Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Umeelewa hoja yangu lakini?Mimi siko hapa kubishana bila mantiki!Jaribu kufikiri kabla hujaandika!
Nimekuuliza swali ambalo mara zote unalikwepa!Huko shule za English medium kwanini wanafanikiwa sana?..

Kumbe huwa wanaongea kingereza wakati mwalimu yupo ila akiondoka ndio wanaongea kiswahili? sasa hiyo ni kwa faida ya nani? Kwani ndio wanajua umuhimu wa kukijua hicho kingereza baada ya kumaliza chuo? mbona hawaweki jitihada ya kukijua kingereza wakati wako shule? kutaka kukijua kingereza wakati wa usahili ni sawa na kusoma zima moto je ndio maisha yetu hayo shuleni?

Mbona shule za kayumba ndio zipo top ten kwa wingi kuliko hizo medium school? au hufatilii na kuona hilo? Halafu pia mbona huongelei wanaofanya vibaya shule za msingi ambako ni kiswahili mwanzo mwisho? hata kuandika sentesi hawawezi, hata miandiko yao tu haieleweki nao pia tatizo ni lugha ya ufundishaji?

Sijawahi kuwa mtu wa siasa mkuu, wala sizielewi siasa za bongo.
 

..Nikisema Mwalimu Nyerere alikosea ktk hili nitakuwa namvunjia heshima?

..kwasababu kiswahili kilikuwa kimesambaa kila mahali, na wanafunzi walikuwa wanajifunza kiingereza bila matatizo.

..angalia kizazi cha wasomi wa miaka ya 60, 70, na 80. wanamudu lugha za makabila, wanaongea kiswahili murua, na kiingereza wanakizungumza bila matatizo.

..Nadhani serikali ya awamu ya 1 ilichukua huu uamuzi na athari zake tunakabiliana nazo leo ktk serikali ya awamu ya 6.
 
Mimi sizungumzii matokeo ya darasani,uwe unaelewa hoja iliyoko mezani ni nini!Hapa hoja ni uelewa wa lugha ambayo inafundishwa ili mtu aweze kuimaster!Suala liliko wazi ni kuwa mfuko umefeli kuzalisha wanafunzi ambao wako competent kwenye lugha ya kiingereza!Hii ni kutokana na ukweli kwamba asilimia kubwa wanakuwa wabovu!Na unapoona kundi kubwa linapata changamoto kama hiyo,basi tatizo lipo kwenye mfumo moja kwa moja!Ndio maana nikasema shule za english medium wanafanya vizuri kwenye eneo la kuimudu lugha ya kiingereza!Hapa sizungumzii matokeo ya mtihani!Kwanini serikali isiige mfumo huo?
Sasa labda hoja iwe je,lugha ya kiingereza kutumika kama lugha ya kufundishia ni muhimu?Wakati wanasiasa wanajaribu kukurubuni kuwa tunakuza lugha yetu,wao wenyewe hawajachukua hatua!
1.Mahakama inaandika hukumu kwa kiingereza!
2.Bunge linatunga sheria kwa kiingereza!
3.Serikali inaingia mikataba kwa kiingereza!
Ukiangalia ni kama tumekwama na tuko katikati,hatueleweki tunataka nini!
Bado nasisitiza hoja ya Lissu ina mashiko sana kwa upande wangu!
 

Mkuu, kama swala ni kuwa competent na kuimudu hiyo lugha ya kingereza ni simple tu. Kufanya mazoezi ya kuzungumza mara kwa mara na kujisomea machapisho mbali mbali ya lugha hiyo. Nimekwambia kuna watu hata shule ya msingi hawakumaliza ila wanazungumza kingereza vizuri tu. Ni kwa sababu waliweka juhudi na kutambua wanataka nini.

Shida ni mfumo wa elimu na mitaala, inafanya wanafunzi kukariri zaidi kuliko kuelewa. Hii pia inachangiwa na mbinu mbovu za ufundishaji. Lugha sio ishu, ila content ya unachofundishwa vile unakipokea na kukihusianisha na mazingira na maisha ya kila siku ndio changamoto.
 
We jamaa aisee kichwan kumejaa kamasi tupu...EMBU PENGA HARAKA...HALAFU NJOO USOME TENA UNAWEZA KUMUELEWA LISSU
 
Aisee,wahitimu wanapaswa wamalize wakiwa competent kwenye lugha ya kiingereza!Kama haiko hivyo,ndio tunataka mwarobaini wa hilo kupitia mfumo rasmi!Sio uniambie kila mtu akapambane anakojua na kwa namna yake ili ajue lugha,huko ni kukwepa majukumu ambapo shule zetu zilipaswa ziwe jawabu!Utakuwa unamtania mwanafunzi anayechukua sayansi eti aache kusoma Mechanics aende kusoma vijarida kujiweka sawa kwenye lugha!Hilo haliwezekani na ndio maana nasema madarasa ya awali ndio sehemu sahihi!
Nakukumbusha tu,jipange mwanao umsomeshe shule nzuri za awali ili huko mbeleni asijepata tabu!
 

Mbona mimi sijapata tabu na nimesome shule hizo hizo? Halafu ona unavyo kariri..kwamba mtu wa uhandisi wa magari asisome machapisho ya kingereza? Kwamba mechanics ni robot ajue maswala ya ufundi tu? Vipi kuhusu masoko na usimamizi wa biashara? Umeshaona sasa shida ni mfumo na mtaala na sio lugha sio?

Mbona wanafunzi wanakwepa wajibu wao kutumia kingereza kwenye mijadala shuleni na vibao vya kuzungumza kingereza kutumika? Hivi huoni ni aibu kusema umepita shule miaka sita kwa kufundishwa kwa kingereza halafu useme hujui kuwasiliana kwa kutumia kingereza? Huko shuleni ulikuwa unasoma vipi na unasoma nini?
 

Lissu ana ugonjwa wa "phobia" ya kitaaluma (professional phobia) kwa kuwa kwenye kampeni zake anasahau kuwa hayuko mahakamani bali jukwaa la kisiasa kueleza Sera za maendeleo za chama chake, kwa kugha rahisi.

Kwa mfano ulioutoa Mkuu Return Of Undertaker, ni nadharia inayohitaji wataalamu walioobea kwenye tasnia/sekta ya elimu, kujadili mbinu sahihi za kutoa elimu (delivery modes)
 
Hata hujanielewa!Ninasema hivi,hicho kiingereza ambacho wanahitimu nacho ni cha kuombea maji!Au unadhani ninaposema hawako competent ni kwamba hawajui kabisa kiingereza?Sio hivyo,ndio maana nikakupa mfano wa Magufuli ambaye ni PhD holder na thesis yake amefanya kwa kiingereza lakini bado lugha inampiga chenga pakubwa!
Niliposema Mechanics nilimaanisha topic moja A level kwenye physics,hii ni topic ndefu na ngumu na inahitaji muda sana!Sasa ndio hapo nikasema mtu unachukua PCM,unapata wapi luxury time ya kusoma hivyo vijarida kujifunza kiingereza?Fanya research kwa wanafunzi hao uone kama wana hiyo luxury!
Mimi bado naona muda sahihi ni kuanzia chekechea na si sekondari!

Naomba ukinijibu hii comment nijibu kwa kiingereza ambacho unajisifia kukimudu huku ukiwa umepita saint kayumba!Naomba sana ufanye hivyo!
 
Mkuu

Mh Tundu yuko sahihi

Mifano halisi IPO.. Mf font fed, lait track
Umenifanya nicheke usiku huu nikikumbuka hii Font fed aisee Kiingereza kigumu jamani mwacheni Lissu atambe nacho ila yule mgombea wa Mataga akianza tuu kuongea English sura yake inabadilika ghafla kuwa ya huzuni na hasira kibao matamshi afadhali hata mwanangu anaeleweka.
 
[SUP]Communication Skills, [/SUP]
[SUP]mataga watabisha [/SUP]
 
E bwana eee
 
MATAGA bwana! China kwa taarifa imewekeza mno kwenye Kiingereza sasa.
China wamewekezaje? wameacha kichina na kufundisha kingereza tuu au wanaendelea na kichina chao na kujifunza kingereza pia(if yes mbona ndo ilo analokataa lisu?)
For me tunahitaji lugha zote mbili kiswahili kama lugha yetu na kingereza kama lugha ya kimataifa, ni kweli hatuko fluent in English lkn wengi waliosoma angalau mpaka form4 wanaweza kuelewa kingereza japokuwa hawawezi kuongea fluently na hiyo kwangu Mimi sio tatizo. After all kuna good number ya watanzania wanaozungumza kingereza vzr, we are not an English speaking country hivo kujua kingereza kwa ufasaha sio hoja, na hatiwezi kusema tuache kiswahili kabisa tuzungumze kingereza utakuwa ni ushamba.
 
KISWAHILI KITUMIKE KUFUNDISHIA KINGEREZA KIBAKI KAMA SOMO KAMA ILIVYO HIVI SASA KWA KISWAHILI. ILI KUPITIA HILO SOMO WATU WATAJIFUNZA LUGHA HIYO KAMA ILIVYO KWA KIFARANSA NK.

NAUNGANA NA LISSU, SERA NI MUHIMU JUU YA LUGHA HASA YAKUFUNDISHIA, KWA MFANO, WANAFUNZI WA VETA HUFUNDISHWA KINGEREZA NA WAKATI WA MTIHANI HUCHAGUA KATI YA KISWAHILI AU KIBGEREZA KATK KUJIBU MITIHANI. NA HAKUNA TATIZO.

LABDA TUJIULIZE, MFUMO WA KUZUNGUSHA DAMU MWILINI UNAHITAJI KUFUNDISHWA JWA LUGHA GANI ILI UELEWE. AU ILI KUJUA ATHARI ZA MMOMONYOKO WA UDONGO HAITAWEZEKANA KWA KISWAHILI.

MAANA YANGU KUNA MASOMO TUNAYASOMA KWA KIINGEREZA BILA KUWA NA SABABU ZA MSINGI MFANO HISTORY, CIVICS, GEOGRAPHY, BIOLOGY, ongezea mengine
 
Lugha yoyote utaijua kwa haraka na kuielewa vizuri kama hakuna lugha nyingine rasmi inayotumika katika mazingira husika.

Kama kingereza kipo shuleni tuu na kwa baadhi ya shule chache, ila nyumbani tunaongea kiswahili full tym,tunaota ndoto kiswahili, tunawaza mawazo kiswahili, ila mitihani tujibu kiingereza na bado tunaimbishana elimu ni ufunbuo wa maisha kufuli la kibongo funguo za mzungu... kweli?
 
Umeelewa hoja ya Lissu lakini?

Sent from my TECNO F3 using JamiiForums mobile app
 

Na kwanini kuwe na topic ndefu hivyo ya mechanics ambayo iko ki nadharia zaidi? Ambayo hata mwanafunzi akimaliza hiyo form six hawezi kuitumia kwa chochote maana hana practicala nayo? Kuna degree za lugha ndugu hao ndio wako competent na lugha, sasa kwa mtu wa kawaida tu unatakiwa ujue business communication. Hiyo inatosha kuweza kuwasiliana na mtu. Sasa kama hata kuwasiliana na mtu na kuelewana mtu anashindwa hilo ni tatizo la mtu binafsi maana haiwezekani ufaulu darasani kwa masomo ya kiingereza ila ushindwe hata basic skills za kuwasiliana na kuelewana na mtu kwa hicho kiingereza. Mfumo mbovu wa kukariri huo.
 

Shule zote zinatumia kingereza kuanzia kidato cha kwanza, na masomo yote yanafundishwa kwa kingereza. Mtu anafaulu vipi hayo masomo na wakati hajui kuwasiliana kwa kingereza? Hapo tatizo ni kusoma kwa kukariri badala ya kuelewa. Hivyo tatizo ni mtaala mbovu na mbinu mbovu za ufundishaji na ujifunzaji. Tukisema lugha ni tatizo bado tutakuwa tumepotea hatujaijua direction. Lazima tuangalie tatizo la msingi katika ubora wa elimu inayotolewa. Sio lugha inayotumika.
 
Ndio hoja ya Lissu,kwamba sio kuwa watanzania ni wajinga bali mfumo ndio unawakwamisha!Ndio maana iko hoja hapa ya kufumua mfumo wa Elimu hasa kwenye lugha ya kufundishia ieleweke tunataka kipi,sio kuwa nusu nusu au katikati!Yaani kiswahili tunakitaka na kiingereza tunakitaka!Mwisho wa siku ni watoto wa masikini tu ndio wanaohangaika,watoto wa wakubwa wako shule ambazo lugha ya kufundishia ni moja na wanafundishwa mpaka kuielewa!
Mimi naona kiswahili kwasababu ni lugha tunayozaliwa na kuijua mtaani,basi kibaki kama somo na kiingereza kiwe lugha ya kufundishia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…