Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna habari za ndani kabisa zisizo rasmi zinasema muungwana anakula sahani moja na wote waliohusika na rushwa wakati wa Mkapa. Inasemekana hata Mkapa mwenyewe yuko matatani. Nasikia wanatakiwa kurudisha walichochota na kuficha nje ya nchi. Hata Balali nasikia kaambiwa asiguse faili lolote Benki Kuu hadi uchunguzi ukamilike. Actually amefukuzwa kazi kimya kimya.
Kila mtu ana haki ya kimsingi ya kutathmini ushahidi na kutoa conclusion Field Marshall ES,
Nashukuru kwamba bado tunaendelea kukata ishu huku tukielimishana/kueleweshana na kuipa jamii ya JF mitazamo mbali mbali ya jambo husika.
That said, hoja yako ya msingi kwamba mimi na wewe ni watazamaji tu na kwamba hatuwezi kutoa tathmini zetu isipokuwa mahakama ni hoja hafifu mno. Kama unavyosema ndivyo basi nakushauri uondoe neno DEBATE kwenye kamusi.
Hivi ulipobandika list ya Dr Slaa ulitegemea kwamba wasomaji wasome tu kama bibilia bila kutoa uchambuzi wao?
Hoja hujibiwa kwa hoja, kama MMKJJ anavyosema....ila naona mzee mwenzangu concept hii ndo kwanza unai-abuse. Badala ya kujibu hoja zangu kwa kueleza strength za ushahidi wa Dr Slaa,
naona unarukia character assassination kwa kudai kwamba nimetoa uchambuzi kwa lengo la kuonyesha education credential zangu....I think Field Marshall ES you have more to offer to JF than this. You have my trust in your wisdom when it comes to JF but sometimes your lowest points reduce your JF wisdom to nothing.
Then katika posting yako unamwingiza Mugongo-Mugongo katika kujaribu kunifanya niamini kwamba Mugongo-Mugongo akikubali jambo basi na mimi nikubali. Naamini kwamba una utashi wa kujuwa kwamba Mugongo-mugongo ni mtu mwenye mawazo na msimamo wake unaojitegemea, kadhalika na mimi.
JF hatushawishi watu kwa kutoa reference ya watu tuliofanikiwa kuwashawishi katika jambo fulani. Kesho naweza kukubaliana na wewe, keshokutwa nikapingana na wewe na kukubaliana na MMKJJ, wala sitasema kwamba kwakuwa MMKJJ alikubaliana nami basi ni budi wewe nawe pia ukubaliane nami.
All in all mzee mwenzangu, sikubaliani nawe kwamba niwe mtazamaji bila kutoa uchambuzi wa ushahidi wa Dr Slaa. Kama unapingana na uchambuzi wangu, it is very simple; leta wakwako. Na hilo tu ndilo litanishawishi vinginevyo. Kweli uchambuzi wangu ni wamitaani, kama ulivyodai, ila ni bora ukasema hivyo baada ya kutoa uchambuzi wa ofisini....nisaidie kwa kunipa uchambuzi unaouna ni wamaana. Sio kunitaka nizibe kinywa na nisubiri mahakama. Mahakama itatoa uamuzi wa mwisho, na it is possible ikaamua kwamba Dr Slaa ana ushahidi mzito, bado nitakuwa na uchambuzi wangu, na conclusion yangu, na wala haitakuwa mwisho wa debate.
6. NIMROD ELIREHEMA MKONO
Hoja ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu ni kuwa kesi hii haina muda maalumu wa kumalizika na hivyo inawezekana kabisa malipo ya wanasheria yakazidi kiasi cha fedha inachodaiwa Benki Kuu.
Kampuni ya mawakili ya Mkono & Co. Advocates imekuwa ikitajwa kuhusiana na kashfa kubwa za ufujaji na/au ubadhirifu wa fedha za umma kwa muda mrefu.
Kwa mfano, ‘Taarifa ya Uchunguzi Kuhusu Tuhuma Dhidi ya Makampuni ya Tanfarms Ltd., Makinyumbi Estates Ltd., Centrepoint Investments Ltd., na Arusha Farms Ltd. Yanayomilikiwa na V.G. Chavda Kuhusiana na Matumizi Mabaya ya Fedha za Debt Conversion Programme' iliyotolewa Bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi, Mheshimiwa Edward Oyombe Ayila mwezi Novemba 1994 ilisema yafuatayo kuhusu Mheshimiwa Nimrod Mkono: "Mhe. Spika si nia yangu kulichosha Bunge lako tukufu na hotuba ndefu lakini ni vizuri nikaelezea juu ya uhusiano unaotia mashaka kati ya V.G. Chavda na Mashamba yake na Subash Patel mwenye makampuni ya DECO ART, MM Motors, MM Garage, Hotel Sea Cliff, City Bureau De Change na Nimrod Mkono, Wakili wa kujitegemea ambaye pia ni Mkurugenzi katika makampuni ya AZANIA AGRICULTURAL ENTERPRISES, LIBERTY LEATHER SHOE LTD., AZANIA EXIMCO, n.k. (AIMS GROUP OF COMPANIES)
Baada ya kuelezea uhusiano huo ulivyokuwa Mheshimiwa Ayila alimalizia kwa kusema yafuatayo: "Mheshimiwa Spika, ni vigumu kabisa katika hali ya kawaida kwa mtu yeyote kuamini kwamba makubaliano haya na uhusiano uliojitokeza hapa haukuwa wa hila.
Chavda kwa kupitia wakili wake Nimrod Mkono, aliomba Mahakama Kuu kuzuia kabisa shughuli za Kamati (permanent injunction). Aidha ni wakili huyo huyo ambaye ameshuhudia uuzaji wa deni la Deco Art (reassignment) kwa Chavda. Mheshimiwa Spika, hali hii ukiitazama kwa undani utaona kwamba pengine kuna kitu kinafichwa.
Mkono ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma alisema tuhuma zote zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake hazina ukweli na kuwa lengo la kiongozi huyo wa upinzani lilikuwa kuwadanganya wananchi.
Akifafanua kuhusu tuhuma hizo, Mkono alisema madai ya Dk. Slaa kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imekuwa ikilipa malipo makubwa kwa Mkono & Co. Advocates hasa yale yanayohusu kesi ya Valambhia, siyo sahihi.
TUHUMA zilizotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA), dhidi ya viongozi kadhaa wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinachukua sura mpya kila kukicha na jana mmoja wa watuhumiwa aliibuka na kutoa majigambo huku akiwaingiza watu wengine kadhaa katika shauri hilo.
Aliyefanya hivyo alikuwa ni Mbunge wa Musoma Vijijini na mwanasheria maarufu nchini, Nimrod Mkono (CCM), ambaye mbali ya kutangaza kuwa amekuwa akivuna kiasi cha dola 500 za Marekani kwa saa (karibu sh 650,000) kutokana na kazi yake ya uwakili, aliwalaumu mawakili wawili akiwataja kuwa watu wanaoonea wivu mafanikio yake.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkono aliwavuta katika wavu wa tuhuma hizo mawakili wawili maarufu wa kampuni moja jijini, na kubainisha kuwa wamekuwa wakimtumia Dk. Slaa, kutokana na vita kati ya kampuni yake (Mkono) na wao kuhusu kesi moja inayohusisha mabilioni ya shilingi.
Mkono alisema sababu za yeye kuingizwa kwenye orodha ya wabadhirifu, ni ushindi alioupata wa kuiendeleza kesi ya Devram Valambhia na Kampuni ya usafirishaji ya Equipment.
Kesi hiyo imekuwa ikiendelea kwa miaka 20 sasa na Mkono jana alikiri kuwa analipwa mabilioni ya fedha kutokana na kuisimamia.
Katika mkutano huo, Mkono alidai kuwa Dk. Slaa anatumiwa na mawakili wa kujitegemea, Moses Maira na Mabere Marando, ambao walishindwa katika jitihada zao za kuipata kesi hiyo yenye malipo makubwa.
Hata hivyo, alipozungumza na gezeti hili jana, Marando alikanusha tuhuma hizo zilizotolewa na Mkono na kueleza kuwa hajawahi kushindwa katika kesi hiyo.
Marando alisema wakati wanaisimamia kesi hiyo (yeye na Maira) waliishinda serikali baada ya gavana kukutwa na hatia na kupewa hukumu ya kifungo au kulipa faini, na aliokoka kwenda jela baada ya kulipa faini ya sh 400,000 mbele ya Jaji Massati.
Sioni sababu ya Mkono kulipwa mamilioni ya fedha kila mwezi kutoka serikalini wakati kesi ilishamalizika, alisema Marando.
Mkono aliwaambia waandishi wa habari kuwa, yeye ni wakili ghali kwani huwa analipwa dola 500 kwa saa kila siku wakati wa saa za kazi kama wakili katika kesi hiyo, hali inayosababisha chuki dhidi ya mawakili walioshindwa.
Hii chuki yote mnayoiona inatokana na kesi ya Valambhia inayoshughulikiwa na kampuni yangu mwaka 2003 Mabere na Maira walipoona wanashindwa wakaibana serikali na kumtaka Gavana Daudi Balali akamatwe, walitaka kumfunga gavana hawa mabwana.
Walichokuwa wanataka Valambhia alipwe deni feki ili wapinzani wagawane hizo fedha nilipoanza nayo mwaka huo huo nilijiwekea malengo, kwanza gavana asikamatwe katika hilo nilishinda.
Jingine ni kwamba, serikali ianze mwanzo ili kujua chimbuko la kesi hii napo nilishinda kwani mahakama ilianza kusikiliza kesi hii. Kesi hii ni ya siku nyingi sana, lakini hatuwezi kumwachia mhalifu, lazima tuendelee kudai, alisema Mkono huku akionyesha baadhi ya nyaraka zinazohusu kesi hiyo kwa waandishi wa habari.
Ndiyo ninalipwa dola 500 kwa saa kila siku ya kazi na fedha hiyo nalipwa kwa saa nane, alisema Mkono na kuongeza kuwa kesi hiyo inasimamiwa na wanasheria saba. Alifafanua kuwa watatu wapo hapa nchini, wawili wapo Ireland na wengine wawili wapo Jamhuri ya Watu wa Czech, ambako kesi hiyo inasikilizwa.
Kuhusu malipo ya wanasheria wengine wanaosimamia kesi hiyo, Mkono alisema wanaoishi nje ya nchi hulipwa dola 200 (karibu sh 260,000) kwa saa kila siku ya kazi kwa saa nane na kusisitiza kuwa hawezi kuiachia kesi hiyo, kama wanavyotaka wapinzani, hadi imalizike.
Aidha, Mkono alieleza kushangazwa kwake na kutokuwepo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, katika mkutano huo na waandishi wa habari kwani alimualika.
Nashangaa kwa nini Father (Padri) Willibrod Slaa hajahudhuria mkutano huu, nilimwalika lakini simuoni najua angekuja tungeshikana mashati hapa hapa, maana lazima tungebishana kuhusu hili, alisema.
Hata hivyo, Dk. Slaa aliliambia gazeti hili kuwa, hakuwahi kupokea mwaliko wowote kutoka kwa Mkono kuhudhuria mkutano huo.
Mkono ni rafiki yangu na anaijua namba yangu ya simu ukweli ni kwamba wewe ndiyo wa kwanza kuniambia habari hizi, huyu bwana hajaniita kwa namna yoyote.
Kwanini nikatae wito? Siwezi kwenda sehemu ambayo sijaitwa, nielewe hivyo nasema Mkono hajaniita, aache kuwadanganya wananchi, sijapokea wito kutoka kwake, alisisitiza Dk. Slaa kwa njia ya simu.
Lakini katika mkutano wake, Mkono alisisitiza: Huyu (Dk. Slaa) ni Father wa Kanisa Katoliki, lakini anasema uongo mbele ya Watanzania milioni 35, hii ni kunichafulia jina langu kwa sababu ninawakilisha Watanzania kama 400,000 hivi, wanashangaa Mbunge wao kuitwa fisadi.
Nafikiria hatua za kuwachukulia walioniita fisadi, sasa nimshitaki nani hapa, Slaa au Chadema au hili gazeti (alilionyesha gazeti la kila wiki la Mwana Halisi lililoandika na kuchapisha jina lake kama mtafuna nchi) hata nikiwashitaki hawawezi kunilipa, alisema huku akiwaonyesha waandishi waliokuwepo gazeti hilo.
Aidha, Mkono alisema kuwa alisikitishwa na kitendo cha kumtaja rais wa nchi kuwa mmoja kati ya mafisadi na kuonya kuwa, uhuru wa kuzungumza uliopo nchini, usitumiwe vibaya kwa kusema uongo na kutoa mfano wa yaliyosemwa na Dk. Slaa.
Wapinzani wameniweka kwenye list of Shame (orodha ya mafisadi), rais wa nchi naye yumo kwa lugha hiyo unawaambia Watanzania wote wasimheshimu rais wao, ndiyo anavyosema Father Willibrod Slaa, alibainisha.
Alisema zipo sheria za nchi zinazosema kuwa, ni kosa kumtukana rais akiwa madarakani, lakini anashangaa ni kwa nini wapinzani hawajakamatwa hadi sasa.
Rais wetu yupo Marekani, kaenda kuombaomba huko tupate japo fedha za MCC kwa maendeleo ya nchi yetu wenzetu wanamwekea red carpet (zulia jekundu), hapa tunamtukana, hii si vizuri, ni makosa sana kufanya hivi.
Sipo hapa kumsemea rais mimi si msemaji wake, lakini kwa vile amewekwa kwenye list of shame na kwamba yeye ni mkuu wa nchi imebidi nilizungumzie.
Huyu father anasema Mkono ni mkurugenzi wa makampuni (aliyataja baadhi yake na kuonyesha orodha ya wakurugenzi wa kampuni hizo kutoka BRELA). Kampuni zote alizozitaja huyu father hazipo, ni kampuni za uongo, wakurugenzi wake ni Wahindi, alisema na kuongeza kuwa mchango wake katika nchi ni mkubwa na kwamba bila yeye hajui Tanzania ingekuwa wapi sasa.
Alisema alitoa ushawishi mkubwa kwa kushirikiana na wenzake kuhakikisha yanajengwa mahoteli makubwa.
Kazi ya wakili ni kutetea wahalifu, hivi na mimi ninapotetea wahalifu nakuwa mhalifu? Nilimtetea Chavda asiondoke nchini nikafanikiwa na mimi ni mhalifu? Alihoji Mkono na kumtaka Dk. Slaa aache kuudanganya umma, badala yake aendelee na kesi inayomkabili ya uchaguzi katika jimbo lake.
Unaweza kucheka kwa ajili ya hasira!
Hivi kweli Mkono anaona ni sawa kabisa kukuri kwamba analipwa dola 500 yaani zaidi ya shilingi laki sita kwa saa moja? tena analipwa masaa nane??
Nashindwa hata andika! nina hasira sana!!!