Pre GE2025 Lissu: Wasijifiche nyuma ya msikiti, waje hadharani tuyaseme matendo yao maovu

Pre GE2025 Lissu: Wasijifiche nyuma ya msikiti, waje hadharani tuyaseme matendo yao maovu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kuna watu hapos siku za nyuma walitaka kutuaminisha kwamba Dr Samia tusimsema kwa sababu ni Mwanamke na Kwa sababu ni mwislam.
yaani ukipinga mambo yake tu unaambiwa hupendi waislam au wanasema eti unamsema kwa sababu ni Mwanamke.
Ukiona mtu anakimbilia mambo ya udini basi jua huyo amefirisika kisiasa
 

...tunaendelea

Ingekuwa hoja kama tusingemsema Magufuli kwa mfano, kuna mtu alimsema Magufuli kama mie? Kuna mtu alimsema Kikwete kama sisi? Mpaka Mkapa, mie kesi yangu ya kwanza ni ya Mkapa mambo ya madini mwaka 2002 miaka 22 iliyopita, na za Kikwete ngapi sijui za Magufuli ndiyo usiseme.
Hii lugha ni nani asiyeweza kuielewa!
Hata ukiwa CHAWA mara mia huwezi kukosa kuelewa lugha rahisi kama hii.

Sasa tuendelee kusikiliza, hadi hapo 2025, tutakuwa tumefuzu katika uelewa.

Na kama Omar Bongo, jamaa walikataa uhuni, kutakuwa na sababu zipi za sisi hapa tukubali uhuni?

Gabon siyo nchi iliyowahi kupita ndani ya tanuru la moto mkali kama tulivyo wahi sisi enzi za Mwalimu Nyerere. Uelewa wote ule tuliokuwa tumekuwa nao enzi zile, wote tumeupoteza kabisa?
Sidhani, tumeona mwitikio alioupata Magufuli kwa baadhi ya mambo mazuri waliyoyapenda wananchi, na hadi leo ni kielelezo hicho hicho kinachwasumbua hawa wanaotulangua sasa hivi.

WaTanzania watakataa kuuzwa.
 
Hizi zinaitwa Spana
Huyu mama na watu wanaomwezesha siyo watu wa "STAHA" hata kidogo.

Katika juhudi zao za kuendelea kuwa madarakani wanasahau kabisa kwamba waTanzania nao wanazo akili za kufikiri na kuona matendo yasiyostahili wananchi kufanyiwa.
Pengine hii ni dharau na kiburi kinachotokana na majivuno ya kuwa na pesa, na kumwona asiyekuwa nazo kama ni nusu binaadam.
Huyu mama na marafiki zake wamekosa simile kabisa, hawana aibu wala soni kufanya mambo ya aibu.
WaTanzania hawawezi kununuliwa kama bidhaa.
Hawa ni watu wenye kujivunia utu wao. Hawa watu wamechanga damu zao na kutoa maisha yao kuwachangia waafrika wenzao waliokuwa chini ya makucha ya ukoloni.
Huyu mama anasahau na kudhani anaweza kuwanunua kwa vipande vya pesa?
 
Back
Top Bottom