Live from EA Radio Super Breakfast: Mtangaza Nia Urais wa JMT Kupitia Chadema, Dr. Mayrose Majinge Yuko Live, Mubashara

Amefanya vizuri kuonyesha nia ya kugombea urais kupitia chama chake. Lakini inabidi afafanue kwa nini anaona kuna haja ya kuleta siasa safi nchini. Waambie wapiga kura ni nani au chama kipi kina siasa chafu? Chama chake au chama kingine? Na kwa nini anaona kina siasa chafu na atafanya nini kukisafisha?

Amandla...
 
Umbea UTAKUUWA we Mayalla aka Njaa, hamu yote ni kusikia jinsi huyo Dr atakavyo ivuruga CHADEMA. Acha mambo hayoo muda utapita tuuu.
 
Haya ni maigizo kabisa, CHADEMA hakuna Demokrasia. . . .Mayrose asitegemee kuungwa mkono na wanachama wa CHADEMA. Imagine apo tuu anaonekana msaliti tayari kwa kuonesha nia hiyo. Kikubwa zaidi anahatarisha maisha yake
Ni nani lakini kamuita msaliti? Wengi humu ni mashabiki na sio wanachama. Kwa kuwatuhumu wenzako kwa mauaji umeonyesha hauna tofauti na wale wanaomuita msaliti.

Amandla...
 
Hiv mkuu P,Ni fair kabsa kumuita mwanataaluma mwenzio ni kiazi?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni TISS, taarifa zake Kigogo2014 ameshazitoa. Msaliti. Kama hakuna.mgombea afadhali CDM isisimamishe mgombea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sioni kama ni tatizo mtu wa TISS kugombea urais kupitia vyama vya upinzani.

Kwa sababu TISS siyo ccm hivyo ni muhimu kuwa na watu wa aina hiyo kwenye chama.

Ina maana akitangaza Mwamunyange kugombea urais kupitia CDM mtamkataa kwa sababu ni former CDF ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naombea isiwe kama ya wakina Sumaye na Mwambe. Anatangaza nia kugombea nafasi ambayo kwa vyovyote vile hawezi kupata. Atakaposhindwa, analalamika kuwa mchezo mchafu umetumika kumnyima haki yake ya kugombea. Anahama chama, halafu anazunguka kukisema kuwa ametoka kwa sababu maisha yake yalikuwa hatarini na alikataa kutoa hongo ya ngono. Akifanya hivyo atakuwa hajawatendea haki watanzania na hasa wanawake wenzake. Akishindwa na kukubali kushindwa na kuunga juhudi za atakayeteuliwa kugombea na chama chake atajijengea heshima na sifa kubwa katika jamii.

Amandla...
 
TISS wanafanya kazi kwa ajili ya CCM. Siyo Tanzania , or for that matter Africa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…