OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
...tunaendelea
Ingekuwa hoja kama tusingemsema Magufuli kwa mfano, kuna mtu alimsema Magufuli kama mie? Kuna mtu alimsema Kikwete kama sisi? Mpaka Mkapa, mie kesi yangu ya kwanza ni ya Mkapa mambo ya madini mwaka 2002 miaka 22 iliyopita, na za Kikwete ngapi sijui za Magufuli ndiyo usiseme.
Tunamsema Samia siyo kwa sababu ni Muislam tunamsema kwa sababu ni Rais, Urais wake unatuangamiza, matendo yake yanatuangamiza, matendo yake yanatapanya mali za, rasilimali zetu, na kwenye hili tuwe magerezani, tukiwa makaburini tuwe wafu hatutasema, wafu huwa hawasemi, ila tukiwa magerezani tutasema wasitubabaishe na wasitutishe.
Hatuna hoja ya udini, wanaotaka kujificha nyuma ya msikiti au nyuma ya kanisa, wanataka kuficha uovu wao, Wanataka kuficha uovu wao nyuma ya msikiti nyuma ya msalaba, na watu hao lazima tuwaambie msijifiche nyuma ya msikiti wala nyuma ya kanisa tokeni hadharani tuwaseme kwa matendo yenu, na matendo yao ni mabaya kabisa.
Mnafahamu mmeletewa pikipiki ngapi? Meziona, mkoa huu umeletewa pikipiki 700, na zote zimeandikwa SSH 2025 na zina picha yake, na kila mkoa umepata hizo pikipiki hizi kwa wastani 700, piga hesabu kwa mikoa 26 ya Tanganyika mara pikipiki 700 ni pikipiki 18,200 pikipiki siyo za Serikali, siyo za CCM Ni za Samia Suluhu Hassan 2025 ni za Mama Abduli.
Nyie watu wa Singiga, kuna yeyote anajiuliza huyu mama atakuwa amepata wapi hela, ya kununua pikipiki 18,200 na kuzigawa bure, hiyo hela ameitoa wapi? Mnafikiri amezitoa wapi, amepambwa nchi nzima na mabango, hakuna vitu gari kwa wale wanaojua biashara kama haya mabango, hakuna barabara utapita usikute mama amekaa hivi au vile, hayo mabango hayajawekwa na CCM wala Serikali, yangewekwa na Serikali kungekuwa na bajeti imepitishwa bungeni, ndani ya miaka 3 ya kuwa Rais hizo fedha amezitoa wapi?
Hasa ukizingatia bandari zimekwenda, hekta milioni 8.9 zimekwenda wamasai wamefukuzwa umasaini, Ngorongoro loliondo, mnafikiri hizi hela amezitoa wapi? Mnafikiri amezitoa wapi Watanzania?
Pia soma: Kuelekea 2025 - Baada ya kugawa pikipiki za Samia, inadaiwa pia kuna Helcopta na Magari 400 kwaajili ya Kampeni za mwakani