Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Manispaa ya Iringa CHADEMA wanaongoza katika ngazi zote
Source: ITV
 
Arusha mjini: Chadema inaongoza katika kata 10, CCM kata 5 na TLP anaongoza kwenye kata 2.
 
Kaloleni naona ndiyo inaleta kigugumizi cha kutangaza matokeo huko A-town. Ila nina hakika hapo CCM imelala tu!
 
Moshi mjini kwa mzee Ndesa,

MwanaCBE said:
Mpaka sasa Moshi mjini Ndesambulo kata 18 kati ya 21. Sourse Star TV.

Zanzibar (By ITV),

Mji Mkongwe --CUF imechukua jimbo
 
zitto, any news from Ubungo, Tarime, Lissu, Sugu, Mdee, Komu, ?

Soma hii thread..majibu yote utapata

Kati ya hao kila kitu ni safi isipokuwa kwa Lissu na hatuna data za Komu
 
Hii ni taarifa ya mdau,

 
Naomba nimpongeze dada Regia na washindi wengine wote! Kwa wale ambao hawakupita, watambue kuwa wamepigana vita vitakatifu na huu ni mwanzo tu! Kila la kheri
 
Re: Matokeo ya Uchaguzi Mkoa wa Dar-es-Salaam


Mbezi Beach

Tangi Bovu - Urais
CCM 60,
CHADEMA 108,
CUF 4

Soko Jipya /Mbezi Beach Urais

Kituo namba 1
CCM 51,
CHADEMA 115,

Kituo namba 2:
CCM 63,
CHADEMA 100,

Dar-es -Salaam kwazidi waka moto
Source: Kiranga
 
Lusajo anaripoti:

Matokeo Vituo vya Utawala - UDSM

Vituo Sita (6) vya Utawala:

URAIS:
CHADEMA (Dr. Slaa) - 714
CCM (Kikwete) - 119

UBUNGE:
CHADEMA (Mnyika) - 730
CCM (Ngumbi) - 103​

Hata iweje, nitaprint hii na kuiframe... wasomi ni tofauti na wasio wasomi
 
...na pia jimbo la Rombo Selasini wa Chadema anaongoza kwa margin ndogo sana. SOURCE: Report ya star TV Hii ni taarifa ya mdau.

Kuna mdau alitoa confirmed report kwamba Mramba Chali. Sasa inakuwaje??
 
Kondoa Kaskazini hiyo...
Hili lilitegemewa sana, na kama kuna mtu anafuatilia siasa za kule... kuna udini wa kutisha.... yani hawataki hata kusikia john au peter... kuna kijana mmoja very effective walimchakachua simply because he was christian
 
Kuna mdau alitoa confirmed report kwamba Mramba Chali. Sasa inakuwaje??

Mkuu hizi data ni provisional..Kwa hiyo hakuna matokeo rasmi na kwa maana hiyo kila mdaru anarusha anachokipata toka source yake. Let's keep our fingers crossed.
 
Nafikiri inabidi tuwe tuangalia na muda ambao taarifa hizi zimetoka maana unaweza ukaona taaria kwako ikawa mpya lakini kumbe ilikuwa hewani toka majira ya saa tatu.

Siyo kila unachikiona kwa mara ya kwanza ni kipya. Wadau tuhabarishane updates. Consultant, Dark City, Indume yene na wengine vip!!!!! Tupo pamoja wazee
 
Musoma Mjini.
Urais:
CHADEMA inaongoza kata 9 out of 13
CCM inaongoza kata 2 out of 13
CUF inaongoza kata 1 out of 13

Ubunge: Mwenyekiti wa CCM Musoma mjini amekubali kuwa wameshindwa.
Source: ITV
 

Flow ya matokeo imepungua ila kuna taarifa mpya kuwa Mary Nagu huko Hannang' kapigwa chini na Rose Kamili (aliyekuwa mke wa Dr Slaa)
 
Bukoba umeme unakatika mara kwa mara lakini watu wamegoma kulala wala kuondoka kwenye vituo kuhofia kuchakachuliwa kwa kura.

Hii inatia moyo watu kulinda haki yao.
 
Jamani tutafutieni matokeo ya Bagamoyo kwa Shukuru Kawambwa walikotumia mil 700 kujengea matundu 4 ya choo, hali ikoje huko???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…