LNG Project: Njooni tujadili unadhani kwanini mradi wa gesi ya LNG unachelewa na nini chakufanya ili utekelezwe kwa wakati

Gesi miaka 10 na zaidi ule mtungi mkubwa ulikuwa unanunua tshs 65,000. Baadae ikashuka mpaka 45,000 sasa inapanda taratibu iko 55,000. Kuna namna yule aliyekuwa anauza 65000 anataka ifike huko. Tukiwa na gesi yetu itashuka sana tena waijazie ktk mitungi huko huko mtwara wasisafirishe na bomba ili kupunguza ulanguzi wa watu wa kati.
 
Tulitakiwa kuanza utekelezaji hata kabla ya Mozambique.
Tanzania lipo tatizo!
Tumeanza siku nyingi kubaini uwepo wa gesi na mafuta.
Tanzania tuna urasimu,
Wengine wameanza utekelezaji (Keñya,Uganda wanachimba mafuta)sisi bado hatuna mbinu za majadiliano na ufuatiliaji.
 
Tafakari huu ushauri mikataba ya ‘oil and gas’ ina maeneo sita ya majadiliano; technical and commercial (sehemu kubwa ya majadiliano zilipo na zinachukuwa muda mrefu). Sehemu zinazobaki ni maeneo ya environment, social, political na economic benefit (hapa ndio mambo yenu ya local content yalipo). As far as ‘oil and gas’ negotiations are concerned hayo maeneo ya pili kwenye hoja za Zitto na watanzania mnaopigia kelele faida za local contents kwa wawekezaji hiyo sio key area kwao.

Hayo maeneo sita yamajadiliano yanapelekea kuwa na clauses si chini ya 10 mpaka 12 za lazima kwenye mkataba, na zinaweza kuwa zaidi.

Bado faida (sehemu ya commercial negotiations) kwenye PSA ina fixed terms hizi zinatoka kwanza ambazo ni royalty na recovery costs (investment la deni la $42 billion). Kinachobaki mgawanyo wake ni variable hapo ndio kuna government share, contractors profit na tax watakazo lipa. Sasa ngoja kipindi cha low production kifike ndio utajua hujui ukiingia kichwa na investment kubwa kama hiyo ya $42 billion na bila ya kupekuwa kiasi gani ni mkopo na interests zake.

☝️Kwenye hayo mambo huu mjadala ata aujafika huko, so far ni general discussions tu.

Sasa wewe hujui hata hiyo $42 ni ya nini, kitu ambacho kila mtu humu anajua isipokuwa wewe. Kweli unataka tuelimishane kwenye haya mambo wakati hata common sense ya kuelewa hizo $42 billion huna.

Ukiona mada zipo juu ya uwezo sio vibaya ukabaki kuwa msomaji au ukiingia uende na mtindo wa kuuliza kuliko kuingia na ujuaji wakati hata abc la jambo husika huna nikikwambia ‘unitisation clause’ serikali aijakubali si ajabu hata ukaenda google na kurudi ujaelewa hiyo clause ina maswala gani.

👋
 
Kuongea ni rahisi hata ikiwa mbali sana na uhalisia.

Kufanya utafiti wa madini, gas na mafuta ni risk sana. Ilikuja kampuni ya Brazili kufanya utafiti wa mafuta nchini. Ilitumia dola milioni 760, na haikupata hata tone la mafuta. Ikaondoka, inaendelea na shughuli zake kama kawaida. Fikiria kama ingekuwa ni Serikali ya Tanzania imetumia pesa kiasi hicho, na imeambulia patupu.

Unapoondoka kwenda kufanya utafiti wa mafuta, gas au madini, chance yako ya kupata ni 0.1%. Iliyobakia 99.9% ni kupotea kwa pesa yako. Lakini katika leseni 10,000 za utafiti, ukabahatika kupata japo moja kuwa na matokeo mazuri, itafuta hasara ypte uliyoipata kwenye leseni 9,999. Ndiyo maana makampuni yanayofanya utafiti na uchimbaji mafuta na madini, kwa kiasi kikubwa ni yale tale Duniani kote. Wao wana miradi mingi inayozalisha ndiyo maana wana uwezo wa kuhimili hizo hasara.
 
Tuendelee kujadili jamani kama una ndugu yako yupo TPDC, EWURA, PUMA, ORYX, LAKE GAS, LAKE OIL, BUNGENI, WIZARANI, UDSM, UDOM, DIT, IFM, DUCE, CBE, CHUONI, mvute aje achangie hapa.
 
Exploration is expensive and high risk hakuna anaebisha hilo. Ila ukienda kupekuwa makampuni yanayochukua hizo risks the likes of ‘Tullow’ ni government sponsored, waliobaki ni conglomerates ambao wanashiriki kwenye value chain nzima (upstream, midstream and downstream) wapo ten, they can afford those risk its part of their business.

Kwa Tanzania karibu wote waliofanya exploration na kufanikiwa kupata vitalu ambavyo commercial, washauza (kwa waliopo shell, Exxon na Equinor) kupata faida zao na kusepa mengi yalikuwa government sponsored.

Mikataba ya exploration inatoa exclusive rights tu ya kuendeleza ukigundua gas ila aitoi uhalali wa nchi kuingia mikataba ya ovyo kwenye kuvuna.
 
Wewe unajua nini kuhusu hizo mega projects investment!? Hamna ulichoandika cha maana hapa kupinga hoja zake zaidi ya utopolo mtupu.
Sometimes watu kama hao I admire their confidence (ni watanzania tu tupo hivi), unakuta mtu hana ata abc ya jambo ila anapinga huyo balaa.
 
Tatizo litakuwa linatengenezwa na importer super dealer wa LNG!,hawa Hawawezi kuona na kukubali deal lao life hivi hivi mchana kweupe!
 
Unapichanganya siasa na Biashara Mambo kama haya huwa hayaepukiki.. LNG itaenda kuua Biashara za mafuta na wanasiasa wetu ndo wenye hizo biasha Kwa wingi, hujajiuliza kwanini sahivi vituo vya mafuta vimekuwa vingi kama uyoga?..
 
Unapichanganya siasa na Biashara Mambo kama haya huwa hayaepukiki.. LNG itaenda kuua Biashara za mafuta na wanasiasa wetu ndo wenye hizo biasha Kwa wingi, hujajiuliza kwanini sahivi vituo vya mafuta vimekuwa vingi kama uyoga?..
Labda utueleweshe wengine hiyo LNG ni nini hasa
 
Unapichanganya siasa na Biashara Mambo kama haya huwa hayaepukiki.. LNG itaenda kuua Biashara za mafuta na wanasiasa wetu ndo wenye hizo biasha Kwa wingi, hujajiuliza kwanini sahivi vituo vya mafuta vimekuwa vingi kama uyoga?..
Naomba kukuweka sawa ndugu mchangiaji, lengo la kuzalisha LNG ni ili tuisafirishe kwenda masoko ya nje. Kwa hiyo haiwezi kuua biashara ya mafuta inayotegemea soko la ndani.
 
Tunaomba kichwa kibadilishwe kianze na maneno mjadala wa kitaifa kuhusu mradi wetu wa LNG.
 
Karibuni siti za mbele wataalam kama unashindwa baadhi ya mambo jaribu hata kugoogle kuhusu LNG njoo changie mada hii nzuri.
 
Unaleta masimulizi badala ya kuleta kinachotakiwa kufanyika.Hopelee kabisa.Masimulizi hayabadili gas kuwa pesa Kwa Nchi.
 
Tueleze pia kuhusu huo mradi wa LNG inahusiana na nini ?
 
Hizi shudu zote hazihalalishi malalamiko yako, sababu mkataba haujasainiwa na hao wawekezaji wanalalama tupo slow Sana watavunja muungano wao wa kuwekeza gas ya Lindi,we tayari ushakuja na ujuaji wako Tanzania hatupati kitu, mkataba umeuona wapi!?..kana zitto kasema watanzania watanufaika na kuhudumia huo mradi,kakosea wapi mpaka umdhihaki!?..subiri mkataba usainiwe ndiyo ulie, unamaanisha wewe unajua kuliko wote walioko jikoni ku-negotiate!?..acha ujuaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…