Ukiwa kiongozi jitahidi Sana kutoongozwa na hisia au chuki. Watu wa Mpira wanajua jinsi ya kumfanya mpinzani awe na hasira ili akose utulivu mchezoni.
Unamkumbuka beki kisiki Juma Nyoso au Forward Mkolofi Diego Costa.
Sio lazma ujibu au ulumbane kila kitu muda NI machache Sana. Ukipita sehemu ukaanza kutumia muda mwingi kuzungumzia ugonvi na tume unakosa nafasi muhimu kufafanua Sera yako ya maendeleo ya watu.
Watu wanataka Sera zitakazoinua Hali zao za maisha. Wafanye Kazi wapate malipo mazuri, mfumo wa Kodi uwe rafiki wanunue na bidhaa kwa Bei nzuri. Mi nilishangaa mzee moja miaka karibu sabini alivyombana gwajima kwa mifano dhahili kabisa juu ya Bei ya sukari kuwa Mara mbili bara kuliko Zanzibar.
Watu wanataka fedha wanayopokea itoshe kuwapatia Nyumba Bora, elimu Bora, Afya bora. UCHAGUZI sio Lele mama watu wanakuja kumsikiliza Sera sio kukushangaa.
Hayo mengine ya tume na wewe pambaneni kwa kifupi tu.
Tumia Lugha nyepesi Sana. Usitufundishe vifungu vya Sheria jukawaani. Sheria inaitaji fast learner kukuelewa.
Nimeshangazwa na misimamo yake
1. Unaulizwa swali la ushoga halafu unapoteza muda muhimu kufafanua vipengele vya sheria kuhusu hilo which is irrelevant kwa wananchi wengi. Angesema next question nimeshalitolea ufafanuzi mara nyingi. Mara sera ya majimbo, vitu vyenye zero impacts to majority of Tanzanians.
2. Anawaita polisi, Magufuli, tume, wajinga kabisa, wapumbavu na waovu. Marais wastaafu wote hawajabaki salama. Sasa ni kweli wanaweza kuwa hivyo. Lakini ili kupata kura hautaji kuongeza maadui. Use decent language, umepewa jukwaa to look presidential, ready for day one to rule elezea utafanya nini zaidi ya CCM.
Kuwe na tofauti na hao unaowatukana.
3.Haki, Uhuru na Maendeleo siyo tu uhuru wa kujieleza, democrasia, uhuru wa kukutana, kufanya siasa, hivyo vitu vitatu pia vinahusu watoto kupata Elimu bure, matibabu, maji safi na salama, kipato halali.
Biashara bila bughudha, kodi (makadilio sahihi) ya ukweli, kutodaiwa rushwa, wakulima kulipwa kwa wakati, kuuza mazao yao popote, umeme wa uhakika, barabara zinazopita mwaka mzima, usafiri wa haraka kama reli, ndege za abiria na mizigo nk.
4. Hakuna haja ya kuwatishia watu utawapeleka The Hague. Kwamba Amsterdam anawaangalia. Nina uhakika kila mtu anajua hivyo
Kwamba UN, USA, EU, AU, SADC, EAC wote wanaangalia.
Angejikita zaidi kuongelea sera, jinsi gani Chadema itayafanya mambo ikipewa dola tofauti na CCM.
Hata kama Tanzania Taasisi ya Urais, TISS, Jeshi la Polisi ni wajinga, sidhani kama Watanzania wengi watapendezwa kumuona Rais akihukumiwa ughaibuni. Kama kuna hukumu ifanyike hapa hapa Tanzania.
Siyo kwenye mahakama inayowahukumu only viongozi wa dunia ya tatu, wakati mauaji ya kutisha yanaendelea Yemen, Syria, Iraq, Libya, Azerbaijan, ukiukwaji wa haki za binadamu unaendelea Saudi Arabia, Russia, China, North Korea, Iran nk.
Rai kwa Polisi waache Chadema wafanye mikutano yao kwa amani, ni muhimu kutowapa hawa wazungu sababu yoyote za kutuwekea vikwazo. Hata kama Chadema wakishinda hiyo 20% -30% (DW) watangazwe. Ni muhimu pia uwe free, fair, transparent and Credible.