Lissu: Rais Magufuli haonekani kanisani wala mitaani, Msemaji wa Serikali atujuze

Lissu: Rais Magufuli haonekani kanisani wala mitaani, Msemaji wa Serikali atujuze

Tarehe kama huzu miaka miwili iliyopita, mara kapelekwa india, mara yupo Nairobi yaani ilikuwa vurugu mechi
Wapo memba humu walimtukana Lissu baada ya kutoa dokezo la taarifa sahihi za kuhoji hali ya afya ya Rais wetu, kama kawaida yao wasivyoweza kudadisi, walikurupuka na matusi baadae ikawa kweli.

Nawashauri ktk jukwaa hili kwa uungwana mwombe radhi pia nasi tunaohitaji kupata taarifa watuombe radhi maana walitunyima haki hiyo kwa kutuvuruga badala ya kuendelea kuhoji haki hiyo ya raia kujua halo ya afya ya kiongozi wake.

Cc johnmbatizaji, come, crimea, stroke, nk
 
Kama ingewezekana basi mada hii isipostiwe tena JF

Ila pia inaweza kuwa ni kusudi la Mungu kupostiwa ili tujue kuwa SAFARI BADO, ukidhani umefika au hutakufa unakosea

Lissu aliyepigwa risasi za kutosha yu Hai leo, ambaye hakupigwa risasi hata moja hayupo tena kwenye uso wa dunia

Hili ni Funzo tunakumbushwa
 
Naam wakuu,

Leo ni Jumapili nyingine. Nimezoea kukutana na mnakasha humu JF au kukutana na mabandiko katika makundi sogozi ya WhatsApp yakiambatana na picha yakionyesha Rais alikoshiriki ibada. Mara nyingine hata akipewa nafasi kutoa neno kanisani.

Yupo Dar bado? Leo Machi 7, 2021 amesali wapi? Amepata nafasi ya kutoa neno?

---
Kupitia kurasa ya ya Twita Tundu Lissu amehoji juu ya kutonekana kwa wiki mbili rais wa JMT akiwa kanisani.Pia hajaonekana uraiani, na inashangaza Greyson Msigwa na msemaji wa serikali kutopost taarifa yoyote ya rais akiwa anasali au mitaani kama ilivyokawaida yao.

View attachment 1720084
Lissu alijua njama dhidi ya maisha magufuli.
 
Basi acha nimtete Magufuli kwa hili.

Wenye kanisa lao wameeleza wazi; wanataka watu wachukue tahadhari zote dhidi ya COVID-19, ikiwa ni pamoja na kuvaa BARAKOA.

Magufuli kaweka wazi, kufanya hivyo ni kukosa imani na mungu wake. Hawezi kamwe kuvaa barakoa na kufuata njia zingine zinazotambulika ili kuzuia/kupunguza maenezi ya ugonjwa huo, kutokana na imani aliyonayo kwa mungu wake..

Sasa Lissu na sisi wengine tunataka aende kanisa gani? Akilazimisha kwenda huko alikowapa semina, itamlazimu avae barakoa. ambayo kwake ni mwiko kabisa.


Hiyo ndiyo sababu haonekani kanisani Jumapili.
Njoo usome tena ulichoandika hapa
 
Back
Top Bottom