Argument # 1,
Dr Slaa acha kutufanya wajinga baba, wewe tueleze nini Balali alifanya haswa. Aliruhusu? Aliidhinisha? alinyamazia? Kama wewe mwenyewe huna uhakika na alichofanya Balali sisi wasomaji ndo inakuaje?
In my view, Dr. Slaa, ni mwananchi na kiongozi mwenye uchungu na nchi yake, yeye professionally, sio mwanasheria, au Prosecutor ama mtaalamu wa sheria, lakini ameweza kutumia elimu yake kwa manufaa ya umma at large, ambao ni sisi mimi nilifikiri ni wajibu wetu kuyatafakari kwa makini aliyoyasema, na ikibidi kuyafanyia uchunguzi hata wa kisayansi, ili kuhakikisha ukweli ulipo na uongo ulipo,
badala ya kuja na general statement kuwa aache kutufanya wajinga!,
badala yake tungesema ahsante kwa kutupatia changamoto na sasa kazi kwetu kuutafuta ukweli wa uliyosema, FULL STOP!
Dr. Slaa, hatufanyi wajinga kwa sababu anaanza na kusema wazi kuwa viongozi anaowatuhumu wamehusika kwa
"namna mbali mbali" za ujanja ambazo matokeo yake yamekuwa kuliletea hasara taifa letu, na namna mbali mbali anazozisema zinajumuisha kuruhusu, kuidhinisha, au kunyamaza, kwa makusudi huku wakijua wazi kuwa matokeo ya vitendo hivyo vitatu alivyovitaja, vitawaletea faida wao binafsi kwa migongo ya sisi wananchi, kwa njia ambazo ni kinyume na sheria zetu,
Kisheria ilitakiwa by now serikali yetu iwe tayari imetangaza kuunda kamati maalum ambayo ni independent kuchunguza madai haya ya Dr. Slaa, kwa nini mpka leo serikali haijafanya hivyo? Mbona kwenye tuhuma za minofu ya samaki serikali iliunda kamati mara moja, this time mbona wamekuwa na kigugumizi?
Kisiasa viongozi waliotuhumiwa walitakiwa wawe tayari wamejibu kwenye public kwamba hawahusiki na hizi tuhuma na kwamba watapigana kufa na kupona kusafisha majina yao, sasa ni kwa ni ni hawafanyi hivyo kama aliyoyasema Dr. Slaa ni ujinga?
Mwalimu Nyerere na Kawawa, walipotuhumiwa kuwa ni wezi na Kambona pale Jangwani, the next day tuliwasikia wakijibu kuwa tuhuma hizo ni za uongo na kwamba iwapo Kambona anao ushahidi autoe hadharani, au aombe radhi, ama sivyo watamshitaki kwenye sheria kusafisha majina yao, lakini Kambona akashindwa kutoa ushahidi na kuomba radhi haraka,
in this case Dr. Slaa ametoa ushaidi sasa ni wakati wa viongozi waliotuhumiwa kujibu mapigo na kupigana na ushahidi, na sio sisi wananchi tusiojua chochote kuhusiana na tuhuma hizo kuja na hizi general statement za kumuita Dr. Slaa ni mjinga, maana wananchi wenye akili watashindwa kuelewa nani hasa ni mjinga hapa, maana kisheria hapa viongozi wetu waliotuhumiwa wanahitaji kujisafisha tena kwa kisheria na kisiasa, kwa kupigana na huu ushahidi mzito uliotolewa na wananchi/kiongozi, tena wa upinzani mwenye very limited resources au tools za kufanyia uchunguzi mzito kama huu wa uhalifu wa viongozi wa juu kwa sisi wananchi walalahoi,
Mkuu MgonjwaWaukimwi, ninaheshimu sana uwezo wako accademically wa kuchamnbua ishus, lakini ninaomba nikuambie one thing, ni kweli kama ulivyosema kuwa kuna mjinga hapa lakini I bet you with my life sio Dr. Slaa!