Live Updates: UD Songo Vs Simba SC, CAF Championship

Live Updates: UD Songo Vs Simba SC, CAF Championship

Wamecheza vzr sana Songo ila FINISH yao ni mbovu.
Mkuu wale walikuwa nyumbani! Kumbuka mwaka jana TP mazembe alikula 3 bila pale Msumbiji.

Nawapa kongole simba kiukweli! Sidhani kama wakija taifa watatoka!! Labda iwe simba baridiiii na sio hii tunayoifaham ikiwa taifa
 
E
Mbona Wabrazil wote wameanzia nje! Tatizo ni nini hasa? Halafu Ajib yupo majeruhi? Au ndiyo amemfuata rafiki yake Tshabalala ili wasugue benchi?
Eti Mkude kacheza Ibrahim nje Mkude pass anawapa wapizani
 
Um
Leo simba wanacheza mpira wa kijinga sana huu.
Hapo midfield wamtoe Mkude au huyo Msudani wanapoteza mipira kijinga kijinga sana.
Umeona Mkude sio kiungo mzuri alikuwa analindwa na Koite
 
Ndio hasara ya kusajili wachezaji wengi,mpaka wazoeane! Since unajua hata kina Kagere,Boko wanaweza kuwa na fatiki!Unakumbuka Chama na Boko walkvoanza msimu uliopita?
 
Kwa away ni mwanzo mzuri si mbaya..IgaUfeThisIsNextLevel NguvuMoja
 
FT Songo 0- Simba 0
Simba imeonyesha mchezo hafifu
Mkuu kweli kabisa,, nlivoona kahata anaenda benchi nikaona sasa mambo magum zaidi! Boko nae sijui uchovu wa kenya? Hata nae nyoni bado ana uchovu,,

Mkuu ajibu habari zake zimekaaje?
 
Mkude alilna kashindwa kabisa kucheza akaanza kukanyaga tu wenzie!!! Ila n matakeo mazuri kwa simba!!
Hayo sio matokeo mazuri kwa Simba abadan.
Kwanini. Ili Simba apite anahitaji ushindi tu.
Lakini mpinzani wake anahitaji ushindi au sare ya magoli.
Simba angepata hata sare ya magoli kwake ndio ingekuwa faida.
 
Mkuu wale walikuwa nyumbani! Kumbuka mwaka jana TP mazembe alikula 3 bila pale Msumbiji.
Nawapa kongole simba kiukweli! Sidhani kama wakija taifa watatoka!! Labda iwe simba baridiiii na sio hii tunayoifaham ikiwa taifa
TP MAZEMBE kweli alioga 3-0 halafu kule Congo TP wakapindua kwa 4-0
 
Hayo sio matokeo mazuri kwa Simba abadan.
Kwanini. Ili Simba apite anahitaji ushindi tu.
Lakini mpinzani wake anahitaji ushindi au sare ya magoli.
Simba angepata hata sare ya magoli kwake ndio ingekuwa faida.
Vipi angelala 1-0 AU 2-0 Pale Songo?.. ndio game ya pili ingekuwa nyepesi dar?
Ndio maana hata Yanga nawaambia bora droo ya jana kuliko kupigwa halafu unaenda kutafuta ushindi ugenini.
Simba wenyeji utambeba labda abugi mwenyewe tu.
Yanga juhudi 'kazi kazi' ndio zitamsaidia.. Asiruhusu tena wamtangulie ugenini.
 
Back
Top Bottom