Litambue Baraza la Mawaziri mwaka 2023 na Majimbo yao

Litambue Baraza la Mawaziri mwaka 2023 na Majimbo yao

MHE. SAMIA SULUHU HASSAN​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO​

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MHE. DKT. HUSSEIN ALI MWINYI​

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi

MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA - Jimbo la Ruangwa - Lindi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

MHE. KAPT GEORGE HURUMA MKUCHIKA - Jimbo la Newala Mtwara

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum)

MHE. JENISTA J. MHAGAMA - Jimbo la Peramiho Ruvuma

Waziri wa Nchi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA - Jimbo la Karagwe Kagera

Waziri wa Ulinzi

MHE. ANGELLAH J. KAIRUKI - Wa kuteuliwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

MHE. SELEMAN S. JAFO - Jimbo la Kisarawe Pwani

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)

MHE. PROF. JOYCE L. NDALICHAKO - Jimbo la Kasulu Mjini Kigoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)

MHE. GEORGE B. M. SIMBACHAWENE - Jimbo la Kibakwe Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)

MHE. PROF. MAKAME M. MBARAWA - Jimbo la Mkoani Pemba Kusini

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi

MHE. UMMY A. MWALIMU - Tanga Mjini Tanga

Waziri wa Afya

MHE. DKT. MWIGULU N. MADELU - Iramba Magharibi Singida

Waziri wa Fedha na Mipango

MHE. MHANDISI HAMAD Y. MASAUNI - Jimbo la Kikwajuni Mjini Magharibi

Waziri wa Mambo ya Ndani

MHE. DKT. STERGOMENA LAWRENCE TAX - Kuteuliwa

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

MHE. HUSSEIN BASHE - Jimbo la Nzega Mjini Tabora

Waziri wa Kilimo

Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko -Jimbo la Bukombe Geita

Minister Of Minerals

MHE. PROF. ADOLF. F. MKENDA - Jimbo la Rombo Kilimanjaro

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. NAPE M. NNAUYE - Jimbo la Mtama Lindi

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

MHE. JANUARI Y. MAKAMBA - Jimbo la Bumbuli Tanga

Waziri wa Nishati

Mhe. Dkt. Angeline Sylvester Lubala Mabula - Jimbo la Ilemela Mwanza

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MHE. DKT. DAMS D. NDUMBARO - Jimbo la Songea Mjini Ruvuma

Waziri wa Sheria na Katiba

MHE. DKT. DOROTHY O. GWAJIMA - Kuteuliwa

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

MHE. DKT. ASHATU K. KIJAJI - Jimbo la Kondoa Dodoma

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara

MHE. JUMA H. AWESO - Jimbo la Pangani Tanga

Waziri wa Maji

MHE. DKT. PINDI H. CHANA - Viti maalumu

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - Jimbo la Rufiji Pwani

Waziri wa Maliasili na Utalii
Katibu wa Balaza Chief Secretary Kwa nini umemuacha kwenye list? Tueleze Kusiluka ni WA wapi?
 
Rukwa 0
Katavi 0
Arusha 0
Kilimanjaro 0
Manyara 0
Simiyu 0
Shinyanga 0
Mbeya 0
Songwe 0

Kazi iendelee.
Mbeya yupo Naibu Waziri Atupele na Songwe yupo Naibu Waziri Kasekenya na yule msaliti wa CHADEMA.
 
Mbeya yupo Naibu Waziri Atupele na Songwe yupo Naibu Waziri Kasekenya na yule msaliti wa CHADEMA.

Wengine wapate mawaziri kamili hadi watatu lkn wengine wapate naibu waziri mmoja.
Sio sawa
 
Pamoja na kuwa mtu atokapo si kigezo lakini ukiangalia kajitahidi sana kubalance baraza lake. Naamini kajitahidi kwelikweli kwani nafasi ni chache kulingana na idadi ya mikoa.
 
baada ya kuona idada ya dini wanopenda kuwa wao tu serikalini wako wengi,roho hazitulii basi wameamia kwenye ukanda na umkao...Tanzania tunasafari ndefu ya kupiga hatua ya maendelea, viongozi wetu wana kazi kubwa sana kwa jamii hii kuiongoza....
 
Rukwa 0
Katavi 0
Arusha 0
Kilimanjaro 0
Manyara 0
Simiyu 0
Shinyanga 0
Mbeya 0
Songwe 0

Kazi iendelee.
Ondoa K'njaro jombaaa, yupo Mukenda,pamoja na Kina Mollel chawa wa mama huyu[emoji1787][emoji1787]
 
Kilimanjaro yupo Adolf Mkenda (Elimu)

By the way, mikoa iko zaidi ya 35 na mawaziri wanaotakiwa ni less than 26..

So, by any means Kuna baadhi ya mikoa haitatoa waziri hata kama wawe wapo wanaofaa...

Labda kama tunataka tuwe na Caninet ya mawaziri 40..!!

Pia, possibly hiyo mikoa inaweza kuwa imetoa manaibu au watu kwenye higher positions zingine..

NOTE: Kusema ukweli kuwa kiongozi mkuu mahali popote hususani uongozi mkuu wa nchi (yaani RAIS) ni kazi kwelikweli. Hakuna zuri waweza kufanya Kisha Kila mtu aka - appreciate...
Nipeni Mimi nitaifanya hiyo kazi unayosema ngumu na nakuhakikishia hakuna atakayelakamika. Nitaondoa matozo na maisha ya wananchi yatakuwa kama wako sayari ya Masi,
 
Hoja yako haina msingi kwasababu unakuta kwenye mkoa mmoja kuna mawaziri watatu alfumomwingie hamna waziri inamaana wabunge wote wa mkoa huo hawafai kuwa wazir
===Acha ubishi usio na kichwa wala miguu Kwa mambo ambayo facts zake ziko wazi mbele ya macho yako..!

===Msingi wa hoja uko hapa;

✓ Kwamba, wizara ziko 25 tu. Mikoa iko zaidi ya 35

✓ Unadhani ungekuwa wewe ndiye mteuzi ungewezaje kuhakikisha kuwa Kila mkoa unatoa waziri?

✓ Bila shaka ungeamua kuunda wizara zingine ili tu Kila mkoa upate waziri, au siyo Fauya ?

===Kuhusu mkoa fulani kuwa na wabunge wasio na sifa ya kuwa mawaziri, hilo linaawezekana Kwa sbb yote hayo yanategemeana na mteuzi anaangalia sifa/vigezo gani..
 
Rukwa 0
Katavi 0
Arusha 0
Kilimanjaro 0
Manyara 0
Simiyu 0
Shinyanga 0
Mbeya 0
Songwe 0

Kazi iendelee.
Baraza la mawaziri la JPM halikuwa na waziri kutoka Kilimanjaro hata mmoja, ni siasa zile zile tu. Uvumilivu ni wa muhimu sana,
 
Back
Top Bottom