Lisu atarudisha itikadi/Imani ya watu kwa CHADEMA. CHADEMA mpeni uenyekiti.

Lisu atarudisha itikadi/Imani ya watu kwa CHADEMA. CHADEMA mpeni uenyekiti.

Shida sio kugombea uenyekiti shida ni kuanza kuponda uongozi uliopo na kutoa siri za ndani...hapo ni amelianzisha tu baada ya kutangaza nia je akishindwa unategemea nini?
Ameponda nn mkuu? Siri Gani za chama? Usiri wa nn kwenye mambo ya umma? Mbona mnaipigia kelele ccm kwa usiri wa mikataba?😂😂
 
Ameponda nn mkuu? Siri Gani za chama? Usiri wa nn kwenye mambo ya umma? Mbona mnaipigia kelele ccm kwa usiri wa mikataba?😂😂
Mimi ni CCM mkuu ila najaribu kuwaonyesha ndugu zetu wa CHADEMA wanapokosea....huwezi ukasikia mwanasiasa yoyote wa CCM anayehama au kukosana kuongelea ya ndani...hao wakipewa nchi mtu wakikosana si wataanza kufunguka hata siri za nchi
 
Yepi ya ndani? Chama ni Mali ya umma, mambo aliyozungumza lissu ni muhimu kwa chama na taifa kiujumla, hata ccm yako mambo wanapaswa kujifunza kutoka hotuba ya lissu
 
Akichaguliwa itafuta ile mindset iliyopo kwamba Chama ni cha watu wa kaskazini.Lakini uoga wangu naona asilimia 110 ya watu wa kaskazini hakuna hata mmoja aliyemuunga mkono kwa kuwepo kwenye mkutano wake au wale maarufu mitandaoni kupost......wengi data ziko off kavisa kuhusu hilo suala
 
Yepi ya ndani? Chama ni Mali ya umma, mambo aliyozungumza lissu ni muhimu kwa chama na taifa kiujumla, hata ccm yako mambo wanapaswa kujifunza kutoka hotuba ya lissu
Hauwezi kukijenga chama kwa kuwapa washindani wako risasi za kukupiga ndio alichokofanya Lissu...CCM haina cha kujifunza kutoka kwa Lissu kwa sababu imeshamudu siasa za Afrika...haya mambo ya chama kuwa mali ya umma sijui uongozi ni kutumikia wananchi hayapo Afrika

1000017229.jpg
 
Hapana, acha inyeshe sasahivi ili TUONE PANAPOVUJA. Hatma yao ndio itakayoamua mustakabali wa uhai na uimara wa chama
Sidhani kama Mbowe kwa sasa yeye anapigania uhai na kukuimarisha chama. Lisu asinge lianzisha hili songombingo uchaguzi huu, kwasabu indicator zilishaonyesha kuwa Mbowe na toops lake wameshapanga mikakati yakumtupa nje ya uongozi, Yeye angeyaacha tu haya maamuzi yaendelee nakukaa pembeni kama walivyotaka, ili lije shinikizo la wanachama na siyo shinikizo lake. Siasa ni technics na tricks, Mbowe apigi kelele zozote kwasababu amesha jipanga na anajiamini, utakapo kuja uchaguzi Kama Mbowe atagombea Lisu apati hata 20% .Lisu washauri wake hawajapiga mahesabu vizuri. Mimi nimshauri Lisu kama Mbowe atagombea kwa kulinda Heshima yake na Uhai wa baadae wachama, safari hii asigombee cheo chochote, kwasabu, Mbowe ameshapanga safu yake yakufanya nayo kazi. Yeye awe kimya na kuwa mwanachama wa kawaida kama watampa ujumbe wakamati kuu apokee bila kinyongo aendelee kukijenga chama lakini ategemee vijembe na maudhi ya kila aina kwa kipindi hiki. Mbowe tayari amekwisha kuwa kama wakina Marando wa NCCR mageuzi kipinde cha Mrema kwa upande mwingine safari hii mtaona ata Dola itamlinda Mbowe. Yote kwa yote, Mtakap liona chukizo la uharibifu limeshakaa patakatifu ni wakati wakukimbia.
 
Mbowe akiendelea kua mwenyekiti basi CDM nayo ni wale wale tu..uwezi taka mabadiliko wakati ndani mwako ambadiliki
 
Mimi naona ni sahihi tu kwa sasa hadi tutakapopata mbadala wake, vyama vya upinzani vilivyopo vinachoweza kufanya ni kutuelezea tu matatizo tunayoyaishi na kutujaza chuki kwa chama tawala basi binafsi sioni cha kunishawishi nione huyu ndio mbadala wa ccm.
Kama kuna mambo yakielezwa kwa wananchi ni maovu kiasi kwamba watu wanajawa na chuki dhidi ya chama tawala unataka yafichwe wananchi wasiyafahamu ili wasijawe na chuki dhidi ya CCM?
 
LISU ATARUDISHA ITIKADI/IMANI YA WATU KWA CHADEMA. CHADEMA MPENI UENYEKITI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Watanzania ni watu ambao huwaamini kama wanaweza kuishi bila kuonewa. Bila kutetemekea watawala. Bila kuwa machawa wa wenye navyo.

Watanzania wengi huamini kuonewa, kudhulumiwa na Wakubwa ni HAKI yao.
Watanzania wengi wamejenga kasumba kuwa ukiwa na cheo unahaki ya kufanya chochote kwa wasionavyo.

Watanzania wengi ni conservative au tuseme wamedumaa na hawahitaji mabadiliko mazuri zaidi.

Watanzania wengi hawamaani katika utu, HAKI, ndio maana hawawezi kupigania HAKI Zao hata kwa kusema tuu.

Watanzania ndio watu pekee ambao hata wewe hapo unaweza jifanya Usalama wa taifa ukaenda kijiwe chochote ukamchukua mtu yeyote au ukampiga makofi mtu kwa kisingizio cha Usalama wa taifa na Watanzania wakakuangalia tuu

Watanzania wengi ndio watu pekee ambao unaweza kuwaweka benchi wakasugua wakisubiri huduma ya hospital au huduma yoyote na wasiwe kuhoji.

Tundu Antipas Lisu tunamhitaji kwa wakati huu ili kubusti akili za Watanzania. Kuamsha Ari.
Kung'arisha fikra,
Kuchochea Moyo wa kupenda haki na kuipigania.

Kuufanya ukweli uwe mwamvuli wa wananchi.

Kuondoa uchawa na Tabia mbaya za kujipendekeza.
Moja ya dalili ya ukosefu wa HAKI katika jamii ni uchawa na kujipendekeza.
Uchawa na HAKI havikai pamoja.
Uchawa na ukweli havikai pamoja.

Mtu yeyote anayejitambulisha na kujionyesha. kama Chawa hawezi kuwa mtenda HAKI.

LISU atarejesha imani ya watu kwenye vyama vya upinzani. Kama ilivyokuwa 2010-2015.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam
Lazima tubadilika,Neema ya Vyakula vingi inatufanya tujione huru na sawa,hata HAKI ikipotea sawa tuu.Huu ni ukosefu wa fikra!Umenena vyema.
 
Kuna tatizo la watu kuchanganya chama na watu, CCM kama CCM haina
Tatizo, ila ni kweli kuna wana CCM wachache ambao kweli ni mashetani lakini wana CCM wengi ni malaika na kwenye upinzani mashetani pia wapo!.
Nimeandika sana humu mambo ya malaika na shetani
P
Kama wanaunga hoja na kusifu kila kiongozi Wa CCM,hapo ni kipengere,lakini Mungu fundi tutafika tuu.
 
LISU ATARUDISHA ITIKADI/IMANI YA WATU KWA CHADEMA. CHADEMA MPENI UENYEKITI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Watanzania ni watu ambao huwaamini kama wanaweza kuishi bila kuonewa. Bila kutetemekea watawala. Bila kuwa machawa wa wenye navyo.

Watanzania wengi huamini kuonewa, kudhulumiwa na Wakubwa ni HAKI yao.
Watanzania wengi wamejenga kasumba kuwa ukiwa na cheo unahaki ya kufanya chochote kwa wasionavyo.

Watanzania wengi ni conservative au tuseme wamedumaa na hawahitaji mabadiliko mazuri zaidi.

Watanzania wengi hawamaani katika utu, HAKI, ndio maana hawawezi kupigania HAKI Zao hata kwa kusema tuu.

Watanzania ndio watu pekee ambao hata wewe hapo unaweza jifanya Usalama wa taifa ukaenda kijiwe chochote ukamchukua mtu yeyote au ukampiga makofi mtu kwa kisingizio cha Usalama wa taifa na Watanzania wakakuangalia tuu

Watanzania wengi ndio watu pekee ambao unaweza kuwaweka benchi wakasugua wakisubiri huduma ya hospital au huduma yoyote na wasiwe kuhoji.

Tundu Antipas Lisu tunamhitaji kwa wakati huu ili kubusti akili za Watanzania. Kuamsha Ari.
Kung'arisha fikra,
Kuchochea Moyo wa kupenda haki na kuipigania.

Kuufanya ukweli uwe mwamvuli wa wananchi.

Kuondoa uchawa na Tabia mbaya za kujipendekeza.
Moja ya dalili ya ukosefu wa HAKI katika jamii ni uchawa na kujipendekeza.
Uchawa na HAKI havikai pamoja.
Uchawa na ukweli havikai pamoja.

Mtu yeyote anayejitambulisha na kujionyesha. kama Chawa hawezi kuwa mtenda HAKI.

LISU atarejesha imani ya watu kwenye vyama vya upinzani. Kama ilivyokuwa 2010-2015.

Acha nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Dar es salaam
🙋‍♂️✍️🎯👌👍👊👏🤝🙏💐🎁🎖️🗼🏆🛡️
 
Mtu anayependa ukweli na kuufanya hawezi kuwa adui wa demokrasia.
Demokrasia ni kukubali nguvu ya ukweli

Mbowe ni kiongozi mzuri lakini sio katika mazingira ya sasa ya taifa lililokumbwa na uchawa, kujipendelea, umungumeza, na usultani
🎯💐🎁🤝🙏
 
Back
Top Bottom