Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Naangalia Bunge live asubuhi hii, kusubiria hotuba ya hali ya uchumi, ndio nikakumbuka kumbe leo ni siku ya Alhamisi, ni siku ya maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu, sasa naomba kuuliza, jee kuna uwezekano wa kukosekana kwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, kumepelekea kupunguza msisimko wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu hivyo sasa kipindi hiki kimekosa impact kama enzi zile za uwepo wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni? .
Enzi za uwepo wa kambi rasmi ya upinzani, kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu ilikuwa moto, sii ya kukosa, siku zote swali la kwanza lilitoka ama kwa kiongozi wa upinzani bungeni ama kwa mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani.
Je ni mimi tuu?, vipi nyinyi wenzangu? . Msikie JJ. Mnyika
View: https://youtu.be/r-SmiYZUOXc?si=VjwownS936rlz14K
Ushauri wa Bure kwa Mhe. Spika.
Pamoja na kutokuwepo kwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, kutokana na wapinzani kutokukodhi akidi, lakini kuna wapinzani bungeni, hivyo ili kurejesha msisimko wa Bunge la vyama vingi, wapinzani wote waliopo Bungeni waunde kundi la "the minority", to act kama kambi rasmi ya upinzani, hivyo kipindi cha maswali ya papo kwa papo kianze na maswali ya papo kwa papo swali la kwanza litoke kwa the minority.
Pia kitendo cha Chadema kutowatambua wale wabunge wake 19 na kuwaita covid 19, kumepelekea kuwavunja confidence wabunge wake machachari kama Mhe. Halima Mdee, Esta Bulaya, Ester Matiko and the like, wanaonekana wako wako tuu bungeni kwa ajili ya maokoto kwa kuvuta tuu bingo kusubiria Bunge kuvunjwa hapo mwakani.
Paskali