Lori lililobeba mafuta limepinduka Kibaha, wananchi wachota mafuta bila woga

Sio roho mbaya zee ila hao wote Wana akili timamu ila wamekubali kurisk roho zao kwa malipo ambayo hayawezi kukupa hata pesa ya kula mwaka mmoja, watu kama hao ni bora watangulie akhera tubaki na wenye akili timamu
Ogopa umaskini. Ogopa kukosa hata 100 mfukoni.
Ogopa kuwa na familia yenye majukumu halafu mzee huna kitu ogopa sana.
 
Tukio la moto katika ajali kama hiyo liliwahi kumpa umaarufu Reinfred Masako, a. k. a Prof Bill Mazengo wa Juakali. Wengi walimfahamu baada ya kutangaza kwa mbwembwe jinsi watu walivyokuwa wanachota mafuta.... Mwenye bakuli haya.... Mwenye kidumu hayaaa.... mwenye ndoo hayaaa!
 
Ni umaskini au ujinga?

Watu hawajajifunza tu?
 
Rahisi sana kuwadhibiti bila kutumia nguvu, kijiti kimoja cha kibiriti wote wanaondoka.
Umasikini ni aghari.
 
Huu sio uamuzi wao bali wanalazzimishwa na umasikini uliowajaa ambao umesababishwa na serikali ya kipimbi ya CCM. Walaaniwe maCCM na vizazi vyao.
 
Nani wa kuchomoa betri? Hawa wanataka kuitukanisha serikali tu. Kwa ujinga wao.
 
Watu kama wapo kisimani vile ilihali kuna cheche za hatari asee
Kuna gari la mafuta liliwahi kuanguka Kisha watu Kama kawaida yao wakajichotea mafuta , Kisha mwenye busara zake akaona mafuta sio kitu akafuata betri kubwa za gari , kwenye kuchumoa terminal sasa jamaa akakoroga ikawa Kama kapiga kiberiti.....
 
Mungu awanusuru na Dhiki walizonazo. Inaonekana maisha yao yanakabiliwa na Moto wa Umasikini. Ambao hauna tofauti na Huo wa petroli sema speed ya kuunguza ndio zinayofauti.

Anaewashutumu Asemehewe Bure.
Yaani naomba yasitokee kama yale wakati ule likawapitia na mama ntilie waliokuwa wamekaa zao

Kuna watu walimeza ule mvuke walipowaka moto moto ulikuwa unatoka puani na mdomoni kama Dragon nilishangaa sana ila walikufa kwa maumivu makali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…