Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa aikana Richmond, asema alijiuzulu kwa heshima ya serikali na chama chake!

Lowassa said:
"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa na kuitwa fisadi kwanini?".

"
Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?


Redbold


Katika hotuba yake ya mwisho kama waziri mkuu Bungeni Mh. Lowassa alisema hivi na mnukuu "
Mheshimiwa Spika, lakini nimetafakari kwa makini sana jambo hili nikajiuliza hivi kulikoni mpaka watu wazima wenye uwezo wao, watu maarufu wenye heshima zao, mpaka wafike mahali waache jambo la msingi kama hilo kulikoni? Mimi nadhani there is a wish which I am going to grant, ni Uwaziri Mkuu. Nadhani tatizo ni Uwaziri Mkuu. Kwamba ionekane Waziri Mkuu ndio amefanya haya, tumuondolee heshima au tumwajibishe.

Mheshimiwa Spika,
nimetafakari kwa niaba ya chama changu, kwa niaba ya Serikali yangu nimeamua kumwandikia Rais barua ya kumwomba niachie ngazi. Nafanya hivyo kwa moyo mweupe kabisa ili kuonyesha dhana ya uwajibikaji lakini kutokubaliana na utaratibu uliotumika kusema uongo ndani ya Bunge wa kumsingizia mtu.

Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kumshukuru sana Rais kwa heshima aliyonipa ya kutumikia nchi hii kwa Uwaziri Mkuu kwa miaka miwili.


Namshukuru sana Mheshimiwa Rais.
mwisho wa kunukuu.

1. Mh.Lowassa naye alilidanganya bunge kwa kusema kuwa alifikiria tuhuma dhidi yake ni uwaziri mkuu wakati anajua kabisa hilo haikuwa sababu ya kutuhumiwa hivyo.

2. Kama alijiuzulu kwa kulinda heshima ya chama(Mwenyekiti wake) na serikali yake(Rais); huku akijua kitendo hicho kilikuwa kinatoa fursa ya kuficha uovu(ufisadi), haoni kuwa hakututendea haki watanzania tupendao utawala bora na wala hatupendi kabisa utawala balaa?
 
Ukumbi wa mikutano wa White House uliopo Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini hapa, jana ulizizima kiasi cha baadhi ya wajumbe kutokwa machozi, wakati Edward Lowassa aliposimama kwa mara ya kwanza na kujibu tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazomkabili.

Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli, alikuwa mtu wa kwanza kusimama na kuchangia ajenda ya kujivua gamba iliyosomwa katika kikao hicho na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa.

Kabla ya Lowassa kusimama na kuanza kutoa utetezi wake, Msekwa aliwaeleza wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwamba, Kamati Kuu ya chama hicho ilikuwa imependekeza kurejeshwa kwa suala hilo katika Kamati ya Maadili. Katika maelezo yake Msekwa alisema, uamuzi wa kulirejesha suala hilo katika kamati ya maadili linafanyika baada ya watuhumiwa wawili, Lowassa na Andrew Chenge kutotekeleza maazimio ya kikao cha NEC kilichowataka wapime wenyewe vinginevyo chama kingechukua hatua dhidi yao.

Akizungumza akiwa mtulivu, Lowassa alianza kwa kuunga mkono uamuzi huo wa suala lao kupelekwa katika Kamati ya Maadili akieleza huo ndiyo utamaduni wa CCM anaoufahamu vyema tangu alipojiunga na chama hicho miaka ya mwanzo ya 1975 baada kumaliza elimu yake ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Katika hilo, pasipo kuwataja Lowassa alieleza kushangazwa na viongozi wa juu wa chama hicho kukaa kimya pasipo kuchukua hatua zozote wakati wote Nape na Chiligati walipokuwa wakipita na kumshambulia kwa tuhuma zisizo na ukweli wala ushahidi.

Akimuelekezea hoja zake Rais Kikwete, mbunge huyo wa Monduli Lowassa alisema viongozi hao wamekuwa wakimhusisha na tuhuma za ufisadi kupitia mkataba wa Richmond wakati rais akijua kwamba hakuna jambo alilofanya ambalo yeye Kikwete hakulifahamu au ambalo hakumtuma yeye.

Lowassa ambaye katika utetezi wake alikuwa ameshika mkononi hansard ya Bunge alisema, Ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ambayo ilisababisha ajiuzulu uwaziri mkuu, Februari mwaka 2008 ilisema bayana kwamba alifikia hatua hiyo kutokana na makosa ya watendaji wa chini yake. Mbali ya hilo, Lowassa alirejea kauli za Kikwete mwenyewe ndani ya vikao vilivyopita vya NEC ambako alipata kukaririwa zaidi ya mara moja akisema kulikuwa hakuna ushahidi wa rushwa katika Richmond.

Kama hiyo haitoshi, aligusia pia matamshi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ndani ya Bunge ambayo yalithibitisha kutokuwapo kwa rushwa katika mchakato ulioipa zabuni kampuni ya Richmond hata kufikia hatua za kutowaadhibu hata wale ambao majina yao yalitajwa moja kwa moja kwenye ripoti ya Kamati Teule ya Bunge. Baada ya kulijadili hilo, Lowassa alikumbusha historia ya neno ‘ufisadi' akisema lililetwa na CHADEMA kupitia mkutano wa Mwembeyanga na kuwataja viongozi 11 wa CCM akiwamo yeye kwa ufisadi.

Mwanasiasa huyo alisema, katika tamko hilo la CHADEMA, alijumuishwa katika orodha ya mafisadi akihusishwa na uamuzi wake wa kuuvunja mkataba wa City Water ambao hata hivyo baadaye serikali ilishinda kesi katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa mizozo ya uwekezaji. Alisema ni jambo la ajabu kwamba viongozi wa CCM walilidaka neno hilo na kuanza kulitumia kuwashambulia wenzao akiwamo yeye katika mambo ambayo hayakuwa na ukweli.

Alipofika hatua hiyo alihoji, Nape anapata wapi ‘moral authority' (uhalali wa kimaadili) wa kumtuhumu yeye kwa ufisadi hata kudai kwamba amekipotezea heshima chama hicho wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Akifafanua, alisema matokeo ya kura alizopata Rais na yeye mwenyewe katika jimbo la Monduli unazidi asilimia 89 na kwamba wakati yeye (Lowassa) na wengine wakipambana kukijenga na kukipigania chama chao kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, Nape na wanasiasa wengine wanaomshambulia walikuwa katika harakati za kusajili Chama cha Jamii (CCJ).

Akirejea tuhuma dhidi yake ambazo hazina ushahidi huku akitumia neno la Kiingereza, ‘perception' Lowassa alimkumbusha Kikwete jinsi yeye (Kikwete) alivyozushiwa tuhuma za ukosefu wa maadili na mwanasiasa mkongwe Paul Sozigwa mwaka 2003. Lowassa alisema katika tuhuma hizo dhidi ya Kikwete ambazo ziliwasilishwa mbele ya kikao na Sozingwa kwa niaba ya Kamati ya Maadili, zilizimwa kwa hekima ya mwenyekiti wa CCM wakati huo Rais mstaafu Benjamin Mkapa.

"Mheshimiwa Mwenyekiti naamini kama si hekima za mzee wetu Mkapa wakati ule, leo hii usingekuwa umekaa katika kiti hicho," alisema Lowassa ambaye alisisitiza ni makosa kuwahukumu watu pasipo ushahidi. Alisema kama kungekuwa na makosa aliyotenda, kanuni za CCM ziko wazi na zingefuatwa ikiwa ni pamoja na kuitwa katika kamati ya maadili ambako angehojiwa juu ya tuhuma hizo.

"CCM ninayoifahamu ni ile inayotenda haki na hakiwezi kumtuhumu mtu hadharani bila ushahidi kama walivyofanya Chiligati na Nape na kwa mujibu wa kanuni ni vibaya kumtuhumu bila vikao vya maadili ya chama," alisema.

Fredrick Sumaye amuunga mkono
Akichangia mjadala huo ambao hasa ulihusu uamuzi wa kurejesha hoja ya dhana ya kujivua gamba na tuhuma za ufisadi kwa kamati ya maadili, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye aliungana na Lowassa kuhoji busara ya kuitwa na kuhojiwa wakati tuhuma zimeishasambazwa nchi nzima. Sumaye alisema halikuwa jambo la busara kuwatuhumu watu na kutangaza tuhuma dhidi yao kabla ya kuthibitishwa kwa tuhuma zenyewe.

Alikwenda mbali zaidi na kuhoji iwapo kamati ya maadili itabaini kuwa Lowassa hakuwa na hatia, hatua gani zitachukuliwa dhidi ya Chiligati na Nape waliosambaza tuhuma hizo wakati viongozi wa juu akiwamo mwenyekiti wakiwa kimya? "Kama mtu ametuhumiwa kwa stahili hii nchi nzima, alafu uchunguzi ukibaini kuwa alionewa, watamfanyaje? Kama Nape na Chiligati wakibainika kuwa walimwonea, wachukuliwe hatua gani? alihoji Sumaye.

Maneno hayo ya Sumaye mara moja yalijibiwa na Rais Kikwete ambaye alisema hilo likithibishwa, kutakuwa hakuna njia isipokuwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Sumaye alipokaa aliinuka Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha ambaye naye alieleza kusikitishwa na hatua ya kuzusha tuhuma nzito dhidi ya watu wengine pasipo kuzithibitisha.

Mara tu baada ya mjumbe huyo kuzungumza, Rais Kikwete kwa ushauri wa Mkapa aliwaomba wajumbe kulimaliza jambo hilo akisema ‘imetosha'.

Wakati akifunga mjadala huo mmoja wa watu waliokuwa wamenyosha mkono wakitaka kuchangia alikuwa ni mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale-Mwiru.
Akihitimisha mjadala huo kwa angalizo, Rais Kikwete alisema suala hilo linapelekwa katika Kamati ya Maadili ambako aliwataka kuwasilisha ushahidi wa vielelezo na siyo hujuma dhidi ya watuhumiwa.

SOURCE: TANZANIA DAIMA 25/11/11.

WanaJF, sasa nitawahoji:
1. Je, baada ya kupasua jipu huko Dodoma, CCM sasa ni wamoja na wamepona kabisa au jipu limegeuka kuwa kidonda ndugu?
2. Kitendo cha Mkapa kumpa mwongozo Kikwete wa jinsi ya kuipotezea hii issue ya ufisadi kinaleta taswira gani juu ya uwezo wa Kikwete kama kiongozi mkuu?
3. CCM waendelee na mfumo wa sasa wa mwenyekiti kuwa ndiye mtendaji mkuu, mkufunzi mkuu, mnadhimu mkuu, judge mkuu na msimamizi mkuu wa mambo yote ya chama?
 
Acha kuchakachua mada. Hapa tunaongea mambo ya muhimu yenye mustakabali kwa taifa letu. Leo nataka hii siku tuongelee tu chama chetu tawala. Kile chama kingine hakitakiwi kuzungumziwa kabisa hapa JF. Mpaka 2015 watanzania tutakuwa na option moja tu ya chama cha mababu zetu!
Masikini Nape mmemponza mwenzenu (kwa ujinga wake ofcourse) kwa kumvimbisha kichwa na posts zenu zisizo na miguu wala kichwa, kama Nape atawajibishwa wewe Rejao, ritz, mzee, faizafoxy, Topical mnahusika kwa njia moja au nyingine na yatakayompata hamuwezi kujitetea.
 
Nape ni mtu niliyemwaminia sana CCM kuwa ni asset kubwa yenye very bright futute, alipoanza kupuliza vuvuzela la kujivua gamba, kuna kitu nilimweleza humu humu jf, sasa kimetimia!.

Masikini Nape sio asset tena, ni liability!.

Mkuu hebu tuweke hisia zetu pembeni for once. Hebu nieleze makosa ya Nape kwa kuzingatia

1. Nini Kazi za Katibu Mwenezi Taifa wa CCM
2. Kikao cha NEC cha April 2011 kilitoka na maazimio 26, lipi lilipewa uzito zaidi.
3. Hilo Azimio Lilisemaje?

Binafsi bado nafkiri Nape ni kiongozi imara na ameprove kuwa na guts ambazo ni nadra sana kuzikuta kwa wanasiasa za Tanzania.

Lakini Bosi wake mwenyewe ndio haeleweki ana nia gani au ni KIGEUGEU.
 
Licha ya hii ya Richmond ambayo tunajua urafiki, unafiki na kubebana kunakoiua CCM ndio kulimbebesha Lowasa hili zigo (offcouse alipata chochote) kuna ufisadi/ wizi, kutokuwajibika kwingine anakohusishwa nako?

Kujilimbikizia Ranch za Taifa alipokua Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo na hata namba za vitalu zipo. Kuingia mkataba wa kifisadi wa jengo la Umoja wa Vijana CCM, Nape akamchana live kwa kuonesha sahihi yake kwenye huo mkataba bomu. Kwa taarifa tu, huo mkataba umeshafanyiwa marekebisho makubwa sana na kuondoa vipengele vya kifisadi. Jiulize wakati anasign hakuviona hivyo vipengele au kitu alicholishwa kilimpofua?

Na mengine mengi yamejaa kwenye thread nyingine nyingi juu ya huyu mtu...
 
1. Mh.Lowassa naye alilidanganya bunge kwa kusema kuwa alifikiria tuhuma dhidi yake ni uwaziri mkuu wakati anajua kabisa hilo haikuwa sababu ya kutuhumiwa hivo.

2. Kama alijiuzulu kwa linda heshima ya chama(Mwenyekiti wake) na serikali yake(Rais); huku akijua kitendo hicho kilikuwa kinatoa fursa ya kuficha uovu(ufisadi), haoni kuwa hakututendea haki watanzania tupendao utawala bora na wala hatupendi kabisa utawala balaa?
Ndio maana baadhi yetu tunahoji kwa nini Lowasa hakujiuzulu wakati ule JK alipomkatalia kuuvunja mkataba wa Richmond baada ya kumpigia simu akiwa nje ya nchi? Kwa nini suala hili liliendelea kuzimwazimwa na Lowasa mwenyewe kwa kuwatumia akina Hosea hadi Bunge lilipounda kamati ile ya akina Mwakyembe?
 
Mi cjui bana, maana lishanichosha sasa....hata hivyo, ,kuna jambo moja ambalo nalifahamu kwa 100% ambalo naweza kulisimamia hata The Hague. Nakumbuka aliwahi kusema : "Mheshimiwa Spika, Nimedharirishwa sana! Nimechafuliwa sana! Nimetukanwa sana! Lakini najua, tatizo ni uwaziri mkuu!"

Leo hii:
"
tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015."

Sooner or later
"Babaz Maaskofu, nimedharirishwa sana , nimechafuliwa sana, nimetukanwa sana! lakini kubwa ninalofahamu kwa vita hii ya sasa ni Unaibu Katibu Mkuu wa UN!"

Mkuu huyu jamaa anamatatizo sana.

Badala ya kujitazama alipojikwaa, yeye yuko busy kushift the blame.

Kazi kusema TATIZO NI UWAZIRI MKUU, mara TATIZO NI URAIS,... Hakuna hata siku amejiuliza pengine TATIZO NI TAMAA YANGU NA TABIA YA WIZI.
 
Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alinukuliwa akisema: “Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?”.

“Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,”alinukuliwa akihoji Lowassa.

Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: “Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo”.

Lowassa alisema kama alivyozungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa walipokutana jijini Dar es Salaam, tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015.

“Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,”alinukuliwa Lowassa katika maelezo yake ndani ya NEC

Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo alidai kwamba siyo la kweli.



"LOWASSA UKIGOMBEA MIMI KURA YANGU UNAYO NA KAMPENI NITAPIGA. ACHA WALE WENYE CHUKI BINAFSI KWA SABABU YA NAFSI ZAO BINAFSI. TUNAHITAJI KIONGOZI WA KUIVUSHA NCHI KUTOKA HAPA ILIPO KWENDA KWENYE HALI NZURI ZAIDI" WEWE NI CANDIDATE NAMBA MOJA AMBAYE MIMI NAMWONA HASA KUTOKA KATIKA CCM NA HATA UPINZANI!
 
Lowassa, acha waseme tu lakini wewe unafaa najua wale watz wasiopenda kuwajibika hawataki kukuona uko bado kwenye system!
 
wadau niwaambie ukweli lowasa wamemchafua tu.kama ccm itakuwa madarakani basi raisi wao awe lowasa hawa wngn wanafiki tu
 
Nakubaliana nawe Mr President. Nasikia pia upo muafaka kati ya wakatoliki na waprotestant kuwa Rais ajaye atoke kwa waprotestanti na si mwingine bali Lowassa ingawa mwanzoni walimtaka Sitta wakaja gundua hana msimamo. Sitta na kundi lake hawatakaa kimya. Wana mpango wa kuyaanika yote yaliyobaki kwenye ripoti ya Richmond hata kama yatamuumiza JK.

Damn... I hope and pray this is not the case. Outright udini na MoU kabisa!

Mkuu ninavyofahamu mimi, wakatoliki na waprotestanti wanavyama mabalimbali miongoni mwao. Sasa hapa unataka kusema hata wapenzi na wanachama wa CHADEMA, chama chao hakitasimamisha mgombea wa URAIS iwapo Lowassa atapitishwa na CCM pamoja na zigo la mikashfa ya kuliangamiza taifa kwa ufisadi au watamuweka mgombea "boya" ili Lowassa ashinde kirahisi na kusiwe na mgogoro ya uchakachuaji?

If that is the case then naililia nchi yangu. UKOMBOZI wa kweli kumbe bado sana... Akina Slaa, Mbowe, Lissu wote watakua wanatuchezea akili zetu kama watoto wadogo. Huku hawana chembe ya uzalendo wa kweli. It has to be Slaa or LISSU for CHADEMA
ticket.

Lets wait and see 2015 kama CHADEMA wasiposimamisha a "really strong" candidate then the WRITING WILL BE ON THE WALL!
 
Hakuna mkweli kati yao. Kwa nguvu na mamlaka aliyonayo jk ndani ya chama na serikali kwa ujumla. It was a deal between lowassa aje aseme ivyo. Since wanachama wa ccm wanasurvive kwa kujipendekeza kwa rais ,ivyo walijua hakuna wa kumuandama jk kama wanavyofanya kwa lowasa
 
Watanzania sasa amua wenyewe. Lowassa kwa mara nyingine amemshinda Kikwete je Bunge letu litaendelea kuchekelea kwa vile wote ni nyani wana mikia?
Haya chini ni maneno mazito aliyomwaga Lowassa akiamua kumwaga mboga baada ya Kikwete kutaka kumwaga ugali.

"Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".

"Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji Lowassa.

Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: "Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo".

Hapa anatumia tu vitisho wasimshughulikie. Tatizo lipo kwenye kuingia huo mkataba, angetueleza aliyeshinikiza kutuingiza kwenye mkataba huo wa kitapeli, anatumia hoja dhaifu kutisha magamba wenzake na kwa sababu sehemu kubwa ni wezi basi wanahofu.

Atueleze mchako tangu mwanzo, unaingia mkataba mbovu na kampuni hewa, kisha unajijengea mwanya wa kuja jitetea eti nilimshauri rais tuvunje, utetezi wa kitoto kabisa.
 
Niceeeeee............!!!!! veriiiiiiiii gudiiiiiii, let me add this ujue Lowassa is free from magamba,...

JK kasemaaaaaaa....MWENYE USHAHIDI KUHUSU TUHUMA ZA LOWASSA AZILETE, LA SIVYO WAPAYUKAJI WAKINA NAPE & CHILLI. WATACHUKULIWA HATUA ZA KINIDHAMU, eeeehh bana JK kamaliza kazi, SUMAYE KAPIGILIA MSUMARI WA MOTO, yaani NGUVU YA SUMAYE + LOWASSA ni nomaaaa,

EL FOR PRESIDENT 2015, u hve ma vote, sisikii, sielewiii, sioniii, tunataka Kiongozi mchapa kazi, hata YESU ALICHUKIWA NA KUUAWA, sembuse Lowassa, go buddy....i am done, period..!!!
 
CCM wanamwaya EL and of course he has bigger brains than the rest Ikulu aspirant. CCM mtaji wao uliobaki ni EL JK anamalizia last chapters za riwaya yake ya Maendeleo kwa Kila Mtanzania.
 
Safari hii akina Makongoro kimyaaaa! Au wamepata ukweli mwingine kutoka "site"?
 
  • Thanks
Reactions: 911
Mfumo wa Vyama vingi ulianza kipindi cha 92/93.

Uchaguzi Mkuu wa Urais ni kila baada ya miaka mitano, yaani 1995, 2000, 2010 n.k

Hiyo ripoti ya Mwakawago ya 1997 naamini ilikua ni huko CCM.

Jakaya Kikwete alishateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa tangu 1995.

Rais Mkapa kwa utamaduni wa CCM ilikua akae vipindi viwili mpaka 2005.

Sasa hili la wananchi kutomkubali Jakaya Kikwete, tena mwaka 1997 mbona haliingii kichwani? au waandishi wamekosea kumnukuu?

Hii haijakaa sawasawa...
 
Mamvi ni rais wa JF tu na si vinginevyo... na ni raisi wa wale tu walio na mtindio wa Ubongo
 
Hiyo ni sehemu tu ya yale mengi ambayo Lowassa atayaweka wazi kadri siku zinavyozidi kwenda kimaandishi na kisauti pia kuna na hapo ndipo utakapogundua kuwa hakurupuki na ana sababu za kukaa kimya. Walimtoa Sokoine sasa tunae lowassa kumbuka mmsai hakisoma hafanyi ajizi.
Mkuu ebu acheni Ujinga wengine hapa tunatumia akili na sii masaburi... Sasa kama habari hii ni yakweli.. Lowassa alijuaje na kutaka kuuvunja mkataba ikiwa mkataba ulikuwa wa JK rais wake....Halafu JK kusema tu alikuwa akipata ushauri wa makatibu wake (watendaji wa kiserikali) inaonyesha wazi JK alikuwa akifuata sheria na taratibu za kiserikali laa sivyo asingewahusisha makatibu wakuu kama alivyofanya Lowassa na ushahidi upo akiwaamrisha hao makatibu na waziri wafuate maagizo yake....Tafuta jingine!

Hayo ya 1997 we are interested ni kujikosha na kutafuta huruma za JK...Hata mahakamani mkosa baada ya kupatikana na kmakosa, hupewa muda wa kuomba, kujieleza kabla ya kuhukumiwa kifungo..
 
Na bado, mengi yaja maana watu walimchafua sana EL bila kutafakari huku wakijua kuwa mzee huyu bado hajavunja ukimya wake! Kikubwa tumsisitize EL avunje ukimya aseme ukweli na aache huruma ya kuulinda maslahi ya serikali na chama kinachomchafua kila kukicha!! Huo ndio mwanza bado traller yaja.....pasua jipu hata kama itakugharimu maana ni aheri uhukumiwe na serikali na chama chako kuliko kuadhibiwa na umma. Maana yake ni nini; kwamba umma wataujua ukweli kwamba EL kahukumiwa kwa kuvunja ukimya na kueleza ukweli juu ya Richmond kwa umma!!!
 
Back
Top Bottom