Low IQ Tanzania, wanafurahia Polisi kuondolewa barabarani!

Uongo, zipo nchi nyingi sana unatembea hata kiliometa 20 bila kukutana na Askari barabarani.
 
Kama ni kweli basi tatizo liko kwa watawala tuwaondoe wao chanzo cha matatizo badala ya kuacha trafic wasumbue watu na njaa njaa zao
 
Naunga mkono hoja wapunguzwe,mf ukiingia mkoa wa Pwani Barabara ya Morogoro,kila baada ya km 3 kuanzia Mlandizi to Mailimoja kuna kundi la Traffic Police,yani hadi kero...
 
Hizo speed radars utageuzwa mradi wa watu. Dawa ni kujenga njia kama ile ya Kimara- Kibaha tu!
Waweke na separator katikati kama walivyowekAga mapipa yale
 
Hizo speed radars utageuzwa mradi wa watu. Dawa ni kujenga njia kama ile ya Kimara- Kibaha tu!
Waweke na separator katikati kama walivyowekAga mapipa yale

Unatoa traffic wote ndo unaanza kujenga au unajenga kwanza afu unatoa traffic?
 
Hata mimi nimeshangaa misinterpretation ya Mr High IQ. Kinana hakusema kuwa polisi wote waondolewe barabarani ila wapunguzwe tu. Kwa kweli imekuwa toooooo much!

Inakuwaje safari ya kutoka Dar mpaka Morogoro inachukuwa masaa matano kwa kilomita 192?
Hili linafikirisha mno kipindi cha Late Benjamin W. Mkapa wakati njia ni hafifu watu walikuwa wanaenda within 2.5hrs hadi 3hrs at maximum mtu yuko Morogoro mjini.

Ila sikuhizi njia ni pana lami laini na safi ila watu wanatembea 5hrs na kiini cha tatizo ni hao hao askari.

Kimsingi mimi niko tayari kuendesha gari usiku kwenda safari yeyote ya mkoa kwa mkoa ila sio kero za kuombwa Rushwa kila saa.
 
Unatoa traffic wote ndo unaanza kujenga au unajenga kwanza afu unatoa traffic?
Mkuu niamini hao hao Trafic watazing'oa na kusingizia wezi kwani camera si waliwahi wekaga njia ya Morogoro road hio wahuni wakapita nazo.
 
Low IQ Boss Kijakazi dish leo limeyumba I guess temporarily! Hujamwelewa kabisa Kinana! Shida ni kuwa tuna utitiri wa trafiki kila mahali wanaodai rushwa na kuchelewesha kijinga jinga tu watu kwenda majobu!! full stop.

Mbona ajali zinaendelea na trafiki wapo?
Jamaa mmoja ulaya akiendesha gari mwendo kasi polisi walimkimbiza na hakusimama wakamzingira na wakachukua leseni yake huu sasa ni mwaka wa tano gari lake analo mwanae akitaka kutoka anamwita aje ampeleke town !

Mwarobaini wa ajali si kujaza trafik bali ni kutunga sheria mpya na adhabu kali zaidi za makosa ya barabarani mf kusababisha ajali ikaua mtu leseni ichukuliwe miaka mitano na kifungo miezi mitatu, magari mabovu yazuiliwe road, mwendokasi tochi faini 50,000 kosa la kwanza, mabasi kujaza abiria faini 100,000 mbona Samia atapiga pesa kama kwenye tozo tu!
 
Mob psychology ndio inazingua sana
 
Hata yeye mwenyewe, msafara wake usipoongozwa na askari, na wengine kufunga njia ili apite, hawezi kutoboa, kiongozi kama huyu ana walakini kwenye ishu ya uadilifu
 
Wahalifu hamjifichi
 
Ajali highwaY zitengwe wa kwenda na wa kurudi lanes zao tofauti. Uone kama ajali hazitapungua kwa 90%. Nature ya ajaĺi zeTU ni head on head collision.
Hapa kwetu kuna chawa kazi yao nikupotosha kutukana watu na kutetea serekali
 
Wewe high Q
 
Low IQ !!!
 
Kuweka kamera kila mahali ni gharama na hawawezi kumudu na ndiyo maana badala yake Polisi wanakaa barabarani, nchi nyingine hauoni Polisi kwa maana wana teknolojia lkn hata hizo nchi kabla ya kutajirika ziliweka polisi barabarani pia!
Teknolojia inaongezeka efficiency na kupunguza gharama wewe unaweka askari 6 kwa ajiri ya tochi moja?
 
Kwa nn utoe rushwa kama huna kosa??
 
Traffic wanahaha hivi sasamaji shingoni
Tuwekeze kwenye teknolojia siyo watu kuacha kulinda raia na mali zao
Teknolojia wataihujumu tu sababu wanataka wasimame wao wachukue buku buku zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…