LIVE: JOHN HECHE ANAZUNGUMZA MUDA HUU MAKAO MAKUU YA CHADEMA

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
15 September 2026

Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani, yaliyofanyika leo Septemba 15

LIVE: JOHN HECHE ANAZUNGUMZA MUDA HUU MAKAO MAKUU YA CHADEMA​


View: https://m.youtube.com/watch?v=lFT4XNZsv50Hon. John W. Heche speaking at the World Democracy Day Celebrations, held today, September 15, 2026, at CHADEMA partyHeadquarters, Dar es Salaam Tanzania ...

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara John Heche akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani, yaliyofanyika leo Septemba 15, 2026, katika Makao Makuu ya CHADEMA, katika ukumbi wa

Edwin Mtei House, Mikocheni jijini Dar es Salaam.Tanzania

Mkutano huu unafanyika ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani. CHADEMA imetumia maadhimisho haya kuandaa kongamano maalum la kujadili mustakabali wa demokrasia nchini Tanzania pamoja na kushinikiza ajenda ya Katiba Mpya na kampeni ya #FreeLissu

Muktadha wa Mazungumzo ya Leo:
  • Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu: Hotuba ya John Heche inakuja saa chache baada ya kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania mtaa Kivukoni Front jijini Dar es Salaam ambapo toka asubuhi na mchana wa leo alikuwa kizimbani kama shahidi wa upande wa utetezi defense witness DW5. Heche amekuwa kizimbani kama shahidi wa tano wa utetezi DW5, ambapo leo amekabiliwa na maswali ya dodoso (cross-examination) kutoka kwa mawakili wa Serikali (Jamhuri) katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
  • Ajenda Kuu ya Kongamano: Kongamano hili la leo la siku ya Demokrasia Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 15 September Duniani kote linajikita katika kudai haki za kisiasa, kuimarisha misingi ya kidemokrasia, na kutoa mada mbalimbali kutoka kwa viongozi na wanaharakati wa chama hicho.
Matangazo haya ya LIVE yanarushwa kupitia chaneli mbalimbali za mtandaoni ikiwemo Millard Ayo YouTube pamoja na kurasa rasmi za kijamii za CHADEMA Digital.

N.B
VIONJO VYA MKUTANO SIKU YA DEMOKRASIA DUNIANI 15 SEPTEMBER

View: https://m.youtube.com/watch?v=F_PJ1mulRUM
 
heche anaweza kweli kumu-outshine Lema? Na alivyovurunda vile kizimbani?

huenda ana stress za kiwango cha juu mno heche 🐒
 
heche anaweza kweli kumu-outshine Lema? Na alivyovurunda vile kizimbani?

huenda ana stress za kiwango cha juu mno heche 🐒
Umekurupuka bila kusikiliza. Ajenda haikuwa lema hapo. Ni maadhimisho ya siku ya demokrasia, hutuba zimejikita kwenye hali ya demokrasia nchini pamoja katiba mpya.

Kumuoutshine lema ni ajenda ya Lumumba.
 
Heche ana kipajo kikubwa sana Cha kuhamasisha watu.
alihamasisha mpaka chadema wakashindwa kuchangia milioni 334 za tone tone.
ni kweli muungwana ana kipaji cha kuhamasisha,
aise dah 🐒
 
Umekurupuka bila kusikiliza. Ajenda haikuwa lema hapo. Ni maadhimisho ya siku ya demokrasia, hutuba zimejikita kwenye hali ya demokrasia nchini pamoja katiba mpya.

Kumuoutshine lema ni ajenda ya Lumumba.
kwamba mropokaji nae anaskizwa, right?🐒
 
Lema nae alisema leo atatoa taarifa ya press yake, vp alitoa?
 
 
heche anaweza kweli kumu-outshine Lema? Na alivyovurunda vile kizimbani?

huenda ana stress za kiwango cha juu mno heche 🐒
Mrembo wa ki Iraq unaendeleaje mama angu mzuri🌹 nikija dongobesh au bashay Fanya tuonane
 
CHADEMA tulindieni vijana kama akina Mahinyila kwa wivu mkubwa sana.

Tuendelee kuchangia chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…