LOGORIDDIM
JF-Expert Member
- Jan 25, 2013
- 1,638
- 1,237
Mimi Logoriddim (JF - expert member since 2013, nimefanikiwa kufika katika 3 bora ya shindano la kutafuta nembo ya brand ya MADE IN TANZANIA. Shindano hili limeandaliwa na TanTrade.
Shindano limefikia hatua ya kupigiwa kura ili kupata nembo bora zaidi. Kura inapigwa katika app ya Instagram search - Tantradetz (hapa haturuhusiwi kuweka links). Ni kitendo cha dakika 2 tu.
Kwa sababu JF imenilea na kunikuza katika tasnia ya ubunifu wa nembo, lakini pia kimsingi, nimejuana na mamia ya wateja kupitia platform hii.
Nawaombeni wateja wangu pamoja na umma kwa ujumla kunipigia kura katika shindano hili.
Kimsingi, ninatamani kabla ya uhai wangu kunitoka niwe nimeacha alama yenye mchango wa kimaendeleo ktk taifa langu pendwa Tanzania. Ingawa bado ninatamani uhai na kuzidi kumuomba Mola Muumba anijaalie umri mrefu ili nizidishe ufanyaji wa matendo mema.
Maelezo ya nembo yangu
1. Rangi za bendera = Utaifa na utambulisho wetu, values na umoja wetu.
2. Nyota = Nuru, ubora, ufaulu, ushindi, weledi, ubunifu (creativity) na uvumbuzi ( innovation). Space.
3. Mishale (Arrows) = "motion/movement", import na export na kusonga mbele (kufikia malengo)
4. Umbo mraba (square) katikati = Bidhaa na huduma (uwepo/upatikanaji wake).
5. Nembo ina ncha 8 = Dira (compass), dunia, uongozi bora (imaging captain in the ship), uelekeo sahihi na ugunduzi (imaging explorers navigation).
6. Umbo la mzunguko wa nembo pia linaashiria gear (manufacturing and production) na pia mzunguko/duara vinaashiria movement, process, mwendelezo wa mambo (masuala endelevu).
Aidha pia nyota ni ishara ya nguvu (power) na mafanikio. Ushahidi wa hili ni uwepo wa nyota katika bendera za mataifa yenye nguvu duniani kama Amerika, China na Urusi. Sijui hapa naweza kuitaja pia Korea kaskazini? maana bendera yake pia ina nyota.
Natanguliza shukran zangu na Mbarikiwe sana. Asanteni.