. Mwenyekiti hatatoa ushirikiano wa aina yoyote, sio Polisi sio Mahakamani. Waamue wao wanataka kumfanya nini”

Ameongeza, “Wakikaa naye wajue hii kelele itakuwa kubwa. Wamuachie menyewe, wakimuachia kwa masharti ya kurudi Polisi siku nyingine hatarudi. Na wakimuachia atarudi Mwanza kwenye Kongamano”

Amesisitiza, “Kama wanamuachia waamue wenyewe, na wamuachie bila masharti yoyote. Sisi hatutashiriki kwa lolote katika kesi hii tunayojua ni ya kijinga”

Awali, Lissu alieleza kuwa kabla ya Mbowe kwenda Mwanza walizungumza naye na kusema tabia ya Polisi kuwakama, kukaa nao kwa muda na kisha kuwaachia kwa masharti ya kurudi kuripoti Kituo cha Polisi kila mara wamechoka na sasa hawatakubali.
 
Njia nzuri ya kumaliza haya maigizo yanayofanywa na jeshi la polisi kila wakati CCM ikibanwa mbavu, na hili liwe fundisho kwa polisi na CCM mbele ya safari, habari ya kumuachia kwa masharti halafu mnamwambia awe anaripoti kituoni kila jumatatu saa tatu asubuhi hakuna tena hiyo.
 
Back
Top Bottom