Ndekrepha
JF-Expert Member
- Jun 4, 2020
- 1,506
- 2,660
Umeelewa hoja yangu lakini?Mimi siko hapa kubishana bila mantiki!Jaribu kufikiri kabla hujaandika!
Nimekuuliza swali ambalo mara zote unalikwepa!Huko shule za English medium kwanini wanafanikiwa sana?..
Kumbe huwa wanaongea kingereza wakati mwalimu yupo ila akiondoka ndio wanaongea kiswahili? sasa hiyo ni kwa faida ya nani? Kwani ndio wanajua umuhimu wa kukijua hicho kingereza baada ya kumaliza chuo? mbona hawaweki jitihada ya kukijua kingereza wakati wako shule? kutaka kukijua kingereza wakati wa usahili ni sawa na kusoma zima moto je ndio maisha yetu hayo shuleni?
Mbona shule za kayumba ndio zipo top ten kwa wingi kuliko hizo medium school? au hufatilii na kuona hilo? Halafu pia mbona huongelei wanaofanya vibaya shule za msingi ambako ni kiswahili mwanzo mwisho? hata kuandika sentesi hawawezi, hata miandiko yao tu haieleweki nao pia tatizo ni lugha ya ufundishaji?
Sijawahi kuwa mtu wa siasa mkuu, wala sizielewi siasa za bongo.