mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
kwa tanzania biashara ya maji ya kunywa sio biashara ndogo kama unavyodhani kisa sio mtaji tu bali urasimu wa serikali yetu hapo mpaka TFDA wakupe kibali utapewa check list ya vitu kama 100 .watakagua mashine,kiwanda,watataka uajiri mtaalamu wa food processing mwenye shahada,gharama ya kufanya followup ya hizo chemicals za kuyatreat nk,muulize jaydee na maji yakeYeah kuwa na kiwanda cha maji sio lazima chupa utengeneze mwenyewe coz ni expensive mtambo wake....unaweza. ukatengeneza kisha ukaoda vyupa vya kufungaahia ukawa unafanya sealed tu.
Hapa ni lazima uwe na matenki. makubwa na dawa ni kuyachimba chini sababu ata uvunaji wa maji ya mvua utakuwa mrahisi. Mfano wa matenki tunayoifadhia uchafu majumbani then haya yanakuwa na muinuko kidogo mpaka juu. Ungekuwa umeshafika Handeni ungenielewa kirahisi wanafanya sana hii ya kuvuna maji ya mvua na kuhifadhi.
Kuhusu treatment ya maji mimi sio mtaalam huko ila nahisi lazima uwe na mtambo fulani mdogo wa kuvuta maji ,kuyachemsha na kuyachanganya. So ishu kubwa hapa ni hiyo. mashine. Na nchi hii ina tatizo sana la mitambo midogo nilienda sido pale nikakuta mimashine ya kusaga nafaka ndio imejaa.
Kuna mtambo nilikuwa natafuta niliangaika sana sasa imebidi nijichange niuagize nje coz nilienda sido mpaka na laptop nikawaonyesha video zake na kila kitu nilidownload wakaishia kunipiga danadana si makao makuu wala vingunguti wote weupe tu.