Lowassa na Chenge wameshawajibishwa huko Dodoma au bado? Ni kwa sababu gani aliamua KUTUFICHA mpaka leo hii sisi walipakodi?
Natafuta tempo ya U moderator nianze kudeal na watu kama wewe!
Mkuu ungweka kabisa hivi:
Lowassa, Sumaye wabwatuka CCM
- WALIA KUCHAFULIWA NA MAKADA WENZAO,NEC YARIDHIA GAMBA KUREJESHWA CC
Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma
Thursday, 24 November 2011
MAWAZIRI Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana walishambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo.
Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichomazika jana mjini Dodoma.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao.
Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,Lowassa alinukuliwa akihoji.
Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.
Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.
Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje? Sumaye alinukuliwa akihoji.
Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama watakuwa wamefanya hivyo.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba.
Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu.
Richmond yatajwa
Vyanzo vyetu vilimnukuu Lowassa akizungumzia suala la Kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond kwamba yeye aliamua kuvunja mkataba baina ya kampuni hiyo, lakini Rais KIkwete alimwambia subiri baada ya kuwa amepata ushauri wa Makatibu Wakuu.
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alinukuliwa akisema: Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?.
Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,alinukuliwa akihoji Lowassa.
Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo.
Lowassa alisema kama alivyozungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa walipokutana jijini Dar es Salaam, tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015.
Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,alinukuliwa Lowassa katika maelezo yake ndani ya NEC
Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo alidai kwamba siyo la kweli.
Baada ya Lowassa na Sumaye kuongoa, kada maarufu wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alisimama akitaka kuongelea dhana ya gamba ndipo Mkapa alipomshtua Kikwete kwamba hoja hiyo ifikie mwisho.
Baadhi ya wajumbe waliiambia Mwananchi kwamba wakati Lowassa akiongea Mkapa alionekana kufurahi.
Kujivua gamba
Kufuatia uamuzi huo wa NEC hivi sasa mpango wa kujivua gamba ulioasisiwa na chama hicho, Aprili mwaka huu unarejeshwa CC ambapo watuhumiwa wote wa makosa mbalimbali watafikishwa mbele ya Kamati za maadili na kuchukuliwa hatua kwa taratibu za chama hicho.
Mpango wa kujivua gamba ulilenga kuwashinikiza watuhumiwa wa ufisadi kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho na sasa unarejeshwa Kamati Kuu (CC) ili ichukue hatua zaidi kwa wale waliogoma kujiuzulu.
Hatua hiyo inatokana na kuwapo ukimya ambao unaashiria kutokuwapo viongozi na makada ambao wako tayari kujiuzulu nyadhifa zao kwa hiari yao kama ilivyotarajiwa.
Tangu kupitishwa kwa mpango huo maarufu kwa jina la kujivua gamba katika kikao cha NEC kilichopita cha Aprili mwaka huu, ni kada mmoja tu, Rostam Aziz aliyechukua hatua za kujiuzulu ubunge wa Jimbo la Igunga na ujumbe wa NEC, lakini wengine wamekuwa kimya hadi sasa.
Katika kikao cha Aprili NEC hiyo ya CCM ilipitisha maazimio 26, lakini kubwa ni lile lililokuwa likihimiza vita dhidi ya ufisadi kuendelea na kutoa mwito kwa watu wanaotajwa na jamii kuhusika na ufisadi ambao wako ndani ya chama kujitathmini kisha kuchukua hatua za kuachia madaraka waliyonayo.
Sehemu ya mwisho ya azimio hilo inasomeka: Wasipoachia madaraka chama kiwachukulie hatua mara moja.
Mmoja wa wajumbe wa CC ambaye ameomba jina lake kuhifadhiwa alisema: Tunawaomba NEC waturuhusu jambo hili tulifanyie kazi sisi (CC) na litafanyiwa kazi kupitia taratibu za kawaida za chama kwa kuzingatia kanuni na taratibu za maadili za chama hicho.
NEC yawakaanga kina Jairo
Katika hatua nyingine, NEC imeunga mkono hatua zilizopendekezwa na Bunge dhidi ya watumishi wa umma waliotajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoanika uozo wa matumizi mabaya ya fedha za Umma ndani ya Wizara ya Nishati na Madini.
Kamati hiyo katika ripoti yake iliyowasilishwa mwishoni mwa Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, iliwataja Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (aliyesimamishwa), David Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba wanastahili kuchukuliwa hatua.
Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, huku wabunge wakipendekeza pia kuondolewa madarakani kwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Adam Malima
Mkuu umetaka kunipa BAN bure umeshanihukumu kuwa mimi CCM, natumia masaburi nk ila kwanza umeshindwa kwa jina la aliye hai aka mungu...Lowassa mwizi tu anawaleeza nyie mlokuwepo chama na kumwona kwenda kanisani basi mnafikiri mtu mzuri sana..Kama yeye alikuwa mkweli kwa nini asiwahutubie Umma mzima wa Watanzania badala yake anaenda katika mikutano ya chama! anajua huko mmejaa masaburi watupu. Kikao cha chama CC wanatokea watu wanafokea wengine as if wao ni Miungu!..damn.
Yeye alikuwa waziri mkuu na sii katibu wa chama, hakuwahi kupendwa na Nyerere hadi leo hii wananchi hawampendi pengine huko kwenu CCM. Halafu naweza sema ni jambazi lililokubuhu yaani anatuondolea watu tu kila mwaka. Kesho sintoshangaa Nape mgonjwa anatakiwa kupelekwa India..
Kwani mkataba anaosema EL ni upi kama si wa DOWANS, ebu tujuze labda?Hivi wewe unasoma habari za kwenye nyuzi hii hii au kwingine? Ni wapi imetajwa Dowans hapo?
Acha kuchakachua mada. Hapa tunaongea mambo ya muhimu yenye mustakabali kwa taifa letu. Leo nataka hii siku tuongelee tu chama chetu tawala. Kile chama kingine hakitakiwi kuzungumziwa kabisa hapa JF. Mpaka 2015 watanzania tutakuwa na option moja tu ya chama cha mababu zetu!kwa mara ya kwanza leo nimeona umeandika zaid ya mistari mitatu...hahahahhaha
"Nguo ya kuazima haisitiri"Masaburi"Hivi hapo kuna habari ya kutishwa Kikwete? Tatizo lenu kubwa huwa mnasoma muandishi anavyotaka na si uhalisia wa yaliyojiri, mtu akiogea kwenye hadhara kama ile halafu mwandishi anukuu vipande atakavyo yeye na kuvijengea hoja, ujuwe huyo mwandishi anataka wewe uyashike yake na si yaliyojiri. Hapo mmepigwa changa la macho.
Sioni mahali ambapo Kikwete ametishwa au kuna cha kumtisha sasa hivi? Kama Ukuu ndio anao, hajatishika hiyo 1997 na akasema kama urais ni Mungu mwenyewe ndiye apangae atatishika leo hii? Unanchekesha.
Sioni la maana, sasa kama Kikwete alimwambia angoje ushauri wa Makatibu wakuu kuna kosa hapo?
Au ya 1997 Zanzibar yanahusu nini?
Hizi habari zimekaa kiudakuudaku hazina mshiko na zimekaa kifataani fataani, mtu aongee kuhusu Nape kwa dakika 7 halafu humu uweke maneno hayajai hata mstari mmoja? Hata angekuwa haongei anaya "spell" tu hayo maneno basi dakika 7 angejaza ukurasa.
Hizi habari ni za kifataani na hazina la maana hata moja, jamani hebu niambieni hapo kuna nini cha maana?
Tatizo lenu CCM wote mnalijua ..tatizo kuu ni kikwete huyu ndiye anakivuruga chama......hizi kashfa za kina Lowassa hizi leo ukimuuliza anaonekana hazijui na anawatetea wezi wenzie....cha maana sijakiona katka vikao vyenu hivyo....Acha kuchakachua mada. Hapa tunaongea mambo ya muhimu yenye mustakabali kwa taifa letu. Leo nataka hii siku tuongelee tu chama chetu tawala. Kile chama kingine hakitakiwi kuzungumziwa kabisa hapa JF. Mpaka 2015 watanzania tutakuwa na option moja tu ya chama cha mababu zetu!
Kweli jk hana ubavu kwa mamvi lakini hilo la mamvi kuwa rais wala haliji.
OK, alitaka kuvunja mkataba huo kama walivyokuja kufanya baadaye na matokeo tunadaiwa mabilioni. Lowasa anaweza kuueleza umma wa watanzania ni nani aliyewezesha Richmond kupewa mkataba huo aliotaka kuuvunja?
Leo asubuhi katika moja ya thread inayomhusu Lowasa, niliandika kwamba Lowasa ni shujaa na mfano wa kuigwa kwa wenye upembuzi yakinifu. Amejitahidi kuvumilia hadi leo na katika uvumilivu kama binadamu kuna kikomo.
Masuala ya uongozi wa serikali si jambo la mtu moja, ila mmoja ndiye mwenye kubeba lawama. Tatizo la Umeme lilikuwa la nchi nzima na sote tulikuwa na matarajio ya kampuni iliyopata dhamani kufua umeme ingetupunguzia matatizo ya giza badala yake ndo mambo yakaharibika zaidi.
Kwa vyo vyote Mkuu wa nchi anahusika moja kwa moja kwa vile ndiye kichwa cha nchi na ndiye mwajibikaji number one. Kwa vile kinga ya urais kwa mfumo wa nchi yetu inavyohusudiwa kama ufalme, mwandamizi wake katika masuala ya serikali ambaye ndiye waziri mkuu alibeba lawama.
Lowasa alitumia busara na uamuzi mgumu kujiuzuru uwaziri mkuu kwa kulinda heshima yake, serikali yake na chama chake kama alivyosema, lakini uamuzi wake umetafsiriwa vibaya na wabaya wake wamepata hoja ya kusimamia. Mzee Ruksa kipindi cha Nyerere akiwa waziri wa mambo ya ndani alipata msukosuko kama huo hadi kujiuzuru na kwa heshima yake hiyo alifaulu kutetea heshima yake hadi baadaye kuwa Rais wa nchi, na kumbuka Nyerere ndiye aliyempendekeza awe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Tanzania wakati aliboronga katika moja ya wizara aliyomkabidhi. Kuna wengi walioborongo kipindi cha Nyerere lakini katu hawakuinuka tena, hii ilitokana na namna kosa lilivyofanyika na mhusika alivyopokea na kutambua kosa lake.
Makosa mengi mabaya kuliko aliyofanya Lowasa katika utumishi wake yametokea na hakuna hata mmoja aliyewajibika au kuwajibishwa, na jinsi anavyonyooshewa vidole na akina Nape si uungawana kabisa, wakati hao wanaomnyooshea vidole kichama ni wahaini kwa kuanzisha CCJ ndani ya CCM wakati hawajajivua UCCM.
Leo Lowasa ameanza kufunua baadhi tu ya yaliyofichika, na kama wasingetuliza vichwa mengi angeyatapika. Na hakuna uthibitisho wa ufisadi wa Lowasa, ila ni tuhuma ambazo hazina uthibitisha na hata kama alikosea basi si ufisadi ila uwajibikaji katika utendaji wake, na alitambua hilo na kwa hiari kutokana na msongo toka bungeni aliamua kuachia ngapi ili wengine wajipange upya.
Matokea mtoto wa Mkulima hana uwezo kabisa wa kuchukua uamuzi mzito. Kwa sasa imethibitika kwamba bora lawama kuliko fedheha. Mtoto wa mkulima ni fedheha tupu ndani ya serikali kuliko lawama za Lowasa.
Duu ama kweli kamvisha gamba gumu mwanangu. Siamini haya maneno Lowasa ameyatapika. Kumbe Lowasa alikuwa amemfichia siri mwenzake lakini yakamfika aeona ngoja atue mzigo wa mtu mmoja ili wengi wafaidi.
Hata hivyo JK kupokea na kuzifanyia kazi simu za makatibu bila ya consultation ya aliyepewa dhamana hiyo ambaye ni Lowasa ilikuwa ni makosa JK aliyafanya. Kumbe JK alitakiwa awarudishe kwa Lowasa ili wasaidiane (Just imagining how things would be ethically/Utendaji) Nahao makatibu watakuwa wameshawishiwa na ROstam Aziz.
Ngoja tuone libeneke litakuaje.