Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Hahaha weka records hapa, intellect haisemwi na maneno, weka hapa chochote aidha thesis yake au publications, ...
You are still suffering from "diploma disease". Some concepts have to be taken judicial notice of from daily experience and public checkability!
 
Hatuendelei na kupata wasomi wakutuondolea matatizo yetu hadi tukubali kama kiswahili ni rahisi kufahamika kuliko lugha zengine.

Kiengereza kiwe ni lugha ya pili, sio ilivyo sasa hadi sheria za nchi kwa lugha ya kigeni.

Hili tatizo la kukumbatia kiengereza ni la colonial mentality.
 
Yeye amesomea hapa mpaka chuo kikuu kiingereza amekijuaje akishajibu ndio tutajua tatizo ni lugha au walimu wanaofundisha
 

Umeandika nini wewe?hivi umemuelewa Lisu? Acha kukurupuka soma alichosema Lisu kisha kielewe.mbona Mataga mnakuwa mbulula kiasi hichi?Acheni kuendeshwa kwa mihemko.
 
Mpaka sasa list yangu ya wenye PhD wasiojua kingreza inasoma 2 na naendelea kufanya utafiti kuwabaini PhD holders wengine lugha gongana.
Usimsahau huyu bwana anaongoza.
 

Attachments

  • IMG_5105.MP4
    690.2 KB
Lisu yupo sawaaaaah kabisaaa
 
Nimekwambia kiingereza ni juhudi ya MTU binafsi,siyo lazima majaji wakijue vizuri kuliko MTU mwingine.
Ukisema ni juhudi unazungumzia st. Kayumba bila shaka. Na kuna watu watakushangaa...

Tutafute hela tu. Walau watoto wetu wasome shule nzuri.
 
Wanatumia lugha zao kufanyia nini mkuu?
Mbona mnakuwa wajinga kiasi hichi, mnatia aibu sana kwa kweli. China wanatumia lugha yao ya taifa kwa kufundishia na shughuli nyengine zote. Lakini lugha za kigeni zinasomeshwa kama masomo tu na wenye interest wanajikita huko kwenye lugha za kigeni.
Sisi tunajifanya tunaipenda sana lugha yetu ya taifa halafu tunapofika form one tunaanza kutumia English kama medium of instruction. Kwanini tusiwaige hao wachina na wajerumani tutumie kiswahili mwanzo nwisho na English isomeshwe as subject na mwenye interest zaidi ajikite huko. Lakini leo mtu anatoka la saba anaenda form 1 anakutana na lugha ngeni inabakia kukremu tu. Ndio maana mtu anamaliza PhD hajui English alikuwa anakunywa madude na kukopi Thesis za watu huko. Ukiongea unaonekana sio mzalendo wakati ukweli unajiojionyesha wazi. Tuchague moja tu tuanze nayo kindergarten hadi PhD.
 
Si yule anayesimamia watu kuelimika
[/QUOTE
95% Wait while the system is decoding your message................................................................
..................
100% decoding completed]
 
Nishawajua, yule bidada pamoja na yule stone
95% Wait while the system is decoding your message................................................................
..................
100% decoding completed
 

Kwanza pole sana kiongozi kwa kukosa huo ufadhili wa masomo, halafu hapa umeibua jambo jipya tena hapa kuhusu hilo la elimu huko Kasulu. Naona umekuja pale pale kwenye ukweli kuwa tatizo ni mtaala tu na sio lugha. Mwalimu anatumia lugha ya Kiha kufafanua zaidi kwa sababu mtaala haujatoa nafasi ya mwanafunzi kuweza kujifunza kwa kutafakari na kujihusisha na mazingira yake na wakati uliopo.

Halafu nitakuuliza kitu, shuleni sekondari kunakuwaga na midahalo ya kiingereza na vibao vile vya kuvaa shingoni kwa wanaoongea kiswahili shuleni. Sasa wakati unasoma sekondari vitu hivyo havikuwepo? Ulikuwa unachangamana vipi na watu? Je ulikuwa unaona umuhimu wa lugha ya kingereza? au kwako ilikuwa bora tu upate marks darasani? Je Lissu yeye kingereza alikifahamia wapi? kwenye shule hizi hizi na mifumo hii au alisomea mtaala wa nje ya nchi? Juhudi Juhudi Juhudi.. ndio ufunguo wa haya yote. Wako watoto wa Kayumba kibao tu na wanaongea hicho kingereza vizuri bila shida.
 
Kwani ili mtu ajue lugha kwa ufasaha inabidi ajifunze miaka mingapi? Kwani mtu hawezi kujifunza lugha peke yake akaielewa hadi iwe amejifunza wakati anasoma masomo mengine kama science katika lugha hiyo hiyo?

Hivi ukimchukua mmalawi aliyeishia darasa la nne au mkenya darasa la nane mbona wanajua kiingereza kwa ufasaha? Kuanzia form one hadi form six na chuo kikuu ni miaka isiyopungua 9 hadi 11 kwa wenye bachelor degree, je hiyo ni miaka michache ya kujifunza lugha? Hapo hujajumlisha miaka 7 ya primary na pengine miwili au mitatu ya chekechea ambapo mtu huyo alijifunza english.

Tatizo lenu kubwa mashabiki wa Lissu mnamuona kama msahafu yeye ndiye anajua kila kitu. Duniani mtu wa hivyo hayupo.

Ukitaka uwe vizuri katika hoja kwanza liendee jambo objectively sio subjectively. Pili jaribu kuutafuta ukweli nje ya boksi kwa kutumia knowledge yako hata kama ni ndogo huku ukiangalia facts mbalimbali zilizo mbele yako.
 
Labda jiulize kwanini wakoloni walipotawala Tanganyika na Zanzibar, waliamua kujifunza kiswahili badala ya kutubadili tukazungumza kiengereza. Nadhani uwo ni mfano rahisi tuu utagundua kuna tofauti baina ya Kenya na Malawi au izo nchi zengine kama Nigeria, Kameroon n.k. Hizi nchi haziko katika lugha moja kuu, hivyo kuwabadili wakazungumza fr/en ni rahisi na inawezekana kwa urahisi.

Nadhani tukitaka kujifunza tujaribu kutazama nchi zilizoendelea, mifano mizuri itakuwa EU (germany, france, portugal n.k). Kwa Asia Russia, China, Japan n.k. Utagundua wote wana wasomi na wanasayansi wazuri lakini si lazima kuwa wanazungumza au wamesoma kwa English.

Pia tofautisheni baina ya kujua english kutumia kwa mawasiliano, na kutumia english kama 'instruction language' yaani lugha ya kufundishia. Hoja ya msingi ni kuondosha english kama ni lugha ya kufundishia/kusomeshea. Hapa nadhani tumechemsha, haihitaji tochi kiswahili kinafahamika vizuri zaidi kuliko english hususan kwa level za chini ya University. Hata University inaweza kuwa vitabu tuu ndio vya English, mitihani ikawa kwa kiswahili na vitabu pia vya kiengereza.Vyote inawezekana na mifano kibao maeneo niliyoainisha hapo juu.
 
Mkuu shule nilizopita ni Mazengo,tukahamishwa baada ya kugeuzwa kuwa st John university,nikaenda Moshi tech,nikaenda kibaha high school na baadaye UDSM!Huko kote nilikopita hakukuwa na hayo masuala ya vibao wala speak English!Kidogo nilikuta msisitizo Kibaha!
Mkuu ukiona asilimia 90 ya wanafunzi wanaopita Kayumba wanamaliza vyuo na kiingereza kibovu au kisichoridhisha,jua kuna tatizo!
Hao akina Lissu ni kati ya wachache walioweka pengine jitihada za ziada,pia masomo yake ya sheria yakamsaidia maana kuna kujieleza kwingi na case zinakuwa kwa lugha ya kiiingereza!Hiyo inawapa advantage wanasheria ya kujifunza kiingereza kwa lazima!Mchepuo kama wa uhandisi ni majanga,huko kiingereza ni technical language ya field husika na unafaulu vizuri tu!Upewe mike ujieleze hata dakika 10,majanga!
Bado narudia,medium schools zinafanikiwa sana,hata ambao tumesoma nao unaona kabisa huyu katoka sehemu fulani tofauti na mimi japo kufaulu mnafaulu wote lakini yeue anakuwa na kitu cha ziada,lugha!
Tunaweza kukawa na tatizo kwenye mitaala,lakini hili la lugha pia halikwepeki!
Mimi napendekeza kiingereza kama lugha ya kufundishia ianzie msingi,japo tutakuwa na kazi kubwa ya kufanya maana hata walimu nao hali ni ile ile!Mfano kipindi cha Corona kuna utaratibu wa walimu kwa kushirikiana na Tv stationa walianzisha wa kufundisha kupitia luninga!Mmmh kuna siku nilijikuta naangalia ufundishaji,aisee nilijikuta aibu naona mimi nikabadili na channel!
Hoja ya Lissu ni ya msingi sana,chama kitakachochukua hatamu naomba waichukue na iwe kwenye agenda za elimu!Uanzishwe mdahalo utakaoshirikisha wadau wa elimu kwa kuzingatia na uzoefu kwa majirani zetu kama Kenya na Uganda tuamua tunashika njia ipi once up for all!
Hapa tulipo tumekwama,tusipuuze hoja hii!Tuichukue na ifanyiwe kazi tupate majibu
 

Sasa wewe umesema huko Kasulu shuleni mwalimu anatumia Kiha ili kufafanua masoma yanayotolewa kwa kiswahili. Kiswahili hiki ambacho ndio lugha ya Taifa watu wanashindwa ndio ianze kingereza kuanzia shule ya msingi? Mbona unataka kuchekesha mkuu? Umeshasema mtu akiweka juhudi hicho kingereza anakijua vizuri bila kujali amesomea wapi hivyo tukubaliane ambae kingereza kinampiga chenga ni mzembe na hakuweka mkazo katika kukijua kiingereza.
 
Nafikiri hoja yangu hujaielewa vizuri.

Lakini kwa kutumia mifano ya nchi ulizozitaja, je raia wake hawajui english? Hao wataalam toka nchi hizo waliosoma kwa lugha zao wakija huku kwetu mbona wanazungumza english fasaha?

Mnaweza mkawa na lugha kuu lakini bado mkawa mahiri vile vile katika lugha zingine kama English au french.

Nchi za kiafrika zinazozungumza french kama Rwanda sasa wameenda mbali zaidi, primary wanajifunza french wakiingia sekondari wanajifunza pia english na wakimaliza wanakuwa mahiri katika english pia. Sasa mtu huyo mnakutana naye katika soko la ajira anajua french na pia anajua english kuliko wewe ambaye ulitakiwa umzidi.
 
Ukiona zaidi ya 90% wanakumbana na changamoto hiyo,basi jua kuna tatizo hasa la msingi linalohitaji utatuzi!
Wangekuwa wachache ndio wanakuwa wabovu,basi tungesema ni uzembe wao!Lakini tunakwepa nini,ni ukweli ulio wazi kuwa watanzania wengi wanamaliza vyuo hawajui kiingereza vizuri kile tu cha kuwasiliana!Fikiri tu PhD holder,Dr Magufuli kiingereza ni kasheshe,bado unaona ni uzembe?Kwanini huoni ni tatizo la mfumo wa elimu?
Mkuu hujaelewa mfano wangu,nimesema mwalimu alikuwa analazimika kutumia kilugha ili wanafunzi waelewe!Mwisho wa siku mpaka wanamaliza darasa la 7,unakuta mtoto kashaadopt na anajua kiswahili!Hii ni kwasababu lugha ya kufundishia ni kiswahili na anajikuta yuko mazingira ya watu wanazungumza kiswahili shuleni,ndio maana akaweza kujifunza taratibu!Hapo inamaana hata tungeweka mazingira ya kiingereza shuleni na ikawa lugha ya kufundishia,mtoto angeweza kuadopt na kujifunza kiingereza!
Tuchague moja,kama ni kiswahili basi na iwe hivyo kuanzia msingi mpaka chuo kikuu na kama ni kiswahili iwe hivyo msingi mpaka chuo kikuu!
Hapa tulipo tupo katikati!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…