gcmmedia
Member
- Jul 19, 2024
- 34
- 75
Mimi namwona Tundu Lisu, mtu imara sana, mwanasheria mzuri, mzalendo wa kweli kwa Taifa lake na mtu mwenye misimamo thabiti asiyeyumbishwa.
Baada ya kumsikia Jana akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA taifa nilijifunza kitu kipya kuwa, pamoja na uzuri na uwezo mkubwa sana alionao, TL siyo kiongozi mzuri kwa sababu ya “ UBINAFSI” aliouonesha katika hoja zake. Kiongozi anayesema “Mimi nita…” atakuwa mbaya sana akiwa madarakani. Uongozi ni “collective responsibility” na siyo “one-man-show”.
Yaliyofanyika katika taasisi ambayo yeye ni Makamu Mwenyekiti hawezi kujitenga nayo. Kujaribu kujitenga nayo ni “udhaifu mkubwa kwake”. Hata akifanikiwa kuwa Mwenyekiti Taifa wa CHADEM, anatakiwa kutekeleza maamuzi ya vikao na wala si matakwa yake. Hoja ikipitishwa kwenye kikao, Mwenyekiti kazi yake ni kusimamia utekelezaji.
Wakati sikubaliani kabisa FAM kuendelea kuongoza CHADEMA, bado sikuridhishwa na TAL uwezo wa kiuongozi. Wanachama wa CHADEMA waendelee kuchukua fomu kugombea Mwenyekiti Taifa.