Ushauri wa Kinana ni sahihi 100%. Hapo ni suala la wahusika kuitafuta njia nzuri kuhakikisha sheria na taratibu zinazingatiwa. Wanaweza hata kuboresha doria na kuweka mifumo mikubwa zaidi ya Kuchunguza , vilevile kuweka sheria Kali zaidi za makosa ya barabarani KAMA INAVYOFANYIKA NCHI ZA ULAYA.Hapo umenena. Nchi zetu hizi watu hatujastaarabika sana, kwa hiyo bado tunahitaji usimamizi wa karibu sana.
Sasa anatokea mlevi mmoja tu eti Police wamejazana mno Barabarani, watu wanashangilia.
Ni shida kweli kweli.
KUNA NCHI ULAYA UNACHANGANYIKIWA UNAPOKUTWA NA TRAFFIC OFFENCE.
Nchi nyingi huwezi kuta kila km 1 eti unasimamishwa, huwezi kuta utitiri wa traffic kama hapo Bongo.
Pia tatizo la Tz yaani ni watu wanaopinga na kukosoa kila Idea Mpya hata kama ina tija, yaani kuwaondoa kwenye maisha waliyoyazoea ni shida sana (rigidity).
Nakumbuka suala maoni ya kuanzishwa vyama vingi, asilimia kubwa walikataa, Katiba mpya wengi wanahoji yanini wakati ipo hii, kuwatoa Machinga barabarani watu wanaona sio sawa kabisa, sasa ushauri wa Kinana nao umeshatafsiria kuwa nongwa.
Timu ya Yanga ibadilishwe mfumo wa kiuendeshaji ikaonekana hapana kabisa eti watuache na timu yetu hii tumeanza nayo kabla hata ya vita vya pili vya dunia.