Pre GE2025 Lissu: Sijui ilikuwaje CHADEMA tukamualika Rais Samia, ila mbeleni tutaelezana

Pre GE2025 Lissu: Sijui ilikuwaje CHADEMA tukamualika Rais Samia, ila mbeleni tutaelezana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nauliza tu,
Ccm kwenye mikutano yao mikubwa uwa wanawaalika wapinzani na kuzungumza kwenye mikutano yao?
Hususani chadema na act wazalendo?
 
Anachokihubiri Tund Lissu ndio wafuasi wa Magufuli wanakitaka, sababu wanajua siasa hizo zinawafanya waweze kuwafanyia wapinzani kitu chochote na wasifanywe chochote

Actually ukichunguza kwa makini utaona mashabiki wa mwendazake wanamshangilia Tundu Lissu japokuwa hawampendi, wanajua atawapa wanachotaka

..Lissu anahubiri Tume Huru na Katiba Mpya.

..Muungano ameuzungumzia kwasababu umetimiza miaka 60.

..Mbele ya safari anaweza kuzungumzia tukio lingine, lakini hoja ya msingi ni Tume Huru na Katiba Mpya.

..Je, unataka tuamini kwamba wafuasi wa Magufuli wamehamia kwa Lissu kuunga mkono Tume Huru na Katiba Mpya?
 
Wafuasi wa Magufuli wanataka extremism kwenye politics, wanataka siasa za CCM kuwaona Chadema ni adui wa taifa ambaye ikiwezekana auawe kwa manufaa ya taifa na Chadema kuwaona CCM ni adui wa taifa ambao akiuawa ni faida, sio kuonana just kama watanzania walio na mtazamo tofauti wa kisiasa, na ndio siasa ambazo Tundu Lissu amekuwa akihubiri
Hana political maturity wala statemanship yoyote angalau kama mwenyekiti wake, cha kusikitisha ndio viongozi ambao Chadema mnawatala
 
Akiwa mkoani Iringa katika mkutano wa hadhara Lissu amesema hajui ilikuwaje CHADEMA ikamualika mama kwenye mkutano wa CHADEMA maana huwa hawaji wenyewe ni mpaka waalikwe.

Aidha Lissu amewatahadharisha wanaCHADEMA kuwa makini maana kwenye uchaguzi wa ndani ya Chama kuna hela nyingi inatumika ambapo Lissu amesema fedha hiyo ni ya Abdul na Mama yake maana chadema hawana hela hata kufanya mikutano huwa inakuwaga ni shida kwasababu ya fedha ila cha ajabu watu wanapewa fedha kwenye uchaguzi wa ndani.

Lissu ameamua kufanya swala la Uchaguzi wa ndani wa CHADEMA kuwa swala la Umma.
Ngoja inyeshe tuone panapovuja!! 🤣 🤣 🤣
 
Wafuasi wa Magufuli wanataka extremism kwenye politics, wanataka siasa za CCM kuwaona Chadema ni adui wa taifa ambaye ikiwezekana auawe kwa manufaa ya taifa na Chadema kuwaona CCM ni adui wa taifa ambao akiuawa ni faida, sio kuonana just kama watanzania walio na mtazamo tofauti wa kisiasa, na ndio siasa ambazo Tundu Lissu amekuwa akihubiri
Hana political maturity wala statemanship yoyote angalau kama mwenyekiti wake, cha kusikitisha ndio viongozi ambao Chadema mnawatala

..mbona Lissu ametulia ukizingatia mashambulizi na mapigo ambayo amepitia?

..Lissu hajawahi kuhamasisha violence mahali popote, wakati wowote.

..Mimi nadhani tuna tafsiri tofauti ya political maturity and statesmanship.

..Mtu anayehubiri Tume Huru na Katiba Mpya, katikati ya hila, na uhalifu wa Ccm, unaweza vipi kusema haijali nchi na amani yake?
 
Huyu mtu wako anamshambulia Rais Samia kuwa "ameuza" rasilimali za bara kwa sababu ni mzanzibari, wakati maamuzi yalifanywa na baraza la mawaziri na bunge
Anaongea pia mengi akisema yanatokana na Samia kuwa Mzanzibari, huu ni ufashisti
Juzi anadai Samia kuhudhuria kikao cha siku ya wanawake duniani alichoalikwa na Chadema ni kufuru, Samia sijui alipomtembelea hospitali sijui kwa nini hakumfukuza

Huyu mtu ni fashisti na mbaguzi wa kisiasa kama Magufuli, na ndio maana anam miss Magufuli hadi kutaka kwenda kwenye kaburi lake kumuombea, hii ni kuhadaa wananchi waliokuwa vanapenda siasa za kifashisti za Magufuli kuwa upande wake
Huyu mtu ni demagogue
IMG_20230729_131431.jpg
 
Back
Top Bottom