Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Kusema tu ni colonial mentality haisadii. Tatizo watanzania wengi tunapinga colonial mentality kwa maneno wakati maisha yetu yote yamejengeka kwenye hiyo dhana. Kujitegemea kwa kutumia lugha yako ni jambo linalohitaji commitment ya hali ya juu ambayo hawa wanasiasa wetu uchwara hawana. Wao wamebakia kung'ang'ania madaraka tu na kuabudiwa kama miungu japo kuongoza kumewashinda.
 
Naunga mkono msimamo wako. Tanzania tulichokosea ni kujaribu kutumia lugha chotara e.i. kiswahili na kiingereza kufundishia. Na mbaya zaidi ikatokea hata wale wanaostahili kufundisha lugha hawajui lugha yenyewe. Sasa hivi wananchi wengi hawajui kuandika kiswahili na kiingereza ndiyo kabisa. Mbona Kenya kiingereza chao ni kizuri tu. Hata ukiangalia vikao vyao chini kabisa wanazungumza kiingereza ambacho Bunge letu haliwezi kutumia.
 
Umenena vyema Kiongozi
 
Natamani ni like mara "Mia Oja"
 
Mnapo Mnaposema Lissu anajua kuongea Kiingereza mnamaanisha nini?
 
Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani Muingereza anaongea Kiswahili kama Mtanzania?
Sawa ila sio lugha inayotumika kwenye kuendesha mambo kikatiba! Documents nyingi za kiserikal huandaliwa kwa kingereza na kama unabisha subr uletewe nots ya mahakama ndio utaelewa zaidi kuwa pombe si chai
 
Nafikiri nyie ndio walengwa haswa wa hii mada kwani inaonekana lugha ya kufundishia imekuathiri vibaya kiasi kwamba hata reasoning inakuwa ndogo.

China imefika hapo ilipo kwa sababu ya watu wake kutia bidii katika kujifunza kiingereza na ndio lugha ambayo imewasaidia katika kukuza Export Economy yao.

Ebu ingia kwenye Website ya Alibaba ujaribu kuagiza bidhaa toka China uone ni lugha gani wanatumia kisha ndio urejee humu na hizo hadithi za abunuasi.
 
Tuboreshe kiingereza kwenye mfumo wa elimu; kuacha kutumia kiingereza kuna hasara nyingi kuliko faida. Sisi tuongee kiswahili chetu, tujifunze kichina, tujifunze kihindi, kirusi na nyingine zenye faida kwetu kiuchumi na kijamii. Tanzania sio kisiwa

Yeye Tundu zile kazi anazowafanyiaga Mabeberu zinakuaga kwenye lugha gani?
 
Wakala wa beberu huyu! Mbona walipanda ndege wakaja hadi huku kuongea na jiwe kuhusu makinikia! Wajifunze wao kiswahili acheni ukoloni mamboleo! Lissu hapati kura ng'ooo
 

Ukweli tu ni kwamba lugha ni commitment, hata ukifikisha miaka 70, ukijifunza utaweza na utaelewa tu. Halafu kama unasema mtoto ana adopt kiswahili huko shuleni kutoka kwenye kilugha sasa mbona anashindwa ku adopt hicho kingereza kwa miaka 6 shuleni? Kitu ukiona umuhimu wake utajifunza na utaweza tu. Tukubali tunakauzembe flani.. halafu unaweza kuona kingereza cha mtu flani ni kibovu ila wewe binafsi hata huwezi kuongea kingereza kwa dakika tano mfululizo. Ndio tulivyo watanzania. Kuchekana kwingi wakati wote wabovu tu na ndio maana tunabaki kulalamika tu hapa. Lugha ni kujifunza kwa kujizoeza kuongea mara kwa mara. Sasa kama mtu anaogopa kuopngea kisa atachekwa bhas huo ndio ujinga wenyewe. Practice makes perfect. Kingereza ni lugha tu kama lugha nyingine.. sio chanzo cha maarifa au uelewa mkubwa kielimu.
 
Kwa hiyo kuwa msomi ni kujua kingereza?

Hata yule beberu wake akisikia hivi ataona aibu sana

Sidhani amezungumzia usomi. Usomi ni kiwango cha ufahamu. Anazungumzia lugha na jinsi kutoamua kwetu - kunababaisha uelewa wa lugha! Beberu unayemtaja hana kigugumizi kwenye uamuzi wa lugha ya kufundishia na wengi husoma kiingereza kwa sababu za kujumuika na mataifa mengine!!

Na sisi tunaweza kusema tutumie kiingereza kwa mawasiliano lakini lugha ya kufundishia toka elimu ya msingi hadi chuo kikuu iwe ni kishwahili. Jambo hilo hatujafanya. Kwa ukweli kabisa, ni rahisi sasa kubadilisha elimu ya msingi ikatolewa kwa kiingereza kuliko kubadilisha elimu ya juu kuwa kiswahili.
 

..story yako imenigusa sana.

..nili-experience something similar to what you did in school.

..asante kwa ujasiri wako wa kuelezea changamoto ulizozipitia.

..unawazungumzia malaki, kama siyo mamilioni, ya waTanzania wenzako.
 
Umeelewa hoja yangu lakini?Mimi siko hapa kubishana bila mantiki!Jaribu kufikiri kabla hujaandika!
Nimekuuliza swali ambalo mara zote unalikwepa!Huko shule za English medium kwanini wanafanikiwa sana?
Nikueleze tu,mtoto mdogo anakuwa na nidhamu!Unapoweka standard ya lugha ya mawasiliano kuwa ni kiingereza,hata wenzake wakimsikia anaongea lugha tofauti watamsema kwa mwalimu!So hiyo inajenga mazingira ya wanafunzi kujitahidi kuongea kiingereza!Tofauti na huku form 1,speak english inakuwa geresha tu pale mwalimu anapokuwepo!Akiondoka kila mtu anaendelea na time yake!
Lakini pia kukifanya kiingereza kuwa lugha ya kufundishia kunawafanya watoto waadopt mapema!
Halafu jambo lingine ni kuwa hapa sisemi kuwa kiingereza sijui ndio maarifa au nini!Ninachosema tuchague njia moja,kama ni kiswahili iwe kiswahili,kama ni kiingereza iwe kiingereza!Ijulikane moja!Hapa tulipo tumekwama,hilo lazima tukiri!
Ninachoona hoja hii inapingwa kwasababu za nani kaileta na kaileta wakati gani!
Hilo ndio tatizo kubwa,siasa mbele kwa mbele hata kwenye mambo ya msingi ambayo tungeweza kujadili bila kuwa na mihemko ya kisiasa!
Mkuu ukiwa na pesa ingiza mtoto wako shule za maana,hizi kayumba unamtengenezea mwanao ugumu huko mbeleni!
Mimi nimejipanga kuhakikisha mwanangu hashindwi kutimiza ndoto zake kisa lugha!Ashindwe kwa sababu nyingine lakini si lugha!Nahitaji mwanangu aje kuwa na confidence akiwa anafanya interview,ashindwe kujibu swali kwa ujinga wake na si kwasababu ameshindwa kulielewa swali au amelielewa ila kuongea alichonacho ndio changamoto!

Hao viongozi wote,watoto wao wako kwenye shule nzuri!
 
Mnapo
Mnaposema Lissu anajua kuongea Kiingereza mnamaanisha nini?
Mjadala hapa ni jinsi baadhi ya majaji wanavyoshindwa kuimudu lugha ya kiingereza ambayo ni moja ya nyenzo zao za kazi. Lissu alitoa angalizo tu (siyo Lissu tu ila wengine tumeshaliona hili tatizo tangu zamani) jinsi baadhi ya majaji wanavyotia aibu. Kiingereza siyo lugha yetu na hatuwezi kukijua sana ila kila level ya elimu mtu anayofikia angalau inatakiwa i-reflect utendaji kazi wake.
 
Ahahahahahahahahh! Hivi unajua George Bush alikuwa hajui kuongea Kiingereza? Ilimzuia kuwa Rais wa Taifa kuwa duniani? Ahahahahahahah!!
 
Ahahahahahahahahh! Hivi unajua George Bush alikuwa hajui kuongea Kiingereza? Ilimzuia kuwa Rais wa Taifa kuwa duniani? Ahahahahahahah!!
Hivi ukiitwa idiot utalalamika? Mbona unaongea vitu vya kijiwe samli hapa! Anyways niachane na wewe kwa sababu mijadala kama hii siyo kwa kila mtu.
 
"Yes you know me sometimes photocopy together, sijui nini na nini pilot standard"........bora kiswazi tu wazee
 
Hivi ukiitwa idiot utalalamika? Mbona unaongea vitu vya kijiwe samli hapa! Anyways niachane na wewe kwa sababu mijadala kama hii siyo kwa kila mtu.
Ahahahahahahahh! Huwezi kujibu hoja kama hii. Unafikiri aliyewaita nyumbu alikosea? Ahahahahahahah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…