Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi isiwatishe bali ihakikishe uchaguzi unakuwa huru na haki ili kuwe na amani.
Kwanza amewataka wawarudishe wagombea wote wa CHADEMA walioenguliwa katika kinyang’anyiro warudishe ili waende kukataliwa na wananchi katika sanduku la kura. Kura zihesabiwe kwa haki na atakaeyeshinda ashinde kwa haki.
Amesema hayo alipokuwa Mbalizi mkoani Mbeya akiwa safarini kuelekea Tunduma. Amesisitiza ya kuwa bila hayo kufanyika hakutakuwa na amani, kwa maneno yake ‘hakuta kuwa na amani kwenye wizi’.
Ikitokea hivyo amesema watadai haki yao kwa namna wanavyojua. Aidha amesema wasifundishwe namna ya kulia au namna ya kupiga kelele. Kama amani inatakiwa amesisitiza haki itendeke.