List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

List of Shame: Mrema na Slaa wazungumzia Vigogo wa Ufisadi Tanzania

Thats is JF we dare to offend openly.... teh teh teh....
 
Kuna habari za ndani kabisa zisizo rasmi zinasema muungwana anakula sahani moja na wote waliohusika na rushwa wakati wa Mkapa. Inasemekana hata Mkapa mwenyewe yuko matatani. Nasikia wanatakiwa kurudisha walichochota na kuficha nje ya nchi. Hata Balali nasikia kaambiwa asiguse faili lolote Benki Kuu hadi uchunguzi ukamilike. Actually amefukuzwa kazi kimya kimya.
 
Kuna habari za ndani kabisa zisizo rasmi zinasema muungwana anakula sahani moja na wote waliohusika na rushwa wakati wa Mkapa. Inasemekana hata Mkapa mwenyewe yuko matatani. Nasikia wanatakiwa kurudisha walichochota na kuficha nje ya nchi. Hata Balali nasikia kaambiwa asiguse faili lolote Benki Kuu hadi uchunguzi ukamilike. Actually amefukuzwa kazi kimya kimya.

Another spinning? Lolote litakalofanyika litawavunjavunja CCM katika makundi mengi zaidi. Ndo maana tunawapongeza kina Dk. Slaa kwa utumishi mwema.
 
MKONO AJIBU MAPIGO KWA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.
-Slaa muongo
-Adai ushahidi alioutoa ni feki
-Afichua mawakili wanaoidai BOT kesi ya mdai mfu
-Asema shughuli zake BOT sio kwa kesi moja tu

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono amejibu mapigo ya Dk. Willbrod Slaa kuhusu tuhuma dhidi yake na kusema kiongozi huyo wa CHADEMA ni muongo.

"Slaa hana silaha...huyu alikuwa kanisani enzi zake inashangaza anasema uongo. Huyo (Slaa) ni muongo, kama mimi amenitungia yote hayo, naamini na wengine kafanya hivyo," alisema jana Mkono alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake.

Mkono ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma alisema tuhuma zote zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake hazina ukweli na kuwa lengo la kiongozi huyo wa upinzani lilikuwa kuwadanganya wananchi.

Akifafanua kuhusu tuhuma hizo, Mkono alisema madai ya Dk. Slaa kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia, siyo sahihi.

Alisema katika kesi hiyo ambayo aliipokea mwaka 2003, amefanikisha mambo mengi ikiwemo kuokoa fedha za serikali zilizokuwa zichukuliwe na wadai na ambazo zina walakini ndani yake na kuwa hatua hiyo imemzushia chuki miongoni mwa mawakili.

Mkono alisema kuna kampuni ya mawakili (majina tunayahifadhi) ambayo katika madai yake ya awali ya Aprili 3, 2003 iliomba kulipwa dola 9,917,850 (sawa na sh. bilioni 11) kama gharama za kuendesha kesi hiyo.

Aliongeza kuwa: "Kampuni hiyo hiyo ilipofika Juni 6, mwaka huu, iliomba kulipwa dola 19,835,701 (sawa na sh. bilioni 25.4) kuhusiana na kesi hiyo ambayo muhusika alifariki dunia muda mrefu uliopita."

"Sasa hapo nani ni mfisadi. Waandaishi mtapima wenyewe, mimi naendelea kutetea BOT ili fedha za walipa kodi ambao ni wananchi isiende bure," alisema Mkono na kuwa anafanya shughuli nyingi mbalimbaliza BOT mbali ya kesi hiyo.

Kuhusu kuhusika kwake na kampuni kama vile Azania Agricultural Enterprises, Liberty Leather Shoe Ltd, Azania Eximco na mengineyo, Mkono alisema hausiki nayo kwa maana ya kuwa na hisa au kuwa mkurugenzi wake.

Katika kuthibitisha hilo, alitoa taarifa kuhusu ukaguzi wa kampuni hizo kwa maana ya wana hisa na wakurugenzi wake kama ilivyotolewa na BRELA wiki hii.

Kuhusu kampuni za Oxford Services Ltd na Marcus Ltd, mbunge huyo alikanusha kuwa mkurugenzi au mwenye hisa na kufafanua kuwa alikuwa wakili wa kampuni hizo.

"Haya ni mambo ya ajabu sana. Hivi mtu kuwa wakili wa kampuni au wa mtu ni dhambi au ndiyo unakuwa mfisadi," alihoji Mkono na kuwa katika biashara za kampuni hiyo miongoni mwa waliochukua fedha na kupata matatizo ni Chavda.

Alisema kutokana na matatizo aliyopata Chavda, alitakiwa kufukuzwa nchini mara moja, lakini kutokana na taaluma yake alimtetea kwa mujibu wa sheria na kuhoji iweje wakili ahusishwe na dhambi ya mtuhumiwa.

"Kila mtu ana haki ya kutetewa. Wapo wauaji wamefanya makosa, lakini wana haki ya kutetewa...hata hivyo wakili anayemtetea mtu wa aina hiyo hawezi naye kuitwa muuaji," alisema Mkono na kuwa baadhi ya mambo hawezi kuyazungumza hadharani kwa undani kwa kuwa kama wakili kuna miiko ya kazi.

Mkono alitumia fursa hiyo kueleza ukweli kuhusu suala la kampuni ya City Water na kuwa katika kesi kwenye Mahakama ya Kimataifa nchini Uholanzi ambayo inashughulikia usuluhishi wa migogoro, kamwe hakupata kumuona.

"Huyu mwingine anayeitwa Tundu Lissu, sikumuona na wala simfahamu kwa kuwa kule mimi nilikuwa naongoza jopo la mawakili wa serikali," alisema Mkono.

Katika tuhuma mbalimbali walizozitoa kwenye mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam ambapo Dk. Slaa na Lissu walikuwa wasemaji wakuu, Lissu alitajwa kama mmoja wa mawakili wa serikali katika shauri la City Water.

Akihitimisha kwa ujumla tuhuma dhidi yake, Mkono alisema waliotoa madai hayo anahisi wanamuonea wivu kutoka na mafanikio katika kazi yake na jinsi anavyojitahidi kupeleka maendeleo jimboni mwake Musoma Vijijini.

"Nimemuita Slaa, lakini amegwaya na kwa jinsi anavyosema uongo huenda ningemchapa makonde,"alisema huku akionyesha kusikitishwa na tuhuma hizo.


Imetolewa kwenye Gazeti la Uhuru 21/10/07.
 
Aende MAHAKAMANI asilete ngonjera hapa.

Kukimbilia kwenye vyombo vya habari wakati umetukanwa si kawaida ya Mafisadi wa Tanzania.

Soo hili lingekuwa na pa kukwepea Mkono angefungua Kesi mara moja.

Tuhuma za ufisadi zimewakolea ipasavyo hapakaliki. Safari hii mtasema yote bila kujitambua.
 
Huyo mzee kibaragashia chekundu anamdanganya nani?

Mbona this day walimuandika vyema anavochota mabilioni BOT kiasi kwamba malipo ya wakili yanazidi pesa zinazo tetewa?? Tena nadhani hiyo thread ilikuwepo pia hapa JF!

Asitufanye sie ni wasahaulifu namna hiyo!

Mbinafsi mkubwa anatanguliza maslahi yake mbele bila kujali maslahi ya taifa, kutetea wawekezaji na kutuingiza mikataba mibovu kama ile ya NBC!
 
1.
Kila mtu ana haki ya kimsingi ya kutathmini ushahidi na kutoa conclusion Field Marshall ES,
Nashukuru kwamba bado tunaendelea kukata ishu huku tukielimishana/kueleweshana na kuipa jamii ya JF mitazamo mbali mbali ya jambo husika.

Tathmini ya ushahidi inatolewa na wataalamu wa sheria, au mahakama na sio mimi na wewe, unless wewe na mimi ni watuhumiwa au mawakili wa watuhumiwa, kama Wakili mtuhumiwa Mkono, alivyofanya leo, ni muhimu sana kuipa JF mitizamo mbali mbali ya ishus, lakini isiwe ni njia ya ku-abuse the luxury, just because JF wananchi wengi wanaikosoa serikali basi kwa mwananchi mmoja kutoa tathmini isiyoendana na ishu ili tu iwe tofauti na the usual maana forum inahitaji mitizamo mbali mbali ni hoja hafifu sana mkuu wangu!



2.
That said, hoja yako ya msingi kwamba mimi na wewe ni watazamaji tu na kwamba hatuwezi kutoa tathmini zetu isipokuwa mahakama ni hoja hafifu mno. Kama unavyosema ndivyo basi nakushauri uondoe neno DEBATE kwenye kamusi.

Hoja yangu ni ya msingi sana na ndio maana hata Spika wa bunge wa CCM, anakubaliana nayo, baada ya kuipitia hii orodha kama mimi na wewe tulivyofanya, ameamua kuwa kuna ushahidi unaohitajika kuchambuliwa na wataalam kama Mwanasheria mkuu wa serikali, ndipo ataamua kama kuna ishu kweli, na ndio msimamo wangu kuwa mimi na wewe hatujui ukweli wa kilichofanyika na ambacho hakikufanyika katika maelezo ya DR. Slaa, kwa hiyo wanaohusika kwanza waipitie na kutoa maoni yao, na inaweza kuwa mahakamani ndio tunapoweza kutoa conclusion, kama kuna ushaidi au hakuna, lakini sio at this stage, tunachoweza kutoa ni political analysis kutokana na orodha hii ya Dr. Slaa, lakini sio hukumu za kisheria kama ulivyofanya mkuu, siasa na sheria ni vitu viwili tofauti na hilo limethibitishwa na msimamo wa Spika wa CCM on this ishu!

Kuhusu neno debate, huwezi kulilazimisha kutumika pasipotakiwa, so far hii ishu ya Dr. Slaa bado ni ishu ya siasa, ushahidi ni ishu ya sheria ambayo ni mapema sana kuizungumzia, mpaka watuhumiwa watakapo jitokeza kama alivyojitokeza mtuhumiwa mmoja tayari ambaye ni mwanasheria, ukisoma maneno ya Mkono on this ishu, ukasema hakuna ushahidi then tutakuwa na a true debate kama bado ninaamini upo, kwa hiyo hoja ya kufuta neno debate, labda uichukue mwenyewe back!


3.
Hivi ulipobandika list ya Dr Slaa ulitegemea kwamba wasomaji wasome tu kama bibilia bila kutoa uchambuzi wao?

Nilitegemea wananchi watoe mishangao yao na analysis zao kisiasa, au kama binadamu na wananchi wa Tanzania, lakini sikutegemea kuwa watatoa hukumu za kisheria based on one side story, kama ulivyofanya mkuu wangu!

Hata Biblia huwa inatolewa uchambuzi, ndio maana kuna makanisa yenye viongozi mashoga na mengine hayana kabisaa!


4.
Hoja hujibiwa kwa hoja, kama MMKJJ anavyosema....ila naona mzee mwenzangu concept hii ndo kwanza unai-abuse. Badala ya kujibu hoja zangu kwa kueleza strength za ushahidi wa Dr Slaa,

Strength za ushaidi wa Dr. Slaa, so far hauwezi kuwepo maana the whole thing inahitaji kuchambuliwa na wataalamu kwanza ili kujua wapi zipo criminal charges na wapi kuna maoni tu ya kisiasa, na huwezi fanya hivyo bila kwanza kuwahoji watuhumiwa unless wewe ni mmoja wa watuhumiwa wenyewe, au wakili wa hao watuhumiwa. Strength za charges za Dr. Slaa zinaweza kuonekana pale tu tutakapokuwa na rebuttal toka kwa watuhumiwa, ndio maana hoja yangu kwako nimeilekeza kwenye general ishu yako ya ushaidi, na sio hoja ambazo kwangu ninaziona kuwa ni imaginations tu, kwa hiyo hakuna abuse yoyote as of your claim!


5.
naona unarukia character assassination kwa kudai kwamba nimetoa uchambuzi kwa lengo la kuonyesha education credential zangu....I think Field Marshall ES you have more to offer to JF than this. You have my trust in your wisdom when it comes to JF but sometimes your lowest points reduce your JF wisdom to nothing.

Hiyo mkuu, ilikuwa kujibu hoja yako kuwa kuna wananchi wanachekesha hapa wanapodai kuwa watuhumiwa wajibu tuhuma za DR. Slaaa, je wananchi hapa forum kuchekesha unaiona ni kujenga character za wananchi hapa forum? The rst ni mazungumzo baada ya habari au ni kelele za mlango huwa hazinizuii kulala, na hazinizuiii kumkoma nyani giladi hapa, tena kiroho mbaya!


6.
Then katika posting yako unamwingiza Mugongo-Mugongo katika kujaribu kunifanya niamini kwamba Mugongo-Mugongo akikubali jambo basi na mimi nikubali. Naamini kwamba una utashi wa kujuwa kwamba Mugongo-mugongo ni mtu mwenye mawazo na msimamo wake unaojitegemea, kadhalika na mimi.

Nimesema hoja za Mugongo, huwa ana hoja nzito za kuwakosoa Zitto na Freeman, na zinakubalika hapa, hiii ya kwako ya ushahidi wengi hapa tunaikataa kwa sababu haijitoshelezi, na sio mahali pake mkuu maana wakati wake bado ila unakuja!

7.
JF hatushawishi watu kwa kutoa reference ya watu tuliofanikiwa kuwashawishi katika jambo fulani. Kesho naweza kukubaliana na wewe, keshokutwa nikapingana na wewe na kukubaliana na MMKJJ, wala sitasema kwamba kwakuwa MMKJJ alikubaliana nami basi ni budi wewe nawe pia ukubaliane nami.

Hiii ndio ile kitu ninaiita kulia mbweha! mbweha! mbweha! ili usaidiwe na watu hapa, Mugongo ametajwa kukufahamisha tu for your future refference kuwa wananchi hapa hawakupingi tu kwa sababu una hoja ya kuitetea serikali, hapana maana kuna kina Mugongo ambao huitetea serikali na hoja zao zinaheshimika hapa forum!

8.
All in all mzee mwenzangu, sikubaliani nawe kwamba niwe mtazamaji bila kutoa uchambuzi wa ushahidi wa Dr Slaa. Kama unapingana na uchambuzi wangu, it is very simple; leta wakwako. Na hilo tu ndilo litanishawishi vinginevyo. Kweli uchambuzi wangu ni wamitaani, kama ulivyodai, ila ni bora ukasema hivyo baada ya kutoa uchambuzi wa ofisini....nisaidie kwa kunipa uchambuzi unaouna ni wamaana. Sio kunitaka nizibe kinywa na nisubiri mahakama. Mahakama itatoa uamuzi wa mwisho, na it is possible ikaamua kwamba Dr Slaa ana ushahidi mzito, bado nitakuwa na uchambuzi wangu, na conclusion yangu, na wala haitakuwa mwisho wa debate.

Mimi nitautoa wapi ushahidi ambao bado haujatolewa na waliotuhumiwa? Spika emshindwa kufanya uchambuzi amepeleka ishu kwa mtaalamu mwanasheria mkuu, sasa sembuse mimi mwananchi wa kawaida? Sasa wewe kuwa na ushahidi kwenye hii stage basi na wewe ni mtuhumiwa au wakili wa watuhumiwa, na ndio maana ninapingana na uchambuzi wako kuwa unless ukinithibitishia kuwa wewe ni mtuhumiwa sitakuwa na pingamizi kuwa una ukweli,

otherwise ni mpaka kesi hii itakapokwenda mhakamani, au watuhumiwa watakapotoa rebuttal, ndio nitakujibu kuhusiana na hoja ya ushahidi kama upo au haupo, maana os far nimesoma maneno ya Dr. Slaa peke yake, ninahitaji pia kusoma maneno ya upande wa pili ili niamue kama ushahidi upo au haupo, na sasa hivi nitasoma maneno ya Wakili/Mtuhumiwa Mkono, na nitaamua kma akweli ushaidi upo au hakuna na nitasema, hapa hapa!

Otherwise mkuu ahsante kwa hii useful debate, na tuendelee kukata ishus, ila for now ninatafuta rebuttal toka kwa watuhumiwa kwanza, ndipo nitaendelea na hii debate kwenye upande wa sheria, for now nitaendelea na kuikata ishu hii on siasa side yake!
 
1. DR. Slaa anasema:-

6. NIMROD ELIREHEMA MKONO

Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.

Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu.


Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme' iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: "Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)


Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: "Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila.

Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa.

Majibu Ya Mtuhumiwa Wakili Mkono:-


MBUNGE wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono amejibu mapigo ya Dk. Willbrod Slaa kuhusu tuhuma dhidi yake na kusema kiongozi huyo wa CHADEMA ni muongo.

Mkono ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma alisema tuhuma zote zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake hazina ukweli na kuwa lengo la kiongozi huyo wa upinzani lilikuwa kuwadanganya wananchi.
Akifafanua kuhusu tuhuma hizo, Mkono alisema madai ya Dk. Slaa kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia, siyo sahihi.


Wakuuu huu ni mfano mdogo wa utata wa hii ishu, DR. Slaa anamtuhumu Wakili/Mbunge Mkono, akitumia madai ya msingi yaliyotolewa na mwenyekiti wa kamati ya bunge iliyomchunguza Mkono na BOT, sasa tazama majibu ya Mkono, je ni kweli yanafanana na the charges?
 
mkono.jpg

Naona akisisitiza jambo, jeee ni kweli anaweza mapambano au just anazuga tu, maana keshapima nyakati na kugundua sasa sooo?
 
Nimrod Mkono kama mwanasheria uliyebobea nenda mahakamani kajisafishe.

Ukweli unauma, ni kweli umeshiriki kutuibia, unachokifanya sasa jimboni mwako ni kuwapatia wananchi makombo.

kama kweli wewe sio mwizi, wewe kama mwanasheria wa kimataifa kama unavyojiita unaonashida gani kumburuza Slaa mahakamani. kumbuka Slaa katoa ushahidi ndani ya serikali na kachambua kazi zako BOT. Wewe ni mwizi, mhujumu, na mfisadi wa fedha za wananchi. Pipi unazo zitoa sasa hivi jimboni mwako ni baada ya kuvimbiwa na wajinga ndio waliwao.

Mkono sidhani kama kuna kuoneana wivu kwenye swala la kuiba fedha za umma, kumbuka Slaa ni mmoja kati yetu sisi waliahoi ambaye amepata nafasi ya kusema hadharani tupo wengi wenye uchungu kuliko unavyofikiria.

Heko Slaa sisi walia hoi tupo nyuma yako.
Ninaomba yeyote mwenye simu ya Mkono anipatie tafadhali ilinifanye mahojiano naye.
 
Ukitupa jiwe kwenye mbwa wengi anaye bweka ndiyo aliyepigwa na jiwe. Hapa inaelekea kibabu kimepigwa na jiwe. Guess what? kinaiona milango ya gereza. Uwiii, uwii, uwiiiiii!
 
Kweli mambo yanakwenda kombo. Huyu jamaa hana sababu yoyote ya kubwata bwata, alitakiwa amburuze Slaa mahakamani na hata kama Slaa hana hiyo fedha ya kumlipa, atakua amejisafisha jina lake. Anaogopa na hata serikali inaogopa kumpeleka Slaa mahakamani kwa sababu hawajui ni mabomu gani mengine atayalipua akipandishwa kizimbani. BAHARI IMECHAFUKA!
 
Mkono: Ninalipwa dola 500 kwa saa

* Ashangaa Dk. Slaa kutokamatwa


Na Irene Mark
TUHUMA zilizotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), dhidi ya viongozi kadhaa wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinachukua sura mpya kila kukicha na jana mmoja wa watuhumiwa aliibuka na kutoa majigambo huku akiwaingiza watu wengine kadhaa katika shauri hilo.

Aliyefanya hivyo alikuwa ni Mbunge wa Musoma Vijijini na mwanasheria maarufu nchini, Nimrod Mkono (CCM), ambaye mbali ya kutangaza kuwa amekuwa akivuna kiasi cha dola 500 za Marekani kwa saa (karibu sh 650,000) kutokana na kazi yake ya uwakili, aliwalaumu mawakili wawili akiwataja kuwa watu wanaoonea wivu mafanikio yake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkono aliwavuta katika wavu wa tuhuma hizo mawakili wawili maarufu wa kampuni moja jijini, na kubainisha kuwa wamekuwa wakimtumia Dk. Slaa, kutokana na vita kati ya kampuni yake (Mkono) na wao kuhusu kesi moja inayohusisha mabilioni ya shilingi.

Mkono alisema sababu za yeye kuingizwa kwenye orodha ya wabadhirifu, ni ushindi alioupata wa kuiendeleza kesi ya Devram Valambhia na Kampuni ya usafirishaji ya Equipment.

Kesi hiyo imekuwa ikiendelea kwa miaka 20 sasa na Mkono jana alikiri kuwa analipwa mabilioni ya fedha kutokana na kuisimamia.

Katika mkutano huo, Mkono alidai kuwa Dk. Slaa anatumiwa na mawakili wa kujitegemea, Moses Maira na Mabere Marando, ambao walishindwa katika jitihada zao za kuipata kesi hiyo yenye malipo makubwa.

Hata hivyo, alipozungumza na gezeti hili jana, Marando alikanusha tuhuma hizo zilizotolewa na Mkono na kueleza kuwa hajawahi kushindwa katika kesi hiyo.

Marando alisema wakati wanaisimamia kesi hiyo (yeye na Maira) waliishinda serikali baada ya gavana kukutwa na hatia na kupewa hukumu ya kifungo au kulipa faini, na aliokoka kwenda jela baada ya kulipa faini ya sh 400,000 mbele ya Jaji Massati.

“Sioni sababu ya Mkono kulipwa mamilioni ya fedha kila mwezi kutoka serikalini wakati kesi ilishamalizika,” alisema Marando.

Mkono aliwaambia waandishi wa habari kuwa, yeye ni wakili ghali kwani huwa analipwa dola 500 kwa saa kila siku wakati wa saa za kazi kama wakili katika kesi hiyo, hali inayosababisha chuki dhidi ya mawakili walioshindwa.

“Hii chuki yote mnayoiona inatokana na kesi ya Valambhia inayoshughulikiwa na kampuni yangu… mwaka 2003 Mabere na Maira walipoona wanashindwa wakaibana serikali na kumtaka Gavana Daudi Balali akamatwe, walitaka kumfunga gavana hawa mabwana.

“Walichokuwa wanataka Valambhia alipwe deni feki ili wapinzani wagawane hizo fedha… nilipoanza nayo mwaka huo huo nilijiwekea malengo, kwanza gavana asikamatwe katika hilo nilishinda.

“Jingine ni kwamba, serikali ianze mwanzo ili kujua chimbuko la kesi hii… napo nilishinda kwani mahakama ilianza kusikiliza kesi hii. Kesi hii ni ya siku nyingi sana, lakini hatuwezi kumwachia mhalifu, lazima tuendelee kudai,” alisema Mkono huku akionyesha baadhi ya nyaraka zinazohusu kesi hiyo kwa waandishi wa habari.

“Ndiyo… ninalipwa dola 500 kwa saa kila siku ya kazi na fedha hiyo nalipwa kwa saa nane,” alisema Mkono na kuongeza kuwa kesi hiyo inasimamiwa na wanasheria saba. Alifafanua kuwa watatu wapo hapa nchini, wawili wapo Ireland na wengine wawili wapo Jamhuri ya Watu wa Czech, ambako kesi hiyo inasikilizwa.

Kuhusu malipo ya wanasheria wengine wanaosimamia kesi hiyo, Mkono alisema wanaoishi nje ya nchi hulipwa dola 200 (karibu sh 260,000) kwa saa kila siku ya kazi kwa saa nane na kusisitiza kuwa hawezi kuiachia kesi hiyo, kama wanavyotaka wapinzani, hadi imalizike.

Aidha, Mkono alieleza kushangazwa kwake na kutokuwepo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, katika mkutano huo na waandishi wa habari kwani alimualika.

“Nashangaa kwa nini Father (Padri) Willibrod Slaa hajahudhuria mkutano huu, nilimwalika lakini simuoni… najua angekuja tungeshikana mashati hapa hapa, maana lazima tungebishana kuhusu hili,” alisema.

Hata hivyo, Dk. Slaa aliliambia gazeti hili kuwa, hakuwahi kupokea mwaliko wowote kutoka kwa Mkono kuhudhuria mkutano huo.

“Mkono ni rafiki yangu na anaijua namba yangu ya simu… ukweli ni kwamba wewe ndiyo wa kwanza kuniambia habari hizi, huyu bwana hajaniita kwa namna yoyote.

“Kwanini nikatae wito? Siwezi kwenda sehemu ambayo sijaitwa, nielewe hivyo… nasema Mkono hajaniita, aache kuwadanganya wananchi, sijapokea wito kutoka kwake,” alisisitiza Dk. Slaa kwa njia ya simu.

Lakini katika mkutano wake, Mkono alisisitiza: “Huyu (Dk. Slaa) ni Father wa Kanisa Katoliki, lakini anasema uongo mbele ya Watanzania milioni 35, hii ni kunichafulia jina langu kwa sababu ninawakilisha Watanzania kama 400,000 hivi, wanashangaa Mbunge wao kuitwa fisadi.

“Nafikiria hatua za kuwachukulia walioniita fisadi, sasa nimshitaki nani hapa, Slaa au Chadema au hili gazeti (alilionyesha gazeti la kila wiki la Mwana Halisi lililoandika na kuchapisha jina lake kama mtafuna nchi)… hata nikiwashitaki hawawezi kunilipa,” alisema huku akiwaonyesha waandishi waliokuwepo gazeti hilo.

Aidha, Mkono alisema kuwa alisikitishwa na kitendo cha kumtaja rais wa nchi kuwa mmoja kati ya mafisadi na kuonya kuwa, uhuru wa kuzungumza uliopo nchini, usitumiwe vibaya kwa kusema uongo na kutoa mfano wa yaliyosemwa na Dk. Slaa.

“Wapinzani wameniweka kwenye ‘list of Shame’ (orodha ya mafisadi), rais wa nchi naye yumo… kwa lugha hiyo unawaambia Watanzania wote wasimheshimu rais wao, ndiyo anavyosema Father Willibrod Slaa,” alibainisha.

Alisema zipo sheria za nchi zinazosema kuwa, ni kosa kumtukana rais akiwa madarakani, lakini anashangaa ni kwa nini wapinzani hawajakamatwa hadi sasa.

“Rais wetu yupo Marekani, kaenda kuombaomba huko tupate japo fedha za MCC kwa maendeleo ya nchi yetu… wenzetu wanamwekea red carpet (zulia jekundu), hapa tunamtukana, hii si vizuri, ni makosa sana kufanya hivi.

“Sipo hapa kumsemea rais… mimi si msemaji wake, lakini kwa vile amewekwa kwenye list of shame na kwamba yeye ni mkuu wa nchi imebidi nilizungumzie.

“Huyu father anasema Mkono ni mkurugenzi wa makampuni (aliyataja baadhi yake na kuonyesha orodha ya wakurugenzi wa kampuni hizo kutoka BRELA). Kampuni zote alizozitaja huyu father hazipo, ni kampuni za uongo, wakurugenzi wake ni Wahindi,” alisema na kuongeza kuwa mchango wake katika nchi ni mkubwa na kwamba bila yeye hajui Tanzania ingekuwa wapi sasa.

Alisema alitoa ushawishi mkubwa kwa kushirikiana na wenzake kuhakikisha yanajengwa mahoteli makubwa.

“Kazi ya wakili ni kutetea wahalifu, hivi na mimi ninapotetea wahalifu nakuwa mhalifu? Nilimtetea Chavda asiondoke nchini nikafanikiwa na mimi ni mhalifu?” Alihoji Mkono na kumtaka Dk. Slaa aache kuudanganya umma, badala yake aendelee na kesi inayomkabili ya uchaguzi katika jimbo lake.
 
Absolutely stupid hata top barristers wanaolipwa $500.00 huku majuu wanahesabika itakuwa yeye. Hii serikali imeoza na hivi viwango ni extortion. Shame on him!

Nategemea TRA analipa kodi ya hizo pesa anazochaji.
 
This was probably the worst thing to say among the millions of hungry and impoverished Tanzanians. Unajua, ingawa huyu jamaa amesoma na kubobea katika sheria, inaonekana ame-panic na ameshindwa kujua aseme nini ili kujitetea. You can't just blubber kwa watanzania kwamba benki yenu ya BoT inanilipa mamilioni ya saa moja wakati mtanzania wa kawaida kiasi hicho hakipati mpaka afanye kazi miaka 10. What an old fart this asshole has become.I feel sooooooooooo sorry for him.
 
Kwani anatetea kiasi gani cha pesa hadi alipwe kiasi hicho? maana tuseme hiyo kesi ikiendeshwa kwa miaka mitano atalipwa kiasi ghani? Duh kweli jamaa anavuna pesa ya wananchi. Hata huruma hana? Any way hata wewe ukipata dili kama hili utakula tuu na watu wanaendelea kufa njaa na maradhi. Kweli hii dunia haiko fair.
 
Unaweza kucheka kwa ajili ya hasira!

Hivi kweli Mkono anaona ni sawa kabisa kukuri kwamba analipwa dola 500 yaani zaidi ya shilingi laki sita kwa saa moja? tena analipwa masaa nane??

Nashindwa hata andika! nina hasira sana!!!
 
sasa inabidi aweke mahesabu yake wazi kwa ummah tujue hiyo kampuni yake inavyopata fedha na inavyotumia pesa hizo au iunde tume maalumu kuchunguza pesa zake hapo ndio haki itatendeka au mnasemaje jamani ?

hata hii benki yake , ni vizuri iwekwe wazi pesa zimetoka wapi mpaka wamefungua
 
Hivi kuna mtu anaweza kupata english translation ya hizi tuhuma za Dr. Slaa? Kama itapatikana, watu waliopo Marekani tunaweza kuji mobilise ili kuomba marafiki na ndugu zetu wapiga kura wa kimarekani ili wawashawishi masenator na representatives wao ili wazuie misaada kwa Tanzania. Muungwana amekua akipewa sifa nyingi za bure tu na Wamarekani ambao hawajui ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya serikali yake ya Mafisadi.

KAMA ENGLISH VERSION INAWEZA KUPATIKANA, TUNAOMBA IBANDIKWE HAPA ILI WATU TUANZE KAMPENI.
 
Unaweza kucheka kwa ajili ya hasira!

Hivi kweli Mkono anaona ni sawa kabisa kukuri kwamba analipwa dola 500 yaani zaidi ya shilingi laki sita kwa saa moja? tena analipwa masaa nane??

Nashindwa hata andika! nina hasira sana!!!

Muhimu ni masaa mangapi alicharge kwenye hiyo kesi? Uthibiti wa hayo masaa ukichunguza ni mdogo sana na alifanya nini kwenye hayo masaa? Kila mahali WIZI WIZI WIZI ama kweli ipo siku.
 
Back
Top Bottom