Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa na Chenge wameshawajibishwa huko Dodoma au bado? Ni kwa sababu gani aliamua KUTUFICHA mpaka leo hii sisi walipakodi?

na hilo ndo kosa lao!
KAMA ANAIPENDA HII NCHI NA ANGEPENDA KUWA RAISI WA HII NCHI KWANINI AFICHE MAMBO MAKUBWA KAMA HAYO HAWA HAWAKO TAYALI KUFA KWA AJILI YA NCHI HII INAFAA NCHI IWAUWE TUU!
 
Mkuu ungweka kabisa hivi:

Lowassa, Sumaye wabwatuka CCM

  • WALIA KUCHAFULIWA NA MAKADA WENZAO,NEC YARIDHIA GAMBA KUREJESHWA CC

Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma
Thursday, 24 November 2011


salamu-lc.jpg


MAWAZIRI Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana walishambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo.

Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichomazika jana mjini Dodoma.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao.

“Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,”Lowassa alinukuliwa akihoji.

Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.

Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.

“Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje?” Sumaye alinukuliwa akihoji.

Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama watakuwa wamefanya hivyo.

Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba.

Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: “Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu”.

Richmond yatajwa
Vyanzo vyetu vilimnukuu Lowassa akizungumzia suala la Kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond kwamba yeye aliamua kuvunja mkataba baina ya kampuni hiyo, lakini Rais KIkwete alimwambia subiri baada ya kuwa amepata ushauri wa Makatibu Wakuu.

Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM),
alinukuliwa akisema: “Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”.

“
Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”alinukuliwa akihoji Lowassa.

Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: “
Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo”.

Lowassa alisema kama alivyozungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa walipokutana jijini Dar es Salaam, tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015.

“Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,”alinukuliwa Lowassa katika maelezo yake ndani ya NEC

Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo alidai kwamba siyo la kweli.

Baada ya Lowassa na Sumaye kuongoa, kada maarufu wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alisimama akitaka kuongelea dhana ya gamba ndipo Mkapa alipomshtua Kikwete kwamba hoja hiyo ifikie mwisho.

Baadhi ya wajumbe waliiambia Mwananchi kwamba wakati Lowassa akiongea Mkapa alionekana kufurahi.

Kujivua gamba
Kufuatia uamuzi huo wa NEC hivi sasa mpango wa kujivua gamba ulioasisiwa na chama hicho, Aprili mwaka huu unarejeshwa CC ambapo watuhumiwa wote wa makosa mbalimbali watafikishwa mbele ya Kamati za maadili na kuchukuliwa hatua kwa taratibu za chama hicho.

Mpango wa kujivua gamba ulilenga kuwashinikiza watuhumiwa wa ufisadi kuachia nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho na sasa unarejeshwa Kamati Kuu (CC) ili ichukue hatua zaidi kwa wale waliogoma kujiuzulu.

Hatua hiyo inatokana na kuwapo ukimya ambao unaashiria kutokuwapo viongozi na makada ambao wako tayari kujiuzulu nyadhifa zao kwa hiari yao kama ilivyotarajiwa.

Tangu kupitishwa kwa mpango huo maarufu kwa jina la kujivua gamba katika kikao cha NEC kilichopita cha Aprili mwaka huu, ni kada mmoja tu, Rostam Aziz aliyechukua hatua za kujiuzulu ubunge wa Jimbo la Igunga na ujumbe wa NEC, lakini wengine wamekuwa kimya hadi sasa.

Katika kikao cha Aprili NEC hiyo ya CCM ilipitisha maazimio 26, lakini kubwa ni lile lililokuwa likihimiza vita dhidi ya ufisadi kuendelea na kutoa mwito kwa watu wanaotajwa na jamii kuhusika na ufisadi ambao wako ndani ya chama kujitathmini kisha kuchukua hatua za kuachia madaraka waliyonayo.

Sehemu ya mwisho ya azimio hilo inasomeka: “Wasipoachia madaraka chama kiwachukulie hatua mara moja”.

Mmoja wa wajumbe wa CC ambaye ameomba jina lake kuhifadhiwa alisema: “Tunawaomba NEC waturuhusu jambo hili tulifanyie kazi sisi (CC) na litafanyiwa kazi kupitia taratibu za kawaida za chama kwa kuzingatia kanuni na taratibu za maadili za chama hicho”.

NEC yawakaanga kina Jairo
Katika hatua nyingine, NEC imeunga mkono hatua zilizopendekezwa na Bunge dhidi ya watumishi wa umma waliotajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyoanika uozo wa matumizi mabaya ya fedha za Umma ndani ya Wizara ya Nishati na Madini.

Kamati hiyo katika ripoti yake iliyowasilishwa mwishoni mwa Mkutano wa Tano wa Bunge uliomalizika wiki iliyopita mjini Dodoma, iliwataja Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini (aliyesimamishwa), David Jairo na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kwamba wanastahili kuchukuliwa hatua.

Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovick Utouh, huku wabunge wakipendekeza pia kuondolewa madarakani kwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Adam Malima

Huyu (ENL) alijipanga kujisafisha na bila Mkapa kumnongoneza Mwenyekiti hili swala la Gamba linge leta mwendelezo mkubwa kwenye kikao..kilicho baki kwa EL ni kuhakikisha njia ya kuingia IKULU ni nyeupe ndo maana anarudisha mambo ya 1997 na sasa yanamlenga mwenyekiti.Kwa garama yoyote huyu anaitaka IKULU na mtu wa namna hii mwogope kama ukoma achilia mbali huo ufisadi anaotuhumiwa nao.
 
Lowassa mwizi tu anawaleeza nyie mlokuwepo chama na kumwona kwenda kanisani basi mnafikiri mtu mzuri sana..Kama yeye alikuwa mkweli kwa nini asiwahutubie Umma mzima wa Watanzania badala yake anaenda katika mikutano ya chama! anajua huko mmejaa masaburi watupu. Kikao cha chama CC wanatokea watu wanafokea wengine as if wao ni Miungu!..damn.

Yeye alikuwa waziri mkuu na sii katibu wa chama, hakuwahi kupendwa na Nyerere hadi leo hii wananchi hawampendi pengine huko kwenu CCM. Halafu naweza sema ni jambazi lililokubuhu yaani anatuondolea watu tu kila mwaka. Kesho sintoshangaa Nape mgonjwa anatakiwa kupelekwa India..
Mkuu umetaka kunipa BAN bure umeshanihukumu kuwa mimi CCM, natumia masaburi nk ila kwanza umeshindwa kwa jina la aliye hai aka mungu...

Pili nakanusha mimi sio CCM bali ni mtaji tarajiwa wa chama cha mgombea binafsi in future ccm naichukia mpaka najikuta nawachukia na watu wake wote mpaka jirani yangu kisa ni ccm, chadema nakipenda sana kwa sera na utekelezaji wake bali sio msimamo kwani Dr..Slaa ni Mtumishi wa mungu na msomi atachukuwa muda mrefu kuikomboa nchii hii kwani ukombozi wa nchi hii unatakiwa ufanywe na mtu ambaye ni jihad kweli kweli maana hakuna democrasia hivo panahitajika nguvu ya ziada ambayo ni uma na yeye Dr slaa anaogopa lawama na kadhia endapo jaribio likifanikiwa au kutokufanikiwa na kwa sababu ana nia ya dhati ya kurudisha madaraka kwa wananchi kikatiba basi anaogopa asije akahukumiwa na katiba hio hio kwa kusababisha au amasisha maandamano ambayo yatakayo sababisha watu kupoteza maisha..

Mfano mzuri Arusha walikufa watu watatu kama sikosei ndani ya maandamano ya masaa chini ya sita je Tanzania nzima unadhani wakiandamana watakufa watu wangapi ndani ya hayo masaa sita? Ikumbukwe maandamano yenyewe hayatakuwa na kikomo je kwa elimu ndogo ya akina mura afwande nanii wataua wangapi? Je wale watakao kufa kwa sababu nyingine ni wangapi? Dr anapata wakati mgumu anapowaza hayo mambo na alivyojengeka kiimani tena ndio anajikuta akionea huruma roho za watanzania..

Back to Mtu kama Lowassa, Lowassa kama angekuwa ndio dr slaa kishaeleweka siku nyingi maana huyu jamaa ana msimamo sana tena zaidi ya sana jiulize alipata wapi ujasiri wa kujiuzulu uwaziri mkuu? ni mfano wa kuigwa, japokuwa anaiba lakini anapiga kazi sana huyu jamaa, mmelia na akina ngeleja, abasi na wengine mbona ni watu wadogo sana ukilinganisha na waziri mkuu na wamegoma kujiuzulu?? unadhani ni kwa nini aliamua kukaa kimya muda wote huo bila kuliongelea hilo? na kwa sisi tunavoelewa huyu jamaa ndio Tanzania na siku akiamua kufunguka ndio tutajua zaidi ila mimi naona bora huyu kuliko jk..

Kwa hiyo ntake radhi bana mimi sio CCM.
 
kwa mara ya kwanza leo nimeona umeandika zaid ya mistari mitatu...hahahahhaha
Acha kuchakachua mada. Hapa tunaongea mambo ya muhimu yenye mustakabali kwa taifa letu. Leo nataka hii siku tuongelee tu chama chetu tawala. Kile chama kingine hakitakiwi kuzungumziwa kabisa hapa JF. Mpaka 2015 watanzania tutakuwa na option moja tu ya chama cha mababu zetu!
 
Hivi hapo kuna habari ya kutishwa Kikwete? Tatizo lenu kubwa huwa mnasoma muandishi anavyotaka na si uhalisia wa yaliyojiri, mtu akiogea kwenye hadhara kama ile halafu mwandishi anukuu vipande atakavyo yeye na kuvijengea hoja, ujuwe huyo mwandishi anataka wewe uyashike yake na si yaliyojiri. Hapo mmepigwa changa la macho.

Sioni mahali ambapo Kikwete ametishwa au kuna cha kumtisha sasa hivi? Kama Ukuu ndio anao, hajatishika hiyo 1997 na akasema kama urais ni Mungu mwenyewe ndiye apangae atatishika leo hii? Unanchekesha.
"Nguo ya kuazima haisitiri"Masaburi"

Nimekuwa nikifuatilia mara nyingi hoja zako na leo hii nimethibitisha kuwa wewe ni"MNAFIKI"
 
Dah Mwalimu, ufufuke uone wezi na majambazi wanavyotamba ndani ya vikao nyeti vya chama ulichokiasisi. Kwa kuwa wote walioko mle hakuna wa kumnyooshea mwenzake kidole. WATANZANIA nao tunatazama mambo haya kama sinema ya kawaida huku nchi inabaki mifupa. Tunaandamana kwa ajili ya Meya wa Arusha tu.
 
Kweli jk hana ubavu kwa mamvi lakini hilo la mamvi kuwa rais wala haliji.
 
Sioni la maana, sasa kama Kikwete alimwambia angoje ushauri wa Makatibu wakuu kuna kosa hapo?

Au ya 1997 Zanzibar yanahusu nini?

Hizi habari zimekaa kiudakuudaku hazina mshiko na zimekaa kifataani fataani, mtu aongee kuhusu Nape kwa dakika 7 halafu humu uweke maneno hayajai hata mstari mmoja? Hata angekuwa haongei anaya "spell" tu hayo maneno basi dakika 7 angejaza ukurasa.

Hizi habari ni za kifataani na hazina la maana hata moja, jamani hebu niambieni hapo kuna nini cha maana?

FaizaFoxy; naamini Thread hii haijakaa vizuri masikioni mwacho. Huu ndiyo ukweli wa mambo from a reliable source. Haya ndiyo matunda ya siasa za kibongo zisizo na mashiko; unaweza kutumwa na boss wako uwe puppet-master ktk issue
Fulani, lakini upepo ukibadirika basi usishangae ukawa scape-goat.
Hizo ndo siasa zenu, sasa unashangaa nini !
 
Acha kuchakachua mada. Hapa tunaongea mambo ya muhimu yenye mustakabali kwa taifa letu. Leo nataka hii siku tuongelee tu chama chetu tawala. Kile chama kingine hakitakiwi kuzungumziwa kabisa hapa JF. Mpaka 2015 watanzania tutakuwa na option moja tu ya chama cha mababu zetu!
Tatizo lenu CCM wote mnalijua ..tatizo kuu ni kikwete huyu ndiye anakivuruga chama......hizi kashfa za kina Lowassa hizi leo ukimuuliza anaonekana hazijui na anawatetea wezi wenzie....cha maana sijakiona katka vikao vyenu hivyo....
 
Gazeti hilihili liliwahi kutuaminisha kuwa CC ni pro Sitta, ila kikao cha maamuzi NEC ni pro Lowassa.

Sasa kama issue ya gamba imerudishwa CC kwa maamuzi, maana yake ni nini?...

Au kwa vile iko dhahiri sasa kuwa Mwenyekiti mwenyewe ni pro Lowassa, kwa hiyo hoja ndio imekufa?
 
OK, alitaka kuvunja mkataba huo kama walivyokuja kufanya baadaye na matokeo tunadaiwa mabilioni. Lowasa anaweza kuueleza umma wa watanzania ni nani aliyewezesha Richmond kupewa mkataba huo aliotaka kuuvunja?

Ajabu ya wadanganyika hawajiulizi hili swali muhimu sana.

Wao kila siku ni kudandia treni kwa mbele, halafu wakishapondeka ndo wanaanza kulalamika.

Golden question: NI NANI ALIWEZESHA/ALISHINIKIZA RICHMOND IPEWE MKATABA WAKATI HAIKUA NA FEDHA, VIFAA, WALA UZOEFU WA KUFUA UMEME?

Tunaomba LOWASSA amwage kila kitu hadharani kama kweli anataka kujisafisha, la sivyo bado GAMBA limemng'ang'ania machoni kwa watanzania.
 
Kama ni kujiuzulu Lowasa alitakiwa kufanya hivo wakati JK amemkatalia kuvunja mkataba wa Richmond mapema kwa kuwa alishajua ulikuwa wa kitapeli na wizi mtupu. Hakufanya hivo.
 
There are currently 698 users browsing this thread. (140 members and 558 guests)

Bado naendelea kufuatilia filamu ya Magamba naona karibu inamalizika au hamjui mwisho wa picha Steering lazima ashinde !!1.
 
Hizi habari za kujivua gamba zinanichefua mno kwa sababu naona kabisa ni usanii.
 
Leo asubuhi katika moja ya thread inayomhusu Lowasa, niliandika kwamba Lowasa ni shujaa na mfano wa kuigwa kwa wenye upembuzi yakinifu. Amejitahidi kuvumilia hadi leo na katika uvumilivu kama binadamu kuna kikomo.

Masuala ya uongozi wa serikali si jambo la mtu moja, ila mmoja ndiye mwenye kubeba lawama. Tatizo la Umeme lilikuwa la nchi nzima na sote tulikuwa na matarajio ya kampuni iliyopata dhamani kufua umeme ingetupunguzia matatizo ya giza badala yake ndo mambo yakaharibika zaidi.

Kwa vyo vyote Mkuu wa nchi anahusika moja kwa moja kwa vile ndiye kichwa cha nchi na ndiye mwajibikaji number one. Kwa vile kinga ya urais kwa mfumo wa nchi yetu inavyohusudiwa kama ufalme, mwandamizi wake katika masuala ya serikali ambaye ndiye waziri mkuu alibeba lawama.

Lowasa alitumia busara na uamuzi mgumu kujiuzuru uwaziri mkuu kwa kulinda heshima yake, serikali yake na chama chake kama alivyosema, lakini uamuzi wake umetafsiriwa vibaya na wabaya wake wamepata hoja ya kusimamia.
Mzee Ruksa kipindi cha Nyerere akiwa waziri wa mambo ya ndani alipata msukosuko kama huo hadi kujiuzuru na kwa heshima yake hiyo alifaulu kutetea heshima yake hadi baadaye kuwa Rais wa nchi, na kumbuka Nyerere ndiye aliyempendekeza awe Mgombea Urais wa Jamhuri ya Tanzania wakati aliboronga katika moja ya wizara aliyomkabidhi. Kuna wengi walioborongo kipindi cha Nyerere lakini katu hawakuinuka tena, hii ilitokana na namna kosa lilivyofanyika na mhusika alivyopokea na kutambua kosa lake.

Makosa mengi mabaya kuliko aliyofanya Lowasa katika utumishi wake yametokea na hakuna hata mmoja aliyewajibika au kuwajibishwa, na jinsi anavyonyooshewa vidole na akina Nape si uungawana kabisa, wakati hao wanaomnyooshea vidole kichama ni wahaini kwa kuanzisha CCJ ndani ya CCM wakati hawajajivua UCCM.

Leo Lowasa ameanza kufunua baadhi tu ya yaliyofichika, na kama wasingetuliza vichwa mengi angeyatapika. Na hakuna uthibitisho wa ufisadi wa Lowasa, ila ni tuhuma ambazo hazina uthibitisha na hata kama alikosea basi si ufisadi ila uwajibikaji katika utendaji wake, na alitambua hilo na kwa hiari kutokana na msongo toka bungeni aliamua kuachia ngapi ili wengine wajipange upya.

Matokea mtoto wa Mkulima hana uwezo kabisa wa kuchukua uamuzi mzito. Kwa sasa imethibitika kwamba
bora lawama kuliko fedheha. Mtoto wa mkulima ni fedheha tupu ndani ya serikali kuliko lawama za Lowasa.

Muheshimiwa hapo kwenye RED mimi nakukatalia 100% siyo kweli kuwa Mzee ruksa alikuwa chaguo la Mwalimu la hasha...Kulikuwa na zengwe kubwa ndani yake...lakini kulikuwa hakuna jinsi ni lazima ionekane kuwa pendekezo la kwanza ni mzee ruksa....

Chaguo la mwalimu wakati ule alikuwa Waziri mkuu wa wakati ule Salim Ahmed Salimu..Lakini kwa busara zao waliona isingependeza kumpendekeza mgombea wa kwanza awe waziri mkuu badala ya makamo wa raisi na raisi wa Zanzibar kwa wakati ule amabaye alikuwa Mzee ruksa....ndipo alipoitwa mzee ruksa na kuombwa akubaili hilo ombi ...lakini akaambiwa wakati wa mkutano mkuu wa CCM pale Chimwaga atakapo tangazwa kuwa yeye ndio Mgombea uraisi ajaye......baadae yeye ashukuru kwa kumpendekeza lakini atoe udhuru kuwa nafasi hii yeye ahiwezi ni kubwa sana kwake....

Naye mzee Ruksa akapata washauri wakamwambia mzee usiwe mjinga wewe lini tena utakuja kuwa raisi...ndipo yeye alipo simama baada ya kutangazwa kuwa ndio mgombea..badala ya kutoa udhuru yeye alikubali moja kwa moja.....na ndio hapo ilipochipuka uhasama wa chini chini kati ya Mzee ruksa na Mwl...na migongano ya hapa na pale...mwanzoni wa utawala wa mzee ruksa...sasa wewe unatumabia Mzee ruksa alikuwa chaguo la mwalimu hii sio kweli...kama unampigia chapuo Mr Lowasa mpigie tuu lakini sio kwa kisingizio hiki
 
Duu ama kweli kamvisha gamba gumu mwanangu. Siamini haya maneno Lowasa ameyatapika. Kumbe Lowasa alikuwa amemfichia siri mwenzake lakini yakamfika aeona ngoja atue mzigo wa mtu mmoja ili wengi wafaidi.

Hata hivyo JK kupokea na kuzifanyia kazi simu za makatibu bila ya consultation ya aliyepewa dhamana hiyo ambaye ni Lowasa ilikuwa ni makosa JK aliyafanya. Kumbe JK alitakiwa awarudishe kwa Lowasa ili wasaidiane (Just imagining how things would be ethically/Utendaji) Nahao makatibu watakuwa wameshawishiwa na ROstam Aziz.

Ngoja tuone libeneke litakuaje.

Makatibu (Luhanjo) + JK = Jairo... Ohhh sorry, should be Richmond and Jairo behind,
 
Back
Top Bottom