Uchaguzi 2020 Lissu: Watanzania sio kwamba hawana akili bali Lugha ya kufundishia ndio shida, Elimu yetu inabidi ifumuliwe na lugha ya kufundishiwa iwe moja

Lugha yetu ya taifa ni kiswahili sasa anataka Kiingereza kiwe kama lugha yetu? Kwani muingereza anaongea kiswahili kama mtanzania.?
Sasa kwaninj mnatuchanganya mara sheria ziandikwe kwa kiingereza. Mara shulen sekondari mpaka elimu ya juu ni kiingereza tu. Sasa lissu anakuambia tumekosa sera ya lugha. Tuamue moja kama ni kiswahili au English
 
Nanukuu hapa "sio kwasababu hatuna akili ila ni kwasababu tumekosa Sera ya Lugha."

Swali kama lissu ni mjinga naonba unitajie sera ya lugha kwa taifa letu

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Hata wewe uelewa wako ni mdogo sana hujui kuwa kwa sasa sera yetu ni kukuza lugha yetu ya kiswahili ili iwe lugha ya Afrika na imeshaanza kukubalika sasa inatumika SADC!! Kweli wanasaccos hawajitambui
 
Huwezo biresha lugha kwenye ngazi ya juu. Lazima tuanzie chini. Lissu yupo sahihi. Mfumo wa elimu yetu ni mbovu sana. Mfano kuna watoto wengi wanafeli masomo ya sekondari kwasababu ya lugha

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Kwa kifupi Lissu anashauri kama taifa tuchague lugha moja rasmi ya kufundishia badala ya kuwa na mchanganyiko ambapo primary tunatumia Kiswahili na Secondary tunaanza kutumia kiingereza hivyo inawapa ugumu wanafunzi kuelewa kile wanachofundishwa.

Tunaweza kuchagua Kiswahili kama lugha ya kufundishia ngazi zote za elimu kisha kiingereza kikafundishwa kama ilivyo kwa masomo mengine ama tukatumia kiingereza ngazi zote na kiswahili kikafundishwa kama somo jingine tu.
 
Kwa hiyo kuwa msomi ni kujua kingereza?

Hata yule beberu wake akisikia hivi ataona aibu sana
Mataga ni wakusikitikia kweli, rudi kasome tena labda utaelewa anacho maanisha.
 
Kuandika tu hujui Kiswahili utakijua kweli?
Mimi Kiswahili nakijua.

Shida ipo kwa huyo baba yako mzee wa kupuyanga mradi sauti imetoka.

Hivi huwa hawatii aibu? Haujawahi kuhisi kuaibika kwa jinsi anavyoongea?
 
Waarabu wana technology???au mafuta ndio yanawabeba kwa utaalamu wa wazungu
 
Kwa nini uwe bubu labda kama hujiamini? Wachina wanakuja hapa nchini hawajui kiingereza hata kiswahili lakini baada ya miezi michache tu wanaongea kiswahili. Wanafunzi kule Soweto walipambana kupinga kutumia Lugha ya Makaburu mashuleni ingekuwa ni nyinyi wanasaccos mngelikubali tu kwa sababu ya kutojitambua. Jua kuwa unapozungumza kuhusu utamaduni ni pamoja na lugha yako. Wanasema mdharau utamaduni wake ni mshenzi sasa ukipata mgombea urais anapigania lugha ya wengine huyo hafai kuwa kiongozi katika jamii hiyo!! Hakupashwa kabisa kuongelea hilo wakati huu!!
 
Sawa! China hawajui kiingereza lakini taifa lao ni tajiri wanaandika bidhaa zao kwa kichina na una budi kujifunza kichina. Mtanzania ukiandika bidhaa zako kwa kiswahili nani atasoma? Waliotangulia kimaendeleo inabidi tujifunze lugha zao. Kiingereza ni muhimu, angalia Wakenya, Waganda wanavyopeta kwa kutumia kiingereza. Afrika mashariki "interview "zinafanywa kwa lugha gani?
 
Mimi Kiswahili nakijua.

Shida ipo kwa huyo baba yako mzee wa kupuyanga mradi sauti imetoka.

Hivi huwa hawatii aibu? Haujawahi kuhisi kuaibika kwa jinsi anavyoongea?
Ukiwa na akili ya kitumwa ndiyo utafikiri hivyo!
 
Bidhaa yako kama inahitajika lazima atanunuliwa! Madini ya Tanzanite mbona yananunuliwa wakati yanajina la Kitanzania?
 
Hapa umetumia lugha ngapi,ipi unaona ipo sahihi. Unataka Tanzania iwe great kutumia kiswahili at the same time unamfundisha huyo mtanzania kwa lugha ya kingereza. Maajabu haya yapo Tanzania tu

Umeweka mfano China, unafananishaje china na Tanzania. China wana lugha moja tu sio km sisi wa kiswanglish.
 
Kiingereza ni kama kijaluo tuu, mbona wachina wengi hawajui kiingereza na wako vizuri kichwani,lissu ni miongoni mwa wale wakiona mtoto mdogo wa kizungu anaongea kiingereza wanamshangaa. Nakusema "mtoto huyu ana akili sana".
Mbona hamuelewi nyie MaCCM..wachina lugha yao ya kufundishia ni kichina...na sisi tuamue iwe kiswahili au English..mfano ukiwa Ulaya ni United Kingdom tu ndio wanaotumia kiingereza...nchi nyingine zote wanatumia lugha zao...
 
Kiswahili kikue SADC itumie hii lugha, rubbish? Lugha ya kingereza ni lugha ya kidunia, inatamkwa na nchi karibia zote duniani, kwa nini mjilimit na opportunities za SADC.. wakati mngeweza ku enjoy... dunia
 
Sawa... mtataka mbadili lugha ya kufundishia, iko wazi asilimia kubwa ya watu watachagua kiswahili.
Je unaweza fundisha physics kwa kiswahili?

Ni bora ibaki kama ilivyo mradi haina madhara kwenye maendeleo.

Kwanini uone aibu mtanzania akikosea kuongea kiingereza?
Kwani ni lugha yake hiyo?
 
Lissu ameeleza ugoro sana! Ni aibu mgombea urais badala ya kuipigia chapuo lugha yake anawadiss wasiyojua lugha ya kiingereza!! Slavery Mentality!!
Najua kuelewa kwa baadhi ya watu ni mchakato mrefu, wengine hadi wakeshe na wengine hadi waloweke miguu, rudia tena labda utaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…