Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani muingereza anaongea kiswahili kama mtanzania.?
Sasa kwaninj mnatuchanganya mara sheria ziandikwe kwa kiingereza. Mara shulen sekondari mpaka elimu ya juu ni kiingereza tu. Sasa lissu anakuambia tumekosa sera ya lugha. Tuamue moja kama ni kiswahili au English
 
Nanukuu hapa "sio kwasababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa Sera ya Lugha."

Swali kama lissu ni mjinga naonba unitajie sera ya lugha kwa taifa letu

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Hata wewe uelewa wako ni mdogo sana hujui kuwa kwa sasa sera yetu ni kukuza lugha yetu ya kiswahili ili iwe lugha ya Afrika na imeshaanza kukubalika sasa inatumika SADC!! Kweli wanasaccos hawajitambui
 
Sasa tukiacha kutumia si ndio mwanzo wa kufa mimi nadhani Kama kuna changamoto za matumizi kwenye ngazi za juu bora zifanyiwe kazi ila kufuta hapana, kiswahili kikakua zaidi ya kufa. Yeye Kama anapima uwezo wa mtaaluma kwa kuongea kingereza badala ya maarifa hayo ni matatizo yake binafsi
Huwezo biresha lugha kwenye ngazi ya juu. Lazima tuanzie chini. Lissu yupo sahihi. Mfumo wa elimu yetu ni mbovu sana. Mfano kuna watoto wengi wanafeli masomo ya sekondari kwasababu ya lugha

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Hapa mh Tundu Lissu anataka kumaanisha nini hasa wakuu hebu tusaidiane kidogo.

Amesema kingereza watu hawakijui japo wanasoma kwa muda mrefu tangu O level hadi A level lakini bado ni tatizo kwao.
Lakini pia amesema kuwa kingereza ni muhimu hususani katika suala zima la interaction with foreigners kwamba tunakosa vitu muhimu kwasababu hatujui kingereza.

Sasa hapa ningeomba mnisaidie wakuu.

Kama tatizo ni lunga ya kufindishia ambapo kwa sasa secondary inatumika kingereza na msingi ni kiswahili. Imaana ili sasa wajue kingereza Lugha ya kufundishia mashuleni iwe kingereza kuanzia chekechea hadi chuo kikuu ndipo watu watajua zaidi kingereza?

Kama jibu ni ndio hii italeta matokeo gani kwenye Lugha yetu ya kiswahili baada ya miaka 10-20 ya utekeleza wa hii sera?

Kizazi kijacho kitakuwa wazungumzaji tena wa Kiswahili Kama sasa tulivyo?

Utamaduni wetu Kama watanzania utaishia wapi?

Tukisema pia tuchague Lugha ya kiswahili ndio iwe ya kufundishia mashuleni katika ngazi zote za Elimu je hapo napo kutakuwa na matokeo gani baada ya miaka 20 ya hii sera?

Hapo sasa sio ndio idadi ya wazungumzaji wa kingereza itashuka zaidi na muingiliano wetu na mataifa ya nje utakuwa mgumu zaidi na tutapoteza fursa nyingi zaidi kuliko sasa?

Huyu aliye weka hii sera ya kuchanganya hizi Lugha kwenye Elimu yetu tutaweza kumuweka kwenye fungu hasi ama chanya ikiwa tu tutajibu hasara na faida na mifumo yote miwili Kama itatumika kwenye Elimu yetu.
Kwa kifupi Lissu anashauri kama taifa tuchague lugha moja rasmi ya kufundishia badala ya kuwa na mchanganyiko ambapo primary tunatumia Kiswahili na Secondary tunaanza kutumia kiingereza hivyo inawapa ugumu wanafunzi kuelewa kile wanachofundishwa.

Tunaweza kuchagua Kiswahili kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu kisha kiingereza kikafundishwa kama ilivyo kwa masomo mengine ama tukatumia kiingereza ngazi zote na kiswahili kikafundishwa kama somo jingine tu.
 
Kwa hiyo kuwa msomi ni kujua kingereza?

Hata yule beberu wake akisikia hivi ataona aibu sana
Mataga ni wakusikitikia kweli, rudi kasome tena labda utaelewa anacho maanisha.
 
Kuandika tu hujui Kiswahili utakijua kweli?
Mimi Kiswahili nakijua.

Shida ipo kwa huyo baba yako mzee wa kupuyanga mradi sauti imetoka.

Hivi huwa hawatii aibu? Haujawahi kuhisi kuaibika kwa jinsi anavyoongea?
 
Kati ya siku Lissu ameongea ujinga na utumbo ni leo, yaani lugha iwe kigezo cha kutopata maendeleo, hapana watanzania sio wajinga kiasi hicho, swali lakujiuliza kwa nini kumekuwa na taaluma ya Tafsiri na Ukarimani. Lissu jipange upya nchi kama urusi, uchina nchi za falme za kiarabu wanatumia lugha zao na wako vizuri kiuchumi.
Waarabu wana technology???au mafuta ndio yanawabeba kwa utaalamu wa wazungu
 
Magu2016. Je wajua kuwa sheria zetu bungeni humo zimeandikwa in English ?! . Hukumu zetu mahakamani ni kwa English !!. Documents karibu zote za maana serikalini mpaka leo ni English ?!. Ukivuka mpaka wetu tu, kama hujui English , automatically unakuwa bubu !!
Kwa nini uwe bubu labda kama hujiamini? Wachina wanakuja hapa nchini hawajui kiingereza hata kiswahili lakini baada ya miezi michache tu wanaongea kiswahili. Wanafunzi kule Soweto walipambana kupinga kutumia Lugha ya Makaburu mashuleni ingekuwa ni nyinyi wanasaccos mngelikubali tu kwa sababu ya kutojitambua. Jua kuwa unapozungumza kuhusu utamaduni ni pamoja na lugha yako. Wanasema mdharau utamaduni wake ni mshenzi sasa ukipata mgombea urais anapigania lugha ya wengine huyo hafai kuwa kiongozi katika jamii hiyo!! Hakupashwa kabisa kuongelea hilo wakati huu!!
 
Sawa! China hawajui kiingereza lakini taifa lao ni tajiri wanaandika bidhaa zao kwa kichina na una budi kujifunza kichina. Mtanzania ukiandika bidhaa zako kwa kiswahili nani atasoma? Waliotangulia kimaendeleo inabidi tujifunze lugha zao. Kiingereza ni muhimu, angalia Wakenya, Waganda wanavyopeta kwa kutumia kiingereza. Afrika mashariki "interview "zinafanywa kwa lugha gani?
 
Mimi Kiswahili nakijua.

Shida ipo kwa huyo baba yako mzee wa kupuyanga mradi sauti imetoka.

Hivi huwa hawatii aibu? Haujawahi kuhisi kuaibika kwa jinsi anavyoongea?
Ukiwa na akili ya kitumwa ndiyo utafikiri hivyo!
 
Sawa! China hawajui kiingereza lakini taifa lao ni tajiri wanaandika bidhaa zao kwa kichina na una budi kujifunza kichina. Mtanzania ukiandika bidhaa zako kwa kiswahili nani atasoma? Waliotangulia kimaendeleo inabidi tujifunze lugha zao. Kiingereza ni muhimu, angalia Wakenya, Waganda wanavyopeta kwa kutumia kiingereza. Afrika mashariki "interview "zinafanywa kwa lugha gani?
Bidhaa yako kama inahitajika lazima atanunuliwa! Madini ya Tanzanite mbona yananunuliwa wakati yanajina la Kitanzania?
 
Hapa umetumia lugha ngapi,ipi unaona ipo sahihi. Unataka Tanzania iwe great kutumia kiswahili at the same time unamfundisha huyo mtanzania kwa lugha ya kingereza. Maajabu haya yapo Tanzania tu

Umeweka mfano China, unafananishaje china na Tanzania. China wana lugha moja tu sio km sisi wa kiswanglish.
 
Kiingereza ni kama kijaluo tuu, mbona wachina wengi hawajui kiingereza na wako vizuri kichwani,lissu ni miongoni mwa wale wakiona mtoto mdogo wa kizungu anaongea kiingereza wanamshangaa. Nakusema "mtoto huyu ana akili sana".
Mbona hamuelewi nyie MaCCM..wachina lugha yao ya kufundishia ni kichina...na sisi tuamue iwe kiswahili au English..mfano ukiwa Ulaya ni United Kingdom tu ndio wanaotumia kiingereza...nchi nyingine zote wanatumia lugha zao...
 
Kiswahili kikue SADC itumie hii lugha, rubbish? Lugha ya kingereza ni lugha ya kidunia, inatamkwa na nchi karibia zote duniani, kwa nini mjilimit na opportunities za SADC.. wakati mngeweza ku enjoy... dunia
 
Sawa... mtataka mbadili lugha ya kufundishia, iko wazi asilimia kubwa ya watu watachagua kiswahili.
Je unaweza fundisha physics kwa kiswahili?

Ni bora ibaki kama ilivyo mradi haina madhara kwenye maendeleo.

Kwanini uone aibu mtanzania akikosea kuongea kiingereza?
Kwani ni lugha yake hiyo?
 
Lissu ameeleza ugoro sana! Ni aibu mgombea urais badala ya kuipigia chapuo lugha yake anawadiss wasiyojua lugha ya kiingereza!! Slavery Mentality!!
Najua kuelewa kwa baadhi ya watu ni mchakato mrefu, wengine hadi wakeshe na wengine hadi waloweke miguu, rudia tena labda utaelewa.
 
Back
Top Bottom