List ya wasanii wa Bongo ambao walipata umaarufu na mafanikio makubwa, lakini leo wako juu ya mawe

Sijawahi kuona mtu mpuuzi kama Mr Nice, niliwahi kwenda kwenye show yake zamani na mwisho wa show nilijua huyu mshamba soon mziki utamshinda na ataishia kufilisika, alipiga Minneapolis siku hiyo watu walikuwa wamejaa vibaya sana kuanzia wakenya, wazungu na west Africans wote walikuwepo, nyimbo zake maarufu wakati huo nafikiri zilikuwa kidari poa na ...i dont remember, kwanza akaanza na vibe mbaya sana akaingia baada ya midnight watu wakamind sana lakini wakampotezea ili show iendelee, badala ya kuimba na kupiga show akaanza kuongea ujinga kwenye stage na kibaya zaidi kiingereza kibovu hakuna anayemuelewa, then akaanza show akatupigia nyimbo hata hatuzijui, watu wakamwomba apige show ya zile nyimbo tunazojua, jamaa akasema leo ni nyimbo mpya tuu, watu wakamind sana na stimu za watu zikakata kabisa, akaimba nyimbo zake za ovyo hakuna anayecheza wala kumsikiliza, akaanza kupiga kelele mbona hamchezi basi mimi naondoka, watu wakachoka naye wakaanza kumzomea na kumwambia aondoke, badala ya show yakawa matusi baina yake na washabiki, zilirushwa beer, viti, maji na kila kitu ilibidi wamtoe kupitia mlango wa nyuma, baada ya hapo nasikia show zake zote States zilipigwa chini na sponsor wake, i hope kaacha kiburi na majivuno yake ya kishamba
[emoji709]
 
Mr Nice nasikia alikuwa anajaza vibunda kwenye buti ya gari. Inasemekana alikuwa na zaidi ya 1.5 billion kipindi hiko.

Kuna interview alifanyiwa na millard ayo akasema alikuwa anatumia pesa haswa yaani hadi pesa zinatoa machozi kwa hiyo hajutii kufirisika. Lakini ukiangalia usoni ni mtu mwenye majuto sana
 
1) Mr Nice - huyu Afrika mashariki nzima na baadhi ya nchi za kusini kama vile Malawi, Msumbiji na Zambia hakuna mtu ambae alikuwa hamjui. Mpaka watoto wadogo huko vijijini Malawi walikuwa wanaimba kidali poo. Miaka ya 2002 mpaka 2005 alipiga hela sana lakini akaishia kushusha zipu, leo hii anazurura tu mitaani hana mbele wala nyuma.

2) Ferouz - Nyimbo kama kamanda, barua, kwaherini aliyoimba na prof Jay zilimpa umaarufu mkubwa hadi kupelekea kutunzwa gari na aliekuwa raisi wa JMT wa wakati huo hayati Benjamin W Mkapa. Na yeye alishika sana hela enzi hizo. Lakini leo inasemekana mambo yake yamekwenda ndivyo sivyo kwahiyo ni kama vile ashapoteza

3) 20 Percent - Huyu nae alikuja vizuri japo kwa muda mchache. Alikuja na vibao vyake matata na ile style yake ya kukwaruza kwaruza sauti huku mistari akiwa kaipangilia vilivyo, pia ukijulimsha na movie yake iliyovunja rekodi. Akaendekeza endekeza mjani na togwa. Leo hii inasemekana ukikutana nae mtaani lazima akupige mkuki umuunge buku akanywe chai.

Wapo wengi lakini acha niwataje hawa wengine mtaongezea wenyewe wasanii waliopata umaarufu na mwisho kupaki juu ya mawe kama gari isiokuwa na matairi.
usiwacheke mkuu baadhi hujui walikumbana na nini,maana dunia ina uncertainity nyingi
 
Dah Hao wote uliowataja ni members wa kidonge FM
 
Mr Nice nasikia alikuwa anajaza vibunda kwenye buti ya gari. Inasemekana alikuwa na zaidi ya 1.5 billion kipindi hiko.

Kuna interview alifanyiwa na millard ayo akasema alikuwa anatumia pesa haswa yaani hadi pesa zinatoa machozi kwa hiyo hajutii kufirisika. Lakini ukiangalia usoni ni mtu mwenye majuto sana
Saizi angeweza kumzidi domo mbali kaabisa ni uzembe wake tu
 
1) Mr Nice - huyu Afrika mashariki nzima na baadhi ya nchi za kusini kama vile Malawi, Msumbiji na Zambia hakuna mtu ambae alikuwa hamjui. Mpaka watoto wadogo huko vijijini Malawi walikuwa wanaimba kidali poo. Miaka ya 2002 mpaka 2005 alipiga hela sana lakini akaishia kushusha zipu, leo hii anazurura tu mitaani hana mbele wala nyuma.

2) Ferouz - Nyimbo kama kamanda, barua, kwaherini aliyoimba na prof Jay zilimpa umaarufu mkubwa hadi kupelekea kutunzwa gari na aliekuwa raisi wa JMT wa wakati huo hayati Benjamin W Mkapa. Na yeye alishika sana hela enzi hizo. Lakini leo inasemekana mambo yake yamekwenda ndivyo sivyo kwahiyo ni kama vile ashapoteza

3) 20 Percent - Huyu nae alikuja vizuri japo kwa muda mchache. Alikuja na vibao vyake matata na ile style yake ya kukwaruza kwaruza sauti huku mistari akiwa kaipangilia vilivyo, pia ukijulimsha na movie yake iliyovunja rekodi. Akaendekeza endekeza mjani na togwa. Leo hii inasemekana ukikutana nae mtaani lazima akupige mkuki umuunge buku akanywe chai.

Wapo wengi lakini acha niwataje hawa wengine mtaongezea wenyewe wasanii waliopata umaarufu na mwisho kupaki juu ya mawe kama gari isiokuwa na matairi.
Daaah! Kwa feruzi umeniacha hoi, nyimbo ulizotaja kwa usahihi ni za Daz nundaz na yakwake umekosea jina "starehe"
 
Back
Top Bottom