Matatizo makubwa ya CCM, bado ninaamini kuwa yapo kwenye ushauri, na hasa Muungwana kama rais, kwa kweli nina tatizo sana na washauri wake wa siasa, kwa sababu anapaswa kuwa bigger than yaliyoandikwa kwenye hii article,
Wa-Tanzania wengi, hasa vijana wanamkubali Muungwana kama agent of change, na hasa jinsi alivyoweza kuikaba establishment, mpaka akawa rais, in the process hata na yeye aliwahi kuwashutumu kina Gama na Msuya, kuwa walikula njama za kumuangusha kwa makususdi asipate urais, mwaka 1995, je kuna aliyemlaumu kuwa anahatarisha amani kwa hayo maneno yake?
Hapana, WHY? Ni kwa sababu hata viongozi wa CCm walisha-sense kuwa time zimebadilika, wakanyamaza kimyaaa, halafu pia kwenye uchaguzi wa NEC, mwaka 2000, Muungwana, alipopigwa chini tena, mbona aliwatukana wajumbe wote wa CC, kule Zanzibar kama watoto, na hasa Mkapa, kwa kumfanyia ujanja kwenye kura zake, je kuna aliyemlaumu kuwa anahatarisha amani na hizo tuhuma zake? Na kwamba sasa yeye amekuwa hakimu, na prosecutor pamoja?
Kwakweli, ningemuomba Muungwana, awaangalie tena washauri wake wa siasa, ambao wanaonekana kutoelewa kabisa siasa za kisasa na kukumbatia siasa zilizopitwa na wakati, kwa sababu:-
1. kufukuzwa kwa Zitto, bungeni,
2. Orodha ya mafisadi,
3. Kuzomewa kwa viongozi wa CCM,
4. Kuvuja kwa mkataba wa Buzwagi,
I mean hizi ni political points, zinazohitaji a serious political response through a change of the way of doing political things katika jamiii yetu, Muungwana alipaswa not only kuzikumbatia hizi points kwa faida yake na CCM kwa ujumla, bali alitakiwa azi-hijack na kuzifanyia kazi kwa manufaaa ya CCM, na wananchi wa taifa letu kwa ujumla, badala ya yeye kushuka chini kwenye level za akina Warioba na Bomani, na kuwafanya waonekane kuwa message zao zina something to do na yeye Muungwana, maana zinafanana sana haswa kwenye point ya amani ya taifa kuchafuliwa, hoja ambayo ni hafifu sana ukifuatilia njia aliyoitumia kufikia urais wake,
Muungwana alipaswa, kukubali mbele ya taifa kuwa wananchi nimewasikia, pamoja na kwamba zilizotolewa ni tuhuma tu, lakini ninawashukuru kwamba mmezipokea bila ya kuvunja sheria zetu za nchi, nimeviagiza vyombo vyetu vya sheria kuzichunguza kwa makini tuhuma hizo nzito dhidi ya baadhi ya viongozi wakuu wa taifa, kwa sababu tunahitaji kuwa na taifa linaloheshimu the rule of law na demokrasia, sita-comment kitu chochote kuhusiana na tuhuma hizo kuepukana na ku-ifluence the outcome,
Lakini at the same token, wananchi nimewasikia tena loud and clear, kuwa kunahitajika mabadiliko ya kisiasa kwa kuanza na viongozi, na the buck stops here kwangu rais wenu. Sasa huu ni wakati mzuri kwa Muungwana to come through na ile ahadi yake kuwa hana ubia na Mtandao au mtu yoyote kwenye urais wake, kwa kuwatosa viongozi wote walioonyesha kuwa na uwezo mdogo katika kipindi chake cha utawala so far, halafu pia wale wote walioshindwa kwenye uchaguzi wa NEC, hii ndiyo ilikuwa nafasi nzuri ya yeye kukubali kura za wanachama wa chama chake CCM, kuwa mawaziri wote walioshindwa akina Ngasongwa, Mungai, na wengine wote wa ngazi za juu kuwa hawafai na busara za political correctness, zina-demand kuwatosa sasa nje ya cabinet, kwa sababu Muungwana apende asipende, kisiasa ukweli ni wananchi wanaanza kumuonyesha kuwa wana wasi wasi kama kumchagua hawakufanya makosa, meaning kwamba confidence ya wananchi kwake kiuongozi, hapa imepigwa kidogo inahitaji kujengwa tena, na pole pole na kwa uangalifu sana, lakini sio kwenda kuzungumza kwa padri kama alivyofanya, maana sasa hivi wananchi sio wajinga tena kujua kuwa kujichomoza kwa makanisa kila kona ya nchi sasa hivi kunaashioria tu kuwa nayo hiyo dini sasa ni biashara safi na yenye manufaaa,
Kuvuja kwa mkataba wa Buzwagi, ni fundisho la kuwepo baadhi ya viongozi wenzake wa juu wasioridhika na utawala wake, sasa tatizo sio ni nani hao, bali tatizo ni wanataka nini? Huenda wanayoyataka ni kwa faida ya taifa zima, sasa dawa ni kuwasikiliza na sio kuwatishia na usalama wa taifa au Takuru, au kuwabagua, Mkapa, pia yalimkuta haya, viongozi wenziwe wakamfanyia uhuni CCM ikashindwa ubunge wa Temeke na Bariadi, alipoingia tu na makiki yake, ingawa alikuwa mjanja na kukaa chini kuwasikiliza, ni bahati mbaya kuwa viongozi hao hawakuwa na nia njema kwa wananchi at large, bali matumbo yao tu, lakini Muungwana asi-assume kuwa in this case pia nia yao ni mabya bila ya kuwaiskiliza,
We can go on and on, lakini kwa maoni yangu Muungwana, anahitaji washauri wapya wenye kuelewa wakati tulionao, na ambao wanahitaji kutambua kuwa uchaguzi wa rais uliisha siku nyingi, sasa ni kazi, kupokewa kwake na wananchi wengi pale Aiport juzi ni dalili tosha kuwa bado wananchi wengi wana imani naye, lakini wana tatizo na wasaidizi wake, halafu Mtandao kwa ujumla wajifunze kusamehe wapinzani wao kiitikadi kwa faida ya taifa at large, kwa sababu msuguano wao so far hautuletei mema kwenye taifa, na pia viongozi wa CCM na serikali ndani ya bunge, wajifunze kusikiliza wabunge wao, badala ya kufikiri kuwa wao tu ndio wanaojua what is best kwa taifa na CCM, kwa sababu wabunge wengi wa CCM tulio ongea nao wanasema kuwa waliwaonya sana kuepuka na kumfukuza Zitto, bungeni lakini wakaziba masikio, matokeo yake sasa hivi wabunge hao wanacheka sana yanayojiri,
Ni wakati wa Muungwana sasa kuzinduka na kutathmini utawala wake, na the legacy anayoitaka kuwaachia wananchi na taifa kwa ujumla,
Mungu Aibariki Tanzania Yetu!