Lisu atarudisha itikadi/Imani ya watu kwa CHADEMA. CHADEMA mpeni uenyekiti.

Lissu mwenyekiti, mbowe mgombea Urais hapo itakaa vizuri, Kwa maslah ya chama na taifa
Haahaa kwenye urais kura zitashuka Sana, kauli yake ya miaka 20 uongozini ni ya kukomaa imezua tafrani Sana mtaani
 
Bongo very special!, hata uwafanye nini, muda ukifika, ni unachukua..., unaweka...
P
Mimi naona ni sahihi tu kwa sasa hadi tutakapopata mbadala wake, vyama vya upinzani vilivyopo vinachoweza kufanya ni kutuelezea tu matatizo tunayoyaishi na kutujaza chuki kwa chama tawala basi binafsi sioni cha kunishawishi nione huyu ndio mbadala wa ccm.
 
Haahaa pole, uelewa tunatofautiana Sana, ukimsikiliza lissu vizuri unaona nchi mpya yenye mabadiliko inayomilikiwa na wenye nchi Yaani wananchi
 
Katiba ndio msingi wa uongozi
Kama Katiba itashindwa kudhibiti Tabia za viongozi kama uliyoitaja Basi inapaswa kurekebisha.

Mtu hapaswi kudhibitiwa na mtu mwingine. Mtu anatakiwa adhibitiwe kwa Sheria au Katiba
Katiba kazi yake sio kudhibiti tabia za viongozi, katiba huweka miingozo mikuu ya nchi pamoja na itikadi yake. Viongozi watabaki na tabia zao ila katiba itawapa muongozo wa namna ya kutenda.
 
..ni vile hamuwezi kuona madhara ya watu wa misimamo ya Lissu kwenye jamii ya watu km watanzania, namhurumia Lissu sababu hawezi kufanikiwa akipewa ridhaa kuongoza chama.
Kwa sasa lissu ndo wakati wake, stail ya mbowe ilifaa wakati wa kikwete
 
Tayari Moshi unafuka na makundi ndani ya chama yameshajionyesha, ile picha waliyopiga yeye na Mbowe na kusema hana nia ya kugombea uenyekiti ilikuwa imezima kelele za wengi na kuonyesha kuna muunganiko
Haahaa Kwa hyo shida ni kugombea uwenyekiti, kwani anajipa? SI wajumbe wataamua?
 
Katiba kazi yake sio kudhibiti tabia za viongozi, katiba huweka miingozo mikuu ya nchi pamoja na itikadi yake. Viongozi watabaki na tabia zao ila katiba itawapa muongozo wa namna ya kutenda.

Katiba ndio Sheria mama. Kupitia Katiba Sheria zote, kanuni na miongozo ya chama au taifa hutokea humo.
Katiba ndio mdhibiti wa Tabia za watu katika taasisi, chama au taifa ili kujenga mahusiano Bora.

Ndio maana tunahitaji Katiba mpya ya nchi. Ili kudhibiti baadhi ya Tabia zenye mapungufu za watawala.

Hivyo watu kama Tundu LISU ambao unawaona ni extremist wakiwa chini ya Katiba Bora u-extremist wao hautakuwa na madhara
 
Lissu hawezi kabisa kuiongoza chadema sababu ni mwendawqzimu na hana nguvu za kiuchumi kupambana na ccm
 
Hili jambo linashabikiwa na CCM zaidi kuliko wale wanaoitakia mema CDM.
Jambo lipi? Ukubali ukatae ccm wanaomba mbowe aendelee kuwa mwenyekiti chadema, lissu ccm wanamuogopa Sana, Kuna mwanaccm mzito kidogo alinitania akanambia siku mbowe akishinda, watakuwa na uhakika wa kupanga ushindi wa Samia mwakani
 
Kwa hiyo lengo la kugombea ni kupata wabunge wengi au kushinda urais?
Kwa kit kinachoitwa the political dynamics za siasa zetu, upinzani ni ubunge tuu na udiwani, rais bado lazima atoke CCM.
Shida moja moja akishinda urais atabadili katiba na kuongeza vipindi vya uongozi, maana atasema mitano ni ya kukomaa
Hili haliwezekani!.
P
 
Katiba huwa haibadili tabia za watu. Katiba hutoa mwingozo wa namna ya kutenda kwa maslahi mapana ya nchi. Tabia ya Trump ni tofauti kabisa na Biden lakini katiba ya Marekani sio kumbadilisha Trump afanane na Biden ila kutoa mwongozo wa utendaji.
 
Mmhhhh......! Don't you think that it's too early kupanga la mgombea urais wakati ndiyo kwanza kimbembe cha mwenyekiti kimeanza? Siasa ina twists and turns every now and then, muda ukifika ndiyo watausoma mchezo who will be the right candidate at that particular time.
 
Katiba huwa haibadili tabia za watu. Katiba hutoa mwingozo wa namna ya kutenda kwa maslahi mapana ya nchi. Tabia ya Trump ni tofauti kabisa na Biden lakini katiba ya Marekani sio kumbadilisha Trump afanane na Biden ila kutoa mwongozo wa utendaji.

Katiba na Sheria hazipo kwaajili ya kubadili Tabia Bali kudhibiti Tabia.
Nisome vizuri Mkuu.

Imani, falsafa na saikolojia ndio zinaweza kubadili Tabia
 
Haahaa Kwa hyo shida ni kugombea uwenyekiti, kwani anajipa? SI wajumbe wataamua?
Shida sio kugombea uenyekiti shida ni kuanza kuponda uongozi uliopo na kutoa siri za ndani...hapo ni amelianzisha tu baada ya kutangaza nia je akishindwa unategemea nini?
 
Haahaa pole, uelewa tunatofautiana Sana, ukimsikiliza lissu vizuri unaona nchi mpya yenye mabadiliko inayomilikiwa na wenye nchi Yaani wananchi
Ushajiuliza kwa nini baadhi ya watu humuona Lissu ni mwanaharakati mzuri ila hawaoni kuwa anaweza kuwa kiongozi mzuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…