Lori lililobeba mafuta limepinduka katika eneo la Misugusu, Kibaha mkoani Pwani, ambapo kundi kubwa la wananchi wamejitokeza kuchota mafuta, ambayo yanamwagika, licha ya Askari kuwazuia lakini wameendelea kuchota mafuta hayo.
Your browser is not able to display this video.
=====
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema:
Chanzo cha ajali ni Lori kuacha njia na kuanguka maeneo ya Misugusugu, baada ya ajali hiyo Wananchi walijitokeza na kuanza kuchota mafuta jambo ambalo ni la hatari.
Tayari Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwadhibiti watu wote waliokuwa wamejitokeza kuchota mafuta, pia hakuna madhara yoyote kwa binadamu kwa maana ya Dereva, Wapita njia na watu wengine wote waliokuwa eneo la tukio.
Hata kama ningekuwa Mimi ningechota.mafuta Yako bei juu kuliko kipindi chochote toka Tanzania izaliwe.petroli Kwa Sasa 3257 halafu Kuna wapuuzi wanasema mama anafanya mambo mzuri.upuuzi kabisaa