Leo asubuhi katika moja ya thread inayomhusu Lowasa, niliandika kwamba Lowasa ni shujaa na mfano wa kuigwa kwa wenye upembuzi yakinifu. Amejitahidi kuvumilia hadi leo na katika uvumilivu kama binadamu kuna kikomo.
Masuala ya uongozi wa serikali si jambo la mtu moja, ila mmoja ndiye mwenye kubeba lawama. Tatizo la Umeme lilikuwa la nchi nzima na sote tulikuwa na matarajio ya kampuni iliyopata dhamani kufua umeme ingetupunguzia matatizo ya giza badala yake ndo mambo yakaharibika zaidi.
Kwa vyo vyote Mkuu wa nchi anahusika moja kwa moja kwa vile ndiye kichwa cha nchi na ndiye mwajibikaji number one. Kwa vile kinga ya urais kwa mfumo wa nchi yetu inavyohusudiwa kama ufalme, mwandamizi wake katika masuala ya serikali ambaye ndiye waziri mkuu alibeba lawama.
Lowasa alitumia busara na uamuzi mgumu kujiuzuru uwaziri mkuu kwa kulinda heshima yake, serikali yake na chama chake kama alivyosema, lakini uamuzi wake umetafsiriwa vibaya na wabaya wake wamepata hoja ya kusimamia. Mzee Ruksa kipindi cha Nyerere akiwa waziri wa mambo ya ndani alipata msukosuko kama huo hadi kujiuzuru na kwa heshima yake hiyo alifaulu kutetea heshima yake hadi baadaye kuwa Rais wa nchi, na kumbuka Nyerere ndiye aliyempendekeza awe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Tanzania wakati aliboronga katika moja ya wizara aliyomkabidhi. Kuna wengi walioborongo kipindi cha Nyerere lakini katu hawakuinuka tena, hii ilitokana na namna kosa lilivyofanyika na mhusika alivyopokea na kutambua kosa lake.
Makosa mengi mabaya kuliko aliyofanya Lowasa katika utumishi wake yametokea na hakuna hata mmoja aliyewajibika au kuwajibishwa, na jinsi anavyonyooshewa vidole na akina Nape si uungawana kabisa, wakati hao wanaomnyooshea vidole kichama ni wahaini kwa kuanzisha CCJ ndani ya CCM wakati hawajajivua UCCM.
Leo Lowasa ameanza kufunua baadhi tu ya yaliyofichika, na kama wasingetuliza vichwa mengi angeyatapika. Na hakuna uthibitisho wa ufisadi wa Lowasa, ila ni tuhuma ambazo hazina uthibitisha na hata kama alikosea basi si ufisadi ila uwajibikaji katika utendaji wake, na alitambua hilo na kwa hiari kutokana na msongo toka bungeni aliamua kuachia ngapi ili wengine wajipange upya.
Matokea mtoto wa Mkulima hana uwezo kabisa wa kuchukua uamuzi mzito. Kwa sasa imethibitika kwamba bora lawama kuliko fedheha. Mtoto wa mkulima ni fedheha tupu ndani ya serikali kuliko lawama za Lowasa.