Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Sio majaji tu hata huyu bwana hapa akiongea utajificha mbali kabisa inasikitisha.
Sikiliza kidogo uone kwanini Lissu ana point ya msingi. Aibu kishenzi.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwamba I am a politicians?
Hatari mzee baba katisha
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwamba I am a politicians?
Hatari mzee baba katisha
Watoto wa darasa la kwanza hawafanyi makosa kama hayo; “I am a politicians”!
 
Umeona aibu ya taifa kwenye hiyo video? Sijui nani alimchagua mtu huyu kuwa kiongozi!
I am a politicians,I don't want to take this time as to say so many political words, simple and clear it's only congregations to you to the university corridor... Columbia University to a good assistance we are getting to this hospital..
[emoji848][emoji848][emoji848]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwa hiyo yeye anakijua hicho Kiingereza kama Majaji na Mahakimu wetu hawakijui?
Lissu anakijua ndo maana kasema hivyo na si mara moja kasema hivyo..ukitaka kujua hudhuria kesi za lissu uone anavyowatesa majaji kwa ngeri
 
Nimekwambia kiingereza ni juhudi ya MTU binafsi,siyo lazima majaji wakijue vizuri kuliko MTU mwingine
Ni juhudi ya mtu binafsi ndiyo lakini kwa jaji wa mahakama kuu lugha ya english is one of the tools of work ambayo ni lazima ajue kuitumia. Sheria nyingi, miendenendo ya kesi na hukumu vyote vinahitaji mtu mwenye uelewa sahihi wa kiingereza. Alichosema Lissu ni kweli na just ameeonyosha jinsi wataalam wetu kwenye sekta mbali mbali walivyochaguliwa huku hawana vigezo.
 
lissu anajifanya anajuwa kila kitu kuliko wenzie wote hana lolote hana alijualo ni kujitapa tu kusiko na msing
 
Kujua kiingereza siyo kujua kila kitu ,na wala si lazima kukijua chote
 
Hivi kwanini JF hakuna Dislike button..!? [emoji848] Napenda hii feature iwekwe kama ilivyo kwenye platforms zingine kwa maana kuna watu huku wanakera na wanapinga tu kila kitu...
 
Fikiria tu muda Mtu anaotumia kujifunza Kiingereza ajifunze na aelewe miaka 4 tu ya Sekondari anakuwa hajaelewa Kiingereza sawa sawa na anakwenda tena form 5 na 6 bado anakuwa vilevile, kwa kifupi Watu wetu hawajui Kiingereza.
Kujua Kiingereza ndio usomi? Basi sawa!
 
Mkuu Chige umemaliza yote. Na zaidi alichokuwa anamaanisha Lissu ni kuwa english ni moja kati ya nyenzo za kazi ambazo majaji wetu wanatakiwa waifahamu. Mazingira ya kufanyia kazi mahakama kuu na jaji kwa ujumla yanategemea sana lugha ya kiingereza hivyo kama jaji hakijui vizuri ni shida na hataweza kutenda kazi vizuri. Hii inaonyesha kuwa jinsi tunavyoteua majaji wetu kuna walakini. Na sishangai sana kwani mambo ya uteuzi hapa Bongo siku hizi yameacha kufanyika on merit na badala yake yanatumia vigezo vya milango ya nyuma. Na hii siyo kwa upande wa majaji tu bali hata kwenye mainjinia, madaktari nk utakutana na wahitimu ambao uelewa wao ni zero kabisa. Unaweza kuamini kuna mtu amemaliza Phd na kuandika thesis za kiingereza lakini sasa hivi ukimwambia aandike insha ya karatasi moja kwa kimombo hawezi? Hapa kuna tatizo zaidi ya uelewa wa lugha...
 
Nataman ile interview ya ke ya marekan alikuwa anagumimia kweli kingereza huyu lisu Leo anataka kujifanya anakijua hahahahaha
 
Ni kweli anakijua au hakijui kiingereza,tuanzie hapo.Au ww ndio hao lawyers nini, si kwa povu hili.bila shaka unaweweseka.Pole mkuu.
 
You're right, nilishindwa kuelezea alichomaanisha Lissu kwa sababu sijasikia full script ya alichosema ila tu niliona tweet inayoelezea TL kuzungumzia umuhimu wa kuwa na mjadala juu ya sera ya lugha!

Na kwa kuangalia tweet ile, wala si kwamba alikuwa ameongea kwa namna ya kukashifu bali it's more about a concern, na akitokea wa kupinga concern ya aina hiyo basi atakuwa na matatizo kwa sababu ni kweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…