Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Elections 2010 Live From TV's: Upigaji wa kura, matokeo na yatokanayo

Kuna ugomvi unaonyeshwa ITV wa mawakala. CHADEMA wanadai kunyimwa haki ya kukagua kitambulisho. Anadai wanataka wasikilize namba tu badala ya kukagua. Msimamizi wa Mawakala wa CHADEMA kawa mbogo sana. Anadai lazima wapate nafasi wakague. Mambo ya Sinza kwa Mugabe hayo.

Aisee babangu huyu ndugu ana lafudhi ya kichaga amechachamaa kweli kweli.

Kituo changu walipata nafasi ya kukagua na pia kusikia kwa sauti.
 
Superman asante kwa picha nzuri za uchaguzi. Tafadhali endelea kutuhabarisha. Great job!
 
Kwa maoni yangu vijana safari hii tofauti na 2005 wamejitokeza kwa wingi sana kupiga kura.
 
Tunawashukuru Superman na Elli kwa kutuhabarisha. Keep it up!!!
 
Kuna ugomvi unaonyeshwa ITV wa mawakala. CHADEMA wanadai kunyimwa haki ya kukagua kitambulisho. Anadai wanataka wasikilize namba tu badala ya kukagua. Msimamizi wa Mawakala wa CHADEMA kawa mbogo sana. Anadai lazima wapate nafasi wakague. Mambo ya Sinza kwa Mugabe hayo.

Aisee babangu huyu ndugu ana lafudhi ya kichaga amechachamaa kweli kweli.

Kituo changu walipata nafasi ya kukagua na pia kusikia kwa sauti.

Bora hao waliomba ndio wakanyimwa. Huku Moro wa mekaa tu, wala hawahangaiki...
 
Big up superman, mie nipo kwa laptop nasubiri update zako maana sina namna ingine mkuu
 
Naona vituo vya Sinza watu wamejitokeza kwa wingi sana hasa wanawake.
 
nimeongea na askari mmoja amesema ni kweli WP amekamatwa na vitambulisho vitano, vya kupiga kura na sasa hivi yuko LUPANGO
 
Mgombea Ubunge kwa ticket yla CCM naye anaonekana akihakiki jina lake huko Sinza.
 
inatia moyo sana, nimetembelea baadhi ya maeneo ya Mbeya vijijini vijana wanafanya kweli.
 
nimeongea na askari mmoja amesema ni kweli WP amekamatwa na vitambulisho vitano, vya kupiga kura na sasa hivi yuko LUPANGO

Mpaka dakika hii kama kuna hila za namna yoyote, nyingi zimefichuliwa. Hakika kuna mwamko mkubwa sana. Kwa ujumla hali si mbaya sana. Tusubiri tu zoezi la kuhesabu kura lianze na majumuisho.
 
shein naye amepiga kura dar, shule ya msingi osterbay, badala ya zanzibar capital tv wameonyesha
 
Mbunge wa Ubungo Kupitia CCM akiwa katika harakati za kupiga Kura.

attachment.php

attachment.php
 
Attachments

  • DSC00044.jpg
    DSC00044.jpg
    33.7 KB · Views: 155
  • DSC00045.jpg
    DSC00045.jpg
    31.3 KB · Views: 154
superman thanx kwa updates keep it up!!!!!!!!
 
Star TV wanareport kuwa kulikuwa na hali ya tafrani huko Tarime lakini wana usalama wameituliza. Sasa hivi hali ni shwari.
 
nasikia tatizo kubwa watu wanachukua mda mrefu sana kwenye vyumba vya kupigia kura!!!!!!!!!hii nayo imekaaje?
 
shein naye amepiga kura dar, shule ya msingi osterbay, badala ya zanzibar capital tv wameonyesha

Du! Inakuwaje? Ina maana alijiandikisha Zanzibar au DSM? lakini 2005 si alipigia Pemba?
 
nasikia tatizo kubwa watu wanachukua mda mrefu sana kwenye vyumba vya kupigia kura!!!!!!!!!hii nayo imekaaje?

Ni kweli, mimi toka ilipofika zamu yangu baada ya kukaguliwa jina langu, ilinichukua takribani dakika 10 hadi 15 kukamilisha zoezi zima. Sijui sehemu zingine.
 
Back
Top Bottom