List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Mgonjwa wa ukimwi.. kuna makosa ya commission... na makosa ya omission. Mtu anaweza kuchukua rushwa yeye mwenyewe (commission) au kwa nafasi yake angepaswa kuhakikisha rushwa haitokei lakini hafanyi hivyo na rushwa ikatokea chini yake (omission). Kati yote ni makosa.

Kiupande wa uhalifu ni hivi, daktari anayempa mgonjwa dawa ambayo anajua haistahili na lengo lake ni kumuua anafanya kosa la commission. Na daktari ambaye anajua kabisa akimpa mgonjwa fulani dawa fulani dawa hiyo itampa nafuu lakini kwa makusudi hampi dawi hiyo na mgonjwa yule anakufa, daktari atakuwa amefanya kosa la omission.

Now, katika hoja za kina Slaa wanachosema ni kuwa kuna viongozi ambao wamefanya makosa ya commission na wapo wale ambao wamefanya makosa ya omission. Tatizo ni kuwa matokeo ya makosa hayo yote ni yale yale, hasara kwa Taifa.
 
Dr Slaa acha kutufanya wajinga baba, wewe tueleze nini Balali alifanya haswa. Aliruhusu? Aliidhinisha? alinyamazia? Kama wewe mwenyewe huna uhakika na alichofanya Balali sisi wasomaji ndo inakuaje?

Bado tupo pale pale, Dr Slaa inaonyesha anabuni kwa wasiwasi mkubwa juu ya kilichoandikwa kwenye barua ambayo anasita kuinukuu. Kaazi kweli kweli.

Dah! hii kali. Sasa endapo Balali ALINYAMAZIA bila kunufaika tunamshitaki kwa kosa gani? la rushwa au ufisadi? Naona Dr Slaa upinzani unamshinda, bora pale alipoamua kutopeleka vigezo hivi bungeni....alijuwa havina nguvu.

Bado tatizo lipo pale pale. Aliruhusu? Aliidhinisha? Alinyamazia? Au vyote? By the way hao watu wasiojulikana ndo akina nani?

2. ANDREW J. CHENGE

Duh! "alishiriki na/au kufaidika." Maneno haya yangeleta maana tu endapo ufafanuzi ungetolewa, ili wasomaji tujuwe ushiriki unaomshitaki ni upi, na ufaidikaji unaomshitaki ni upi. Vinginevyo hapa Dr Slaa anatufumba na kujifumba.

Fumbo linaendelea..."Mheshimiwa Chenge ameshiriki kuishauri vibaya na/au kutokuishauri vizuri." Sasa kosa hapa ni lipi analostahili Chenge kuhukumiwa? La ushauri mbaya? Je kosa la Prof Lipumba la kumshauri Ali Hassan Mwinyi kuiporomosha shilingi ya Tz hadi sasa inashindwa kupaa, atahukumiwa lini?

Sasa mheshimiwa Slaa, ebu tuambie kosa hapa ni lipi, incompetence ya Chenge katika ushauri ama ushauri mbaya wa makusudi. Kama ni ushauri mbaya wa makusudi mbona katika maelezo yako husemi kwamba alishauri vibaya huku akijuwa na ukatupa ushahidi juu ya hilo?

3. BASIL P. MRAMBA

Mheshimiwa Mramba amehujumu taifa la Tanzania kama ifuatavyo:

Huu ni ushahidi mbofumbofu...very weak in deed. Dr Slaa tueleze process alizopitia Mramba katika kuhalalisha Alex Stewart ipewe kazi. Husiturushe rushe, na kama huna uhakika tumia neno 'suspect.' Ushaidi wako utakamilika tu kwa kutuambia alishiriki vipi na utoaji haramu wa kazi kwa Stewart, sio kutokana na maneno ya mdhibiti na mkaguzi mkuu kwamba hakukuwa na ushaidi wa upatikanaji halali wa zabuni ya ushindani. Je kama "hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kwamba wakaguzi hawa wa dhahabu walipatikana kwa kufuata utaratibu wa zabuni ya ushindani," je kulikuwa na ushahidi kwamba Mramba aliwapa kazi kwa njia alizozijuwa yeye?...au Dr Slaa unataka ushahidi wako usomeke between the lines!!! Mnyika uko wapi ebu sahidia hii dokta yako hapa.

Ebu nipige darasa hapa kabla hujanichanganya. Rushwa au Ufisadi? Je kukiwa na Ufisadi bila rushwa bado ni kosa? la uzito gani kulinganisha na ule wa rushwa?

Kaaazi kweli kweli. Ushahidi huu ni rahisi kupingika mana hauna msingi. Barua ya Erwin Flores ilikuwa imfikie nani? Ni barua ya aina gani inashindwa kutaja last name ya subject lakini iko wazi kujata title ya subject huyo....it is like, 'I will tell you what he does but won't tell you his last name.' Alafu barua pepe inaweza kuandikwa na yeyote, kutoka popote, ikamfikia yeyote, mana haina sahihi, bali anuani na logo (perhaps) ambazo zinagushika kiurahisi.

In General ushhidi ulioletwa na Dr Slaa kwakweli unakosa nguzo, nampongeza kwa uamuzi wake wakutofikisha mahakamani, mana angemomonyoa credibility yake.

Kumbe wewe umeishia hapa? Unadhani Dk. Slaa ni mjinga kuchukua ushahidi wa mahakamani kuweka hapa? Haya ni maelezo yanatokana na vielelezo kadhaa alivyowasilisha kwa wananchi.

Ushahidi bado anao na ndio huo ambao Kingunge anauomba. Kwa taarifa yako, serikali ikiwagusa yatakayotokea ni makubwa sio yale ya mkutano wa hadhara.

Usione wanasema "sisi hatuwashitaki wapinzani" ukadhani ni bure. Kama wewe unadhani huu ndio ushahidi umeliwa wewe! Kalagabao!
 
Dr Slaa acha kutufanya wajinga baba, wewe tueleze nini Balali alifanya haswa. ..tupo pale pale, ....unaomshitaki ni upi. Vinginevyo hapa Dr Slaa anatufumba na .. ebu tuambie kosa hapa huku akijuwa na ukatupa ushahidi juu ya hilo?
utakamilika tu kwa kutuambia alishiriki vipi na utoaji haramu wa kazi kwa Stewart, sio

.... yake.

Unatumia sana uwingi kwenye sentensi zako, uko nani vile? au unawakilisha kundi gani ambalo unalisemea?
 
Kumbe wewe umeishia hapa? Unadhani Dk. Slaa ni mjinga kuchukua ushahidi wa mahakamani kuweka hapa? Haya ni maelezo yanatokana na vielelezo kadhaa alivyowasilisha kwa wananchi. Ushahidi bado anao na ndio huo ambao Kingunge anauomba. Kwa taarifa yako, serikali ikiwagusa yatakayotokea ni makubwa sio yale ya mkutano wa hadhara. Usione wanasema "sisi hatuwashitaki wapinzani" ukadhani ni bure. Kama wewe unadhani huu ndio ushahidi umeliwa wewe! Kalagabao!

Kichwamaji;
Kama ulivyosema ni kweli basi huo ndio ufinyu wa mawazo, Dr Slaa anatakiwa kuiharifu jamii ijuwe maovu ya viongozi. Wala hatakiwi kui-adaa jamii anayoitumikia kwa kuficha ushahidi na kuiambia jamii maneno ambayo yako mbali na ushahidi. Nikuulize swali Kichwamaji,,,,kama huu sio ushahidi wa mahakamani ni ushahidi wa wapi? JF? Sasa jamii inajuaje kwamba Dr Slaa bado anaushahidi zaidi ya huu?

MzeeMwakijiji;
Nimekupata vyema, ila tatizo langu ni kwamba Dr Slaa hakuna anapogusia kwamba viongozi, kwa mfano, waliotoa ushauri mbaya walifanya hivyo huku wakijuwa (na kutupa ushahidi kwamba that was the case)...ndo mana nikasema incompetence is not a crime by itself though it may result into one. Nikatoa mfano wa prof Lipumba aliyeididimiza shilingi yetu kwa kumshauri Mwinyi, hadi leo shilingi inatapatapa na bado hajaukumiwa. Naam ushauri mbaya ni kosa, pale tu inapothibitika kwamba mshauri alifanya hivyo hali akijuwa, ila ikithibitika alifanya kutokana na incompetence yake, hana kosa,,,ingawa maamuzi ya ushauri wake niyakimakosa.
 
Unatumia sana uwingi kwenye sentensi zako, uko nani vile? au unawakilisha kundi gani ambalo unalisemea?

Kabisa,natumia uwingi na nitaendelea kutumia uwingi. Juu ya watu ninaowasemea, natunza haki na uhuru wangu wa kutowataja.
 
Kichwamaji;
Kama ulivyosema ni kweli basi huo ndio ufinyu wa mawazo, Dr Slaa anatakiwa kuiharifu jamii ijuwe maovu ya viongozi. Wala hatakiwi kui-adaa jamii anayoitumikia kwa kuficha ushahidi na kuiambia jamii maneno ambayo yako mbali na ushahidi. Nikuulize swali Kichwamaji,,,,kama huu sio ushahidi wa mahakamani ni ushahidi wa wapi? JF? Sasa jamii inajuaje kwamba Dr Slaa bado anaushahidi zaidi ya huu?

MzeeMwakijiji;
Nimekupata vyema, ila tatizo langu ni kwamba Dr Slaa hakuna anapogusia kwamba viongozi, kwa mfano, waliotoa ushauri mbaya walifanya hivyo huku wakijuwa (na kutupa ushahidi kwamba that was the case)...ndo mana nikasema incompetence is not a crime by itself though it may result into one. Nikatoa mfano wa prof Lipumba aliyeididimiza shilingi yetu kwa kumshauri Mwinyi, hadi leo shilingi inatapatapa na bado hajaukumiwa. Naam ushauri mbaya ni kosa, pale tu inapothibitika kwamba mshauri alifanya hivyo hali akijuwa, ila ikithibitika alifanya kutokana na incompetence yake, hana kosa,,,ingawa maamuzi ya ushauri wake niyakimakosa.

Mgonjwa Ukimwi,
Nadhani wewe unaishi mbali na nchi inayoitwa Tanzania, na unadhani Dk. Slaa hajui implications za matamshi yake. Yule siyo mbabaishaji, na kwa taarifa yako hayuko peke yake. Ukitaka kujua nguvu yake serikali ichukue hatua. Unazungumzia JF? JF ina inluence gani katika hili mbali na kujadili likapita? Unasikia TAKUKURU wanatafuta documents hizo ili waharibu ushahidi lakini mambo yameshafika mbali mno.

Usiwe na presha wala haraka ya kutaka kujua kila kitu leo. Utajua hatua kwa hatua, maana system tunaijua. Watz wamezunduka sasa hawachukui mtama wakamwaga mbele ya kuku wengi eti kuwaridhisha watazamaji na wasikilizaji. Vile vile, watu mature hawazungumzi yote kumaliza. Endelea kui-monitor hiyo Mgonjwa...
 
Mgonjwa Ukimwi,
Nadhani wewe unaishi mbali na nchi inayoitwa Tanzania, na unadhani Dk. Slaa hajui implications za matamshi yake. Yule siyo mbabaishaji, na kwa taarifa yako hayuko peke yake. Ukitaka kujua nguvu yake serikali ichukue hatua. Unazungumzia JF? JF ina inluence gani katika hili mbali na kujadili likapita? Unasikia TAKUKURU wanatafuta documents hizo ili waharibu ushahidi lakini mambo yameshafika mbali mno.

Usiwe na presha wala haraka ya kutaka kujua kila kitu leo. Utajua hatua kwa hatua, maana system tunaijua. Watz wamezunduka sasa hawachukui mtama wakamwaga mbele ya kuku wengi eti kuwaridhisha watazamaji na wasikilizaji. Vile vile, watu mature hawazungumzi yote kumaliza. Endelea kui-monitor hiyo Mgonjwa...

Kichwamaji,
Taifa letu limeshuhudia viongozi wabovu na wajinga tangu kupata uhuru, Dr Slaa anaweza kuwa miongoni. Na kwa mtazamo wangu juu ya ushahidi alioutoa kwakweli ni finyu mno. Kusema kwamba anaushahidi mwingine hizo ni speculations, kadhalika kusema kwamba TAKUKURU inatafuta ushahidi ili iuharibu ni speculations unazozitoa, ambazo kwa mtazamo wangu wa kizalendo, zinalenga katika kuharibu credibility ya TAKUKURU. Lakini kama ulivyosema nitaendelea ku-monitor hii issue...ati wanasema kila panapofuka moshi pana moto,,,not knowing ukungu wakati mwingine uonekana kama moshi...!!
 
Mtu anapotetea uhalifu huku akijua kuwa ni uhalifu, huyo pia anaweza kuwa ktk kundi la wahalifu pia. Haiitaji akili ya Chuo kikuu kukuonyesha kwamba kuna mazingira ya Rushwa BOT. Waraka umefafanua vizuri na kueleweka vizuri. Kama Balali hakuhusika, basi anabanwa na kifungu cha utawala bora, kwa sababu Kampuni zilizokuwa zinalipwa pesa naye pia ni Mkurugenzi huko.

Kiwango kilicholipwa ni kikubwa mno hivyo hakiwezi kuidhinishwa na mtu chini yake kutokana na taratibu za kifedha. kwa maana nyingine alikuwa anajua anachokifanya. Kusema kwamba Taifa limeshuhudia viongozi wabovu Tangu uhuru ni kutojiamini wewe mwenyewe una nafasi gani ya kukwamua huo ujinga, kwa hiyo fikra zako unazilazimisha kuwa jinga pia.

Hatuwezi kila wakati kuhalalisha ujinga wa mtu mwingine ili kuendeleza ujinga kwa jamii yetu. Ni lazima tuende mbele si kurudi tena kwenye Ujinga.

Kama Dr, Slaa unaona amekosea, ni jukumu lako pia kumsaidia arekebishe wapi ili statement yake iwe na uzito unaostahili. kumlaumu mtu ambaye anajitahidi kufungua macho yetu juu ya nini kinaendelea Serikalini ni kuonea bure na kumkatisha tamaa.

Lipende Taifa lako na watu wake. sote tunahitaji maisha bora ingawa kama wenzetu tayari mna maisha bora basi hamtujui wenye njaa na ndiyo maana mnabeza juhudi za akina Slaa na wengineo wenye Mapenzi mema.
 
Mgonjwa wa ukimwi, i am afraid, the virus is up on your brains! you can't read in between the lines? What did you score in literature! Mr. Slaa wants to know how the money was allowed out of the bank; iwe ni "Aliruhusu, Aliidhinisha, alinyamazia". Akili kweli ni ..... kila mtu ana zake!
 
Argument # 1,

Dr Slaa acha kutufanya wajinga baba, wewe tueleze nini Balali alifanya haswa. Aliruhusu? Aliidhinisha? alinyamazia? Kama wewe mwenyewe huna uhakika na alichofanya Balali sisi wasomaji ndo inakuaje?

In my view, Dr. Slaa, ni mwananchi na kiongozi mwenye uchungu na nchi yake, yeye professionally, sio mwanasheria, au Prosecutor ama mtaalamu wa sheria, lakini ameweza kutumia elimu yake kwa manufaa ya umma at large, ambao ni sisi mimi nilifikiri ni wajibu wetu kuyatafakari kwa makini aliyoyasema, na ikibidi kuyafanyia uchunguzi hata wa kisayansi, ili kuhakikisha ukweli ulipo na uongo ulipo,

badala ya kuja na general statement kuwa aache kutufanya wajinga!, badala yake tungesema ahsante kwa kutupatia changamoto na sasa kazi kwetu kuutafuta ukweli wa uliyosema, FULL STOP!

Dr. Slaa, hatufanyi wajinga kwa sababu anaanza na kusema wazi kuwa viongozi anaowatuhumu wamehusika kwa "namna mbali mbali" za ujanja ambazo matokeo yake yamekuwa kuliletea hasara taifa letu, na namna mbali mbali anazozisema zinajumuisha kuruhusu, kuidhinisha, au kunyamaza, kwa makusudi huku wakijua wazi kuwa matokeo ya vitendo hivyo vitatu alivyovitaja, vitawaletea faida wao binafsi kwa migongo ya sisi wananchi, kwa njia ambazo ni kinyume na sheria zetu,

Kisheria ilitakiwa by now serikali yetu iwe tayari imetangaza kuunda kamati maalum ambayo ni independent kuchunguza madai haya ya Dr. Slaa, kwa nini mpka leo serikali haijafanya hivyo? Mbona kwenye tuhuma za minofu ya samaki serikali iliunda kamati mara moja, this time mbona wamekuwa na kigugumizi?

Kisiasa viongozi waliotuhumiwa walitakiwa wawe tayari wamejibu kwenye public kwamba hawahusiki na hizi tuhuma na kwamba watapigana kufa na kupona kusafisha majina yao, sasa ni kwa ni ni hawafanyi hivyo kama aliyoyasema Dr. Slaa ni ujinga?

Mwalimu Nyerere na Kawawa, walipotuhumiwa kuwa ni wezi na Kambona pale Jangwani, the next day tuliwasikia wakijibu kuwa tuhuma hizo ni za uongo na kwamba iwapo Kambona anao ushahidi autoe hadharani, au aombe radhi, ama sivyo watamshitaki kwenye sheria kusafisha majina yao, lakini Kambona akashindwa kutoa ushahidi na kuomba radhi haraka,

in this case Dr. Slaa ametoa ushaidi sasa ni wakati wa viongozi waliotuhumiwa kujibu mapigo na kupigana na ushahidi, na sio sisi wananchi tusiojua chochote kuhusiana na tuhuma hizo kuja na hizi general statement za kumuita Dr. Slaa ni mjinga, maana wananchi wenye akili watashindwa kuelewa nani hasa ni mjinga hapa, maana kisheria hapa viongozi wetu waliotuhumiwa wanahitaji kujisafisha tena kwa kisheria na kisiasa, kwa kupigana na huu ushahidi mzito uliotolewa na wananchi/kiongozi, tena wa upinzani mwenye very limited resources au tools za kufanyia uchunguzi mzito kama huu wa uhalifu wa viongozi wa juu kwa sisi wananchi walalahoi,

Mkuu MgonjwaWaukimwi, ninaheshimu sana uwezo wako accademically wa kuchamnbua ishus, lakini ninaomba nikuambie one thing, ni kweli kama ulivyosema kuwa kuna mjinga hapa lakini I bet you with my life sio Dr. Slaa!
 
Field Marshal Es,

Unajua uncle kuna ugonjwa mkubwa umeingia JF sasa hivi kiasi kwamba imekuwa Unazi badala ya kuyaweka maslahi ya taifa letu mbele. napenda sana dira ulochukua sasa hivi maanake haina kabisa unazi isipokuwa ukweli wako ndi unakupa mapenzi zaidi toka kwetu na Mungu mwenyewe!

Kuna watu humu wameisha fikia kudai kuwa hii ni strategy ya Upinzani?.. again what strategy?.. hivi kweli unapogundua na kutangaza maradhi ya mtu hiyo ni strategy.. ama strategy yoyote huanza kutungwa pale gonjwa limeisha bainika.

Yaani kusema kweli kuna mada kibao nashindwa hata kuzishangia kwa sababu hazi na kichwa wala miguu... tunaonekana kama vile wachovu wa kufikiri kabisa kwa sababu khakuna tena ule mtindo wa watu kutoa hoja zao zenye sura tofauti na kile tunachokiona bali hoja humtazama nani kasema! ana elimu gani? ametoka wapi na kadhalika badala ya sisi hoja kwa maslahi ya Taifa zima.

I mean hivi kweli mlalahoi mkulima wa karafuu huko Kilwa hawezi kuwa na mawazo mazuri ama kuzungumzia RUSHWA kwa sababu hana elimu?

Hivi kweli Mbowe hana haki ya kuzungumzia RUSHWA kwa sababu yuko chama cha Upinzani?.. na hivi kweli inawezekana mtu kutoka CCM mwenye elimu akasimama na kupinga rushwa wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa walaji?. Na kama haiwezekani, je ni nani anayetakiwa kusimama na kulilia haki hii?

Kwa wale wote mnaopinga nitafurahi sana kama mtaweza kujibu swala hili maanake najaribu kufikiria mnachofikiri nashindwa kabisa kuelewa!. hoja nyingi humu ni sawa na jahazi linalokwenda kwa Upepo na kutegemea nyota..yaani hakuna tena matumizi ya elimu mliyoipata kuelezea umuhimu wa maswala yaliyoko ubaoni.

Dr. Slaa katupa somo, tukae, tulijadilki na pengine wafumbuzi wa swala hili ni sisi wenyewe sio Slaa tena. Slaa katupa diagnosis ya gonjwa letu na nani mwambukizaji, swala la kuweka karantini ama ufumbuzi ni jukumu letu.

I care less kama huyu Slaa ni Chadema ama CUF bali hoja yake ni ya msingi na ushahidi unaopinga hoja yake ndio nataka kuuona hapa.
 
Tatizo wenzenu wameshaamua kuwa watajenga hoja ya kuwapuuzia.. hawatajibu, hawataenda mahakamani, na wala hawatataka kina Slaa kuomba radhi, watawataka wananchi wapuuzie hoja za upinzani. Huo ndio mkakati wa kina Kingunge.
 
... kadhalika kusema kwamba TAKUKURU inatafuta ushahidi ili iuharibu ni speculations unazozitoa, ambazo kwa mtazamo wangu wa kizalendo, zinalenga katika kuharibu credibility ya TAKUKURU. Lakini kama ulivyosema nitaendelea ku-monitor hii issue...ati wanasema kila panapofuka moshi pana moto,,,not knowing ukungu wakati mwingine uonekana kama moshi...!!

Mkuu nadhani uzalendo wako uko kwenye kutetea TAKUKURU kwamba imekuwa ikifanya kazi nzuri sana. Naomba unipe credibility ya PCCB ambayo wewe kwa vigezo vyako unadhani kwamba inaharibiwa. Hivi siyo Hosea aliyesema kwamba hawezi kuchunguza tuhuma za Mkapa simply because JK amesema asichunguzwe? Niambie credibility ya PCCB hapo iko wapi?

Kauli ya Hosea ilikuwa ni ya kujimaliza mwenyewe na PCCB yake kwa kuwa alituonyesha wazi kwamba PCCB ina mipaka ya utendaji wa kazi na inafanya kazi kwa maelekezo kutoka kwa Rais. Kwa hiyo kama mtuhumiwa akitetewa na Rais basi PCCB haiwezi kumgusa kwa kuwa Boss alishaagiza asiguswe.

Je, kwa vigezo vyako hiyo ndiyo credibility ya PCCB? Wanaacha kuchunguza mambo ya maana yenye ushahidi unao onekana wanaenda kuhangaika akina ole Porkwa kwenye bar.

Labda kama unaongelea credibility ya PCCB kwenye kushughulikia walimu wakuu, watendaji wa kata, makarani wa mahakama za mwanzo na mahakimu wa mahakama za chini lakini siyo ku-deal na cases kama alizoziainisha Dr Slaa kwenye tuhuma zake.
 
Mgonjwaukimwi,

Nakubaliana na wewe mzee kuwa Slaa kachemsha; na kwa sheria za Tanzania ametenda kosa la jinai; kwanza ametoa kauli za uchochezi; pili amesema uongo; tatu amekashifu viongozi wa serikali, akiwemo Raisi wa nchi..tena anendelea...

Kinachonishangaza zaidi ni vile hao waliokosewa wamenyamaza..hii ndio ilikuwa opportunity yao ya kumnyamazisha kwa kumfungulia hayo makesi; kwa kunyamaza kwao wanatoa picha kuwa:

1. Madai yake ni ya kweli hivyo wakienda tu mahakamani atatoa ushahidi (huo unaoutaka wewe hapa)ambao utazidi kuharibu mambo.

2. Wametuma watu (pengine wewe na mimi) tulete vichokoo hapa na kwingineko ili kupata data how much the guy knows..baadae waangalie kama wanaweza kujaribu kujibu mapigo

3. They were taken by suprise ..bado wanapumua na kuwasiliana na wanasheria wao

Zake ni kutaka ushahidi ambao Slaa anawajibika tu kuutoa mahakamani?

Kwenye political platform anachotakiwa ni ku-raise awareness ya wananchi, na ufafanuzi angetoa tu kama mmoja wa waathirika (sorry, sio wa ukimwi) wangemtaka kufanya hivyo.

Nina hakika Slaa has something up his sleeve, and if any of the listed ones wants to taste how deep the water is; let them ask for evidence before a court of law..so far, their silence means consent.
 
Mwendapole kula 5!

Viongozi wote waliotajwa bado wanatafakari issue nzima na iko wazi kwamba imewaelemea na ndiyo maana hata Mkono (mwanasheria maarufu) ambaye alishawahi kutishia ThisDay na Kulikoni amekaa kimya bila kujibu mapigo ya kutaka defamation au apology.

Dalili za serikali kuelemewa niliziona tangu Mh. Marmo alipowataka wapinzani wapeleke ushahidi kwenye vyombo vya dola. Baadaye Mzee Kingunge akasema ni uzushi tu kwa kuwa wapinzani wanataka kuipaka serikali matope. Approach ya kujibu tuhuma nzito za safari hii ni tofauti kabisa na ile ya rushwa ya Mkapa ya milioni 900 ambayo ilisemwa na Mrema na Masumbuko Lamwai kule Temeke.

May be bado ni mapema kwa watuhumiwa kujitetea wao wenyewe na hivyo wanapima kina cha maji ili waone kama wanaweza kuogelea na wakapona au waache ili wasije wakazama. I hope Dr. Slaa na wapinzani wamejiandaa vya kutosha katika hayo mapambano na nina uhakika kwamba lazima watakuwa na mambo mengi.

Swala la BoT halijaanza leo, kitendo cha Spika wa Bunge kutishia kupeleka vielelezo polisi kwa kisingizio kwamba vimegushiwa na baadaye akawa kimya kina ashiria kwamba kuna nondo nzito kwenye hivyo vielelezo. Nina uhakika kwamba kama kungekuwa na nondo za ubabaishaji leo hii hilo swala lingekuwa mikononi mwa polisi. Mpaka leo hii sijamsikia Spika Six wala Katibu wa Bunge Bwana Foka wakiongelea swala la hoja ya Dr. Slaa.

Hizo zote ni dalili kwamba safari hii wameshikwa pabaya na wakikosea step inawezekana wakateleza na mweleka wake unaweza kuwa mkubwa sana. Ngoja tuendelee kuona mambo yanavyozidi kwenda na hatimaye tuone mwisho wa hii picha!
 
Kuna ushahidi wa kutosha ndio maana kila mtu anasema kuwa anataka apelekewe ushahidi, hii ni dalili kuwa hawa jamaa wameiba na wanataka kwanza kuona huo ushahidi ili waanze kuuangalia na kujua kama wamegundulika ama laa ili waweze kwenda mahakamani.

Angalieni pia thread mpya ya wafisadi walivyojieleza ndio utajua kuwa hawa jamaa wameiba na wameshikwa pabaya na Dr. slaa .

Mnaobeza kweli ninyi ni watu msiolitakia mema taifa hili.

Soma alichosema chenge,. kama hutaona aibu bais wewe ni miongoni mwao ama unafaidika na wizi huu .
 
Kama akina marehemu Socrates na Aristotle wakiamka leo na kuona jinsi neno demokrasia linavyotumiwa vibaya, watasikitika sana na labda kulibadilisha maaana.

Tanzania hakuna demokrasia na wababe ndio wanatawala na mifano hai inaonekana na hakuna wa kufanya lolote.

Katika demokrasia iliyokomaa tuhuma kama hizo za ufisadi zinapoletwa basi mhusika au wahusika wote hutakiwa kuandaa barua za kujiuzuru haraka na kupisha watu wengine waadilifu.

Kwa jinsi nnavyoona kwa sasa watuhumiwa wanachanganua namna ya kuzijibu tuhuma hizo, ingawa mheshimiwa Chenge kwa mshangao wangu amethibitisha kwamba nae anakula milo mitatu ya ubunge,uwaziri, na huo ukurugenzi!

Ni lazima mheshimiwa Raisi awaambaie jamaa wajiuzuru kuipa nafasi sheria ichukue mkondo wake ikiwezekana aongee hata na Makamu mheshimiwa Shein si ndio anakaimu kwa sasa?

Wananchi tunatakiwa tujifunze kutofautisha sera za wagombea uchaguzi na mwaka 2010 ndio uwe mwaka wa watu wanaotetea maslahi ya taifa kupewa nafasi.
 
Katika posting yangu nimechambua ushahidi wa Dr Slaa ambao ameutoa dhidi ya watu aliowatuhumu. Na conclusion yangu ni kwamba tuhuma alizotoa ni mzito lakini ushahidi hafifu. Nilitegemea wachangiaji wenzangu waonyeshe wapi ushahidi wa Dr Slaa una strength, badala yake wachangiaji wengi wanajaribu kushawishi kwamba Dr Slaa anayajuwa mengi zaidi ya aliyoyasema. Mimi sio mtaalamu wa ndoto wala sio mpiga ramri, hivyo basi nachambua kile kilichosemwa.

Je Dr Slaa ni mjinga? Sidhani, ila kwa hili anastahili kuitwa mjinga machoni mwangu. Mwenye ushahidi wakutosha, mzalendo mpenda haki na maendeleo ya watu habembelezwi kuutoa, wala hakimbilii waandishi wa habari. Badala yake anakwenda mahakamani, na bungeni ikiwezekana. Dr Slaa hajafanya hivyo, badala yake ana-adaa wananchi wanaolia kwa kipindi kirefu juu ya rushwa.

JF tumekuwa mstari wa mbele kuipiga vita rushwa, ila kwa mshangao naona tuna double standard. Amina Chifupa (R.I.P)alipokatazwa kutoa press conference, JF kulikuwa na movement ya kushinikiza aruhusiwe. Nilitegemea JF kuwe na movement ya kumshinikiza Dr Slaa afungue kesi dhidi ya hao aliowatuhumu...tunapinga rushwa kweli JF ama tuna ibwekea tu?

Kama Dr Slaa ana ushahidi mzito zaidi ya huo alioutoa (kama wachangiaji wanavyojaribu kutuongopea)anasubiri nini kuwashitaki? Vyama kama CUF, TLP, NCCR, viko wapi wakati vina kila ushahidi dhidi ya watuhumiwa? Hivi hii sio BINGO kwa wapinzani? Nadhani Dr Slaa ameamua kutupa makengeza tuzani ukungu ni moshi.

Sasa wachangiaji wengine humu wamenichekesha, wakisema kwamba wanataka viongozi walioshutumiwa wamjibu Dr Slaa. Nadhani JF tunataka kuona malumbano badala ya suluhisho. Hatufiki tunakokusudia. Ukimshika mwizi unampeleka kwa pilato, wala hauhitaji kumhoji kama kaiba au lah, mana kama kuna possibility kwamba hajaiba basi kuna possibility kwamba sio mwizi. Na mwizi ana haki ya kukaa kimya unapomuhoji na akasubiri kwenda kujibu kwa pilato. Hasipokujibu na ukaishia kutokwenda kwa pilato haina mana kaiba, hata kama utampiga.

Kadhalika inanishangaza kuona kwamba JF tunalazimisha viongozi washutumiwa wamjibu Dr Slaa. Kana kwamba rushwa inapigwa vita kwa malumbano. By the way, nitawaona viongozi wa ccm wajinga endapo watajibu shutuma zenye ushahidi wa kuokotezea.

Again, uzalendo wa Dr Slaa sijauona katika hili. Huwezi kuitwa mpenda haki na mtetea wananchi wakati huo huo ushahidi ambao ungetoa maovu ya viongozi unauweka kibindoni, na unasubiri ubembelezwe uutoe. Huwezi kuitwa kiongozi bora kwa kuanzisha malumbano na wala rushwa kupitia waandishi wa habaru, badala ya kuwapeleka kwa pilato. Rushwa haipigwi vita kwa malumbano ya kisiasa.
 
Katika posting yangu nimechambua ushahidi wa Dr Slaa ambao ameutoa dhidi ya watu aliowatuhumu. Na conclusion yangu

What a crap...

umechambua nini zaidi ya kuuliza maswali tu .... CCM kwa kujipa majina makubwa .... mara mchambuzi mara nimechambua... hakuna ulichochambua hapa .....

ila kwa hili anastahili kuitwa mjinga machoni mwangu...... anakwenda mahakamani, na bungeni ikiwezekana.
tuna ibwekea tu?

Matusi hayatasaidia kumaliza rushwa....

Hii case haiendi bungeni wala mahakamani.... case hii ni kwa wananchi na wajichukulie sheria mkononi..... bungeni kwa kina mdhihiri wakaanzishe ngonjera kwenye issue muhimu?

Nadhani Dr Slaa ameamua kutupa makengeza tuzani ukungu ni moshi.

Mko nani hapa?

Hatufiki tunakokusudia. Ukimshika mwizi unampeleka kwa pilato, .. By the way, nitawaona viongozi wa ccm wajinga endapo watajibu shutuma zenye ushahidi wa kuokotezea.

ukimshika mwizi unafanya walichofanya polisi Arusha... unachapa risasi kama mvua. utawashangaa CCM vipi wakati wewe ni CCM?

Rushwa haipigwi vita kwa malumbano ya kisiasa.

Kama sio malumbano wewe unachofanya hapa ni nini?
 
Mgonjwa wa ngoma,

Nakubaliana na wewe kwa kuwa Dr Slaa anao ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani watuhumiwa njia pekee kwa sasa ni kwa yeye na kundi lake la wapinzani kufungua kesi mahakamani.

Hii habari ya kuzunguka mikoani na "kuwaelimisha" wananchi kuhusu uozo wa rushwa wa CCM kimsingi ni kujenga false-hope kwa wananchi na ku-gain cheap political popularity.

Nionavyo hapa at the end of the ni maumivu tu kwa wananchi wa kawaida kwani wanapewa matumaini kuwa wapinzani wanayafanyia kazi masuala ya rushwa ya CCM wakati ukweli hakuna kinachofanyanyika zaidi ya blah blah tu.

Inasikitisha kuona kuwa Dr Slaa anadai kuwa wanawasubiri watuhumiwa wafungue kesi ya kashfa ili wao waende kupambana nao huko huko mahakamani. Kwa mtindo huu tunashuhudia mazingaombwe matupu hapa kwani CCM ni smart sana ktk siasa za ma intrigue hizi washasema wao wanawapuuza wapinzani, hii maana yake nini, maana yake ni acha wapayuke as long as hawana guts za kwenda mahakamani there is nothing to worry abt.

Hoja kuwa kufungua kesi za namna hii Tanzania kuna mlolongo mrefu haina mashiko na imejikita ktk misingi legevu sasa. Its well known kuwa Demokrasia ina gharama na gharama zenyewe ni pamoja na mambo kama haya. Hatuwezi kuwaachia manyang'au wanaiba nchi kwa kisingizio eti kufungua kesi kuna utararatibu mrefu hii inasikitisha sana.

Ndio wakati mwingine unaona siasa za Bongo ni usanii mtupu CCM wasanii na wapinzani ndio wasanii zaidi..
 
Back
Top Bottom