Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa aongea na vyombo vya habari; akataa kugusia suala la Richmond/DOWANS

Lowassa amewaambia waandishi... "This is enough for your stomach" statement hii ni dhihaka kwa taaluma ya habari. Halafu kuulizwa swali ukasema eti hilo swali sijibu, siyo taratibu za kufanya press conference. Haina maana then, waandishi wote walitakiwa kuondoka na kumwacha pekee yake, ama sivyo amewahonga.....
 
Ndugu zangu wana JF. Kwanza kabisa napenda kumshukuru na kumpongeza sana "INVISIBLE" kwa kutuhabarisha juu ya kilichokuwa kinaendelea Monduli, kabla na baada ya mkutano wake Mh. Edward Lowasa na waandishi wa habari leo.

Nimeipitia kwa umakini sana hotuba ya Mh. Edward Lowasa aliyoisoma leo mbele ya waandishi wa habari jimboni kwake Monduli. IENISIKITISHA SANA. Sikutegemea kama Mh. Lowasa baada ya misukosuko yote hii, aendelee kuwa "muongo" kiasi hiki. Hili linanipa tabu kichwani mwangu na, hasa pale anaposema na kuonekana akiombewa na TB Joshua.

Sio kweli kama Mh. Lowasa hukuwahi kupanga kugombea Urais mwaka 2010. Mipango hii ulikuwa nayo na uliwashirikisha baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa kadhaa, wabunge na makatibu wa CCM wa mikoa kadhaa. (Majina na vituo vyao vya kazi tunahifadhi kwa sasa). Mipango yako hii ilikuwa inajulikana kwa viongozi mbali mbali ikiwa ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Baada ya kuona maji ni marefu ktk kutekeleza mipango yako hiyo, ulimshawishi Waziri Mkuu mmoja mstaafu agombee na wewe ulikuwa tayari kumsaidia, tumshukuru mke wa Mheshimiwa huyo, kwani alimkatalia mume wake kata kata, na hata kutishia kuvunjika ndoa. Mama huyo alimwambia mumewe kuwa amtizame mbunge mmoja toka kanda ya ziwa aliyejiuzuru kwa kushawishiwa na kundi lako, na sasa anavyoteseka, maana hata nauli inamshinda.

Kumekuwa na mipango ya kupeleka ktk Halmashauri Kuu ya Chama ijayo hoja ya kutenganisha kofia ya Uenyekiti na Urais, HOJA hii inatoka kwako, na watu wako ndio wanayoiuza kwa wajumbe. Je, hizi sio hujuma kwa Mwenyekiti unayedai kuwa hamkukutana mitaani? Kuipeleka hoja hii ktk vikao vya Chama kunamsaidia nini Mwenyekiti wa Chama?

Hivi karibuni tumemshuhudia Kiongozi mmoja wa UVCCM akiwakemea VIONGOZI wake akiwa Arusha. Siku chache baadae ulimwita na kumpongeza kwa utumbo aliousema. Leo hii unatuambia kuwa eti huhusiki na mgogoro wa kisiasa mkoani Arusha, maneno hayo kawaambie wajinga, welevu wanajua nini kinachoondelea. Halafu umejichanganya ktk maelezo yako kwa kutoa rai kuwa UVCCM waachwe wafanye mambo yao Hivi hiki kinachoendelea UVCCM unaona kinafaa hata waachwe? Wote wanaeleta fujo ndani ya Chama na Jumuiya zake ni watu wako wa karibu, utakaaje kuwa nawe huhusiki? Mbona hatujasikia ukiwakemea waache ujinga wanaoufanya?

Mh. Lowasa, hivi ni kweli kuna kundi la watu wanaotaka kukugombanisha wewe na Rais au wewe na tamaa zako ndio unajigombanisha na Rais? Hivi utaacha lini uongo wa namna hii? Nilidhani ulipoenda kwa TB Joshua basi utaenda kuungama, kumbe sio vile hata kidogo. Tutamwambia Rev. Joshua azidi kukuombea angalau uache tabia ya kusema uongo.

Kusema ukweli hotuba yako ya leo imekera saana na hasa pale unapotumia nafasi zako mbali mbali ulizoshika na unazoshika kukinga maovu yako. Ulishindwa kujirekebisha tabia yako ulipopewa Uwaziri Mkuu na JK, ukatuingiza ktk RICHMOND. Baada ya kushinikizwa UJIUZURU ukadai bungeni kuwa umeonewa. Waziri Mkuu anaonewa na nani????? Nenda kawadanganye hao hao wenye njaa na walio tayari kuona Taifa lao linaingia ktk matatizo kwa ajili ya kukutetea.

Nakushauri ukae kimya au la, utaumbuka kuliko unavyodhani. Utashinda mahakamani kuwashitaki waandishi wote wa habari, maana hata hao wanaokutetea itafika wakati watazidiwa nguvu na Umma. Mh. Lowasa, kubali tu kuwa tamaa zako ndio zimekufikisha hapo. Usichokonoe mengine ambayo watu walikuwa wameamua kukusitiri.
 
Invisible naona huna tofauti na waandishi hao wa udaku

katika maswali yoote wewe ya Richmond ndio umeona muhim kumtuma mtu wako amuulize?

mbona hamjamuuliza kuhusu 300 milion usd alizo nazo Geneva?

acheni kutuchezea akili nyie watu

manajua fika akina kubenea watauliza maswali hayo hayo na nyie meenda kuuliza hayo hayo

Just when you think JF was different from MSM...wapi!
Mkuu jasonbourne nakwaminia kwa data, hivi huyu jamaa ni tycoon wa nguvu heeeeeeeeeeee????????????
 
Sidhani kama huu mkutano alioitisha Mzee Lowassa una uhusiano wowote na watanzania wa kawaida.Hakuna alichoingea ukaona ni message kwa watanzania wauza viberiti Ubungo mataa au wauza maji ya madumu Kijitonyama kwa Ali Maua! Kwa mtazamo wangu huu ulikuwa ni mkutano wake yeye Lowassa na wana-ccm wenzake kupitia vyombo vya habari. Ni hivi, ccm haonani uso kwa uso kwa hiyo wamebuni njia ya mawasiliano ambayo ni vyombo vya habari. Unfortunately, hiki chama (ccm) ndio kina jukumu la kupunguza makali ya maisha, kupunguza mfumko wa bei, kutoa huduma za afya, kutoa ulinzi kwa raia na mali zao, etc etc. Sasa, kama wako busy 'kuwasiliana' kwa nini nchi hii isiendelee miguu juu kichwa chini? And worst of all, we are stuck with these people for another painful 4 years! God help us.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Mh. Lowasa unasema kuwa ndani ya Chama kuna matatizo, je unajua matatizo hayo yameanza lini na yamesababishwa na nani kama sio wewe baada ya kufukuzwa na Wabunge ktk nafasi ya Uwaziri Mkuu? Hivi unajua hujuma zilizokuwa zinafanywa na kundi lako ktk uchaguzi wa Igunga (majina nayahifadhi kwa sasa). Walidiriki hata kusema kuwa "bora CCM ishindwe ili tuheshimiane". Halafu leo unadai eti wewe humhujumu Mwenyekiti JK. Mulitaka CCM ishindwe Igunga ili muitumie hoja hiyo kuzuia zoezi la kujivua gamba ktk NEC ijayo. Kama hili hulijui basi waulize wenyeviti wa DSM na Shinyanga watakwambia.
 
Ndugu zangu wana JF. Kwanza kabisa napenda kumshukuru na kumpongeza sana "INVISIBLE" kwa kutuhabarisha juu ya kilichokuwa kinaendelea Monduli, kabla na baada ya mkutano wake Mh. Edward Lowasa na waandishi wa habari leo.

Nimeipitia kwa umakini sana hotuba ya Mh. Edward Lowasa aliyoisoma leo mbele ya waandishi wa habari jimboni kwake Monduli. IENISIKITISHA SANA. Sikutegemea kama Mh. Lowasa baada ya misukosuko yote hii, aendelee kuwa "muongo" kiasi hiki. Hili linanipa tabu kichwani mwangu na, hasa pale anaposema na kuonekana akiombewa na TB Joshua.

Sio kweli kama Mh. Lowasa hukuwahi kupanga kugombea Urais mwaka 2010. Mipango hii ulikuwa nayo na uliwashirikisha baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa kadhaa, wabunge na makatibu wa CCM wa mikoa kadhaa. (Majina na vituo vyao vya kazi tunahifadhi kwa sasa). Mipango yako hii ilikuwa inajulikana kwa viongozi mbali mbali ikiwa ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Baada ya kuona maji ni marefu ktk kutekeleza mipango yako hiyo, ulimshawishi Waziri Mkuu mmoja mstaafu agombee na wewe ulikuwa tayari kumsaidia, tumshukuru mke wa Mheshimiwa huyo, kwani alimkatalia mume wake kata kata, na hata kutishia kuvunjika ndoa. Mama huyo alimwambia mumewe kuwa amtizame mbunge mmoja toka kanda ya ziwa aliyejiuzuru kwa kushawishiwa na kundi lako, na sasa anavyoteseka, maana hata nauli inamshinda.

Kumekuwa na mipango ya kupeleka ktk Halmashauri Kuu ya Chama ijayo hoja ya kutenganisha kofia ya Uenyekiti na Urais, HOJA hii inatoka kwako, na watu wako ndio wanayoiuza kwa wajumbe. Je, hizi sio hujuma kwa Mwenyekiti unayedai kuwa hamkukutana mitaani? Kuipeleka hoja hii ktk vikao vya Chama kunamsaidia nini Mwenyekiti wa Chama?

Hivi karibuni tumemshuhudia Kiongozi mmoja wa UVCCM akiwakemea VIONGOZI wake akiwa Arusha. Siku chache baadae ulimwita na kumpongeza kwa utumbo aliousema. Leo hii unatuambia kuwa eti huhusiki na mgogoro wa kisiasa mkoani Arusha, maneno hayo kawaambie wajinga, welevu wanajua nini kinachoondelea. Halafu umejichanganya ktk maelezo yako kwa kutoa rai kuwa UVCCM waachwe wafanye mambo yao Hivi hiki kinachoendelea UVCCM unaona kinafaa hata waachwe? Wote wanaeleta fujo ndani ya Chama na Jumuiya zake ni watu wako wa karibu, utakaaje kuwa nawe huhusiki? Mbona hatujasikia ukiwakemea waache ujinga wanaoufanya?

Mh. Lowasa, hivi ni kweli kuna kundi la watu wanaotaka kukugombanisha wewe na Rais au wewe na tamaa zako ndio unajigombanisha na Rais? Hivi utaacha lini uongo wa namna hii? Nilidhani ulipoenda kwa TB Joshua basi utaenda kuungama, kumbe sio vile hata kidogo. Tutamwambia Rev. Joshua azidi kukuombea angalau uache tabia ya kusema uongo.

Kusema ukweli hotuba yako ya leo imekera saana na hasa pale unapotumia nafasi zako mbali mbali ulizoshika na unazoshika kukinga maovu yako. Ulishindwa kujirekebisha tabia yako ulipopewa Uwaziri Mkuu na JK, ukatuingiza ktk RICHMOND. Baada ya kushinikizwa UJIUZURU ukadai bungeni kuwa umeonewa. Waziri Mkuu anaonewa na nani????? Nenda kawadanganye hao hao wenye njaa na walio tayari kuona Taifa lao linaingia ktk matatizo kwa ajili ya kukutetea.

Nakushauri ukae kimya au la, utaumbuka kuliko unavyodhani. Utashinda mahakamani kuwashitaki waandishi wote wa habari, maana hata hao wanaokutetea itafika wakati watazidiwa nguvu na Umma. Mh. Lowasa, kubali tu kuwa tamaa zako ndio zimekufikisha hapo. Usichokonoe mengine ambayo watu walikuwa wameamua kukusitiri.

Mengi ya hayo uliyoongea ndio tulitegemea angeyatolea ufafanuzi, lakini matokeo yake kaishia kutisha vyombo vya habari na wanahabari
 
Sidhani kama huu mkutano alioitisha Mzee Lowassa una uhusiano wowote na watanzania wa kawaida.Hakuna alichoingea ukaona ni message kwa watanzania wauza viberiti Ubungo mataa au wauza maji ya madumu Kijitonyama kwa Ali Maua! Kwa mtazamo wangu huu ulikuwa ni mkutano wake yeye Lowassa na wana-ccm wenzake kupitia vyombo vya habari. Ni hivi, ccm haonani uso kwa uso kwa hiyo wamebuni njia ya mawasiliano ambayo ni vyombo vya habari. Unfortunately, hiki chama (ccm) ndio kina jukumu la kupunguza makali ya maisha, kupunguza mfumko wa bei, kutoa huduma za afya, kutoa ulinzi kwa raia na mali zao, etc etc. Sasa, kama wako busy 'kuwasiliana' kwa nini nchi hii isiendelee miguu juu kichwa chini? And worst of all, we are stuck with these people for another painful 4 years! God help us.

Kama Mungu aliweza kuwanusuru watu wake ktk enzi za Yesu Kristo na Mtume Mohamed, nina imani atatunusuru nasi, tusiache kumuomba.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nadhani tunahitaji kufikiri zaidi kuhusu maendeleao ya nchi badala ya mtu mmoja ambaye ni JANGA kwa mustakabali na ustawi wa nchi. Ina maana Tanzania bila Lowassa haitaweza kusonga mbele? Mnaoendelea kumlamba miguu mna lenu jambo. Let us discuss about the country's development not the country's DRACULA.
 
Hi Forks,
Najaribu kutafakari kwa kina kuhusu mpambano na mnyukano
wa nafasi ya mgombea wa kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania 2015 kupitia chama cha Mapinduzi CCM nafasi yake kwa asilimia kubwa inaweza kumwangukia
Mh Edward N.Lowasa.
Sasa najiuliza:
  • Endapo atapewa hiyo nafasi na akashindwa na vyama vya Upinzani atakuwa tayari kukubali?
  • Na Je,Endapo atashinda atakuwa tayari kufanya kazi na mahasimu wake wakuu?
Nawasilisha

Unaota ndoto. Yeye atakuwa mgombea wa upinzani wakati huo. Tujiulize, yeye atakubali kushindwa na mgombea wa CCM?
 
kumbe hata lowasa hawezi kufanya maamuzi magumu.ni heri angeendelea kukaa kimya.
 
Mh.Lowassa ni mtu mashuhuri na mtu muhimu sana ktk siasa za Tanzania
na kama humfahamu basi wewe utakuwa mgeni hapa Tanzania.
Ni Mbunge wa Monduli na anaheshima kubwa kwenye Jimbo lake na kwa Nchi nzima
Mh Lowassa ameshakuwa na majukumu mengi sana nje na dani ya chama chake cha ccm.
Pi Mh.Lowassa ameshaingia kwenye kashfa mbalimbali za ndani na nje ya nchi na zote ni kashfa zenye akili,
kashfa zilizoenda shule,Mh.hana utani na pesa,anajua jinsi ya kuzitafuta na akiwekwa kwenye nafasi ya urais
anaweza kabisa kutuletea pesa nyingi hapa Tz na zingine akachimbia huko majuu kuongezea za kwake,

Mtoto wa kiume huna aibu kushabikia ujinga? Au nyie ndo wale wanaompa relief huyu bwana. Tumikia baba, ulipe madeni ya watu!
 
Wakuu,

Muda si mrefu tutaweza kwenda Live kutokea Monduli ambapo Mhe. Lowassa (Waziri Mkuu aliyejiuzulu) atakapoongea na vyombo vya habari. Tumefanikiwa kupenyeza mtu hivyo tutaweza kuwaletea alichoongea. Nita-update 1st post kulingana na atakavyokuwa anaongea.

Shukrani

=================

  • Mwandishi wetu kamsisitizia kuwa watu wamesisitiza wanataka kujua kauli yake juu ya Richmond/Dowans/Symbio na suala la kujivua gamba ndani ya CCM, vinginevyo mkutano huu hautakuwa na maana na watu wanahisi labda umetishwa. Kajibu kuwa masuala haya atayazungumzia lakini leo si wakati muafaka, kuna wakati atayazungumzia.
  • Mwandishi kamwuliza kama ametishwa, maana anaonekana kila la muhimu hataki kuongelea, kajibu kirahisi tu "SINTOJIBU MASWALI HAYO"
  • Mwandishi wetu pia kamwuliza juu ya 'Uvuaji Gamba', nalo kakataa katakata kuongelea, kasema si wakati muafaka.
  • Pamoja na mwandishi wetu kumweleza umuhimu wa yeye kuongelea suala la DOWANS/Richmond kakataa katakata na kusema ataliongelea wakati muafaka na si leo.
  • Wakuu... Kamaliza! Ila kamalizia na "I think this is enough for your stomach" sasa sijaelewa anamaanisha alichoongea au ......?
  • Juu ya DOWANS: Kaulizwa itakuwaje asihusishwe kwenye mjadala huo ilhali kuna watu ndani ya CCM wameshasema waliojiuzulu ndo walipe? Kasema SINA MUDA WA KUJIBU SWALI HILO!
  • Juu ya urais 2015: Hata mimi nashangaa, miaka bado sana, kwanini tuanze kuongelea urais wa 2015? Waandishi acheni propaganda, msipoandika chokochoko hizi hakuna atakayehangaika nazo.
  • Mitikisiko ndani ya CCM ni ya muda tu, tutapita katika hali hii.
  • MAJIBU: Si kama napuuza jitihada za serikali juu ya suala la ajira kwa vijana, lakini hali ni mbaya sana. Nashauri tuvunje kanuni, serikali ikope fedha na ijenge viwanda tuweze kuwaajiri watanzania wengi. Fedha zipo!
  • Moses Mashalo kauliza juu ya mustakabali wa CCM kwa siku zijazo kufuatia hali inayoendelea kwa sasa ndani ya CCM.
  • KAMALIZA... Maswali yanafuata
  • Uchumi wa dunia upo taabani, taifa letu linakabiliwa na hali mbaya. Shilingi yetu inazidi kuporomoka vibaya. Inflation inazidi kuelekea kubaya zaidi. Kuna tatizo kubwa la ajira kwa vijana, kubwa sana. Vijana wakiishi katika hali hii tutakuwa tumekalia bomu la muda na itapelekea kuvunjika kwa amani. Ni vyema tukatafuta suluhu ya mambo haya.
  • Naomba vyombo vya habari tusaidie nchi yetu. Tunapoandika propaganda za chuki kwa nia ya 'kulipuana' tujue tunalipeleka taifa kubaya.
  • Sasa niseme rasmi, IMETOSHA. Sintoendelea kuvumilia kuchafuliwa na vyombo vya habari. Nitachukua hatua kali dhidi ya magazeti yatakayonichafua na vyombo vya habari vyote vinavyonichafua. Ukinichafua nitakupeleka kwenye vyombo husika na niseme uhuru usio na nidhami ni fujo. Uhuru wa vyombo vya habari umekuwa 'abused' sana.
  • Vijana mara nyingi ni radical, wasibezwe na wasilaumiwe kwa wanachofanya bali waelekezwe. Anayekiuka sheria asifumbiwe macho.
  • Vijana wa UVCCM tusiwaingilie, ni taasisi muhimu kwa ajili ya chama chochote cha siasa.
  • Sheria ni sheria, hakuna aliye juu ya sheria. Kama kuna sheria inavunjwa hakuna anayetakiwa kuangaliwa tu.
  • Gazeti flani linaloniandama lilishafikia hatua ya kusema ndo nahusika na maasi ya vijana wa UVCCM, ni uwongo na wala sihusiki kwa namna yoyote na vijana wa Arusha. Nilikuwa nje kwa matibabu, ningejuaje nini wanapanga vijana?
  • Sijakutana na rais Kikwete barabarani, waache kunichonganisha naye na waache kunichafua mbele za watanzania. Walishasema eti nagombea urais mwaka 2010. Naamini hata rais Kikwete anajua kuwa huu ni uzushi tu.
  • Masuala ya Chama huwa yanaishia kwenye vikao, hii ya kubomoana nje ya vikao hayana maana. Siwezi kukihujumu chama changu mwenyewe.
  • Kuna waliofikia kudai eti namhujumu Mhe. Rais. Wengine eti nna mpango wa kumpindua kwenye Halmashauri kuu ijayo. Sina mpango wa hujuma na hata mabaya ya rais Kikwete siyafahamu.
  • Toka nilipojiuzulu uwaziri mkuu nilikaa kimya, kimya ni hekima toka kwa Mwenyezi Mungu
  • Anaomba kutoulizwa maswali ambayo ni nje ya hoja anayoongelea.
  • Anaanza kuongea sasa...
  • Alishakaa ili aanze kuongea, kaondoka na inaelekea kama kuna jambo anaenda kuliweka sawa kwanza.
  • Ilitarajiwa angeanza saa 4 kamili lakini inaelekea ataanza saa 4 unusu, waandishi wapo wengi. Atajivua gamba?
=============
UPDATE
=============
Full text ya alichozungumza Lowasa[/ATTACH]

Leo wengi tumekasirika na press conference ya EL kwasababu tu hakuongelea Dowans na Gamba. Ni sawa kabisa kwasababu ndiyo dukuduku la kila mwananchi, kwamba hao wanaomtuhumu kwa gamba au ufisadi ni kwasababu ya Dowans. Lakini kwa wale wanaoelewa vizuri siasa za CCM, press ya leo una ujumbe mzito sana na very intelligent. Wengi tulipongeza hotuba yake ya Maamuzi magumu kwasababu alii-challenge regime, lakini ya leo ni party politics done very well. Lets watch this space, bado ukweli unabakia mtu anayesema Lowassa ni mwizi, hana ushahidi, kama ambavyo unaweza kutuhumu viongozi wote wa CCM na upinzani kwa ufisadi. Na mtu akisema Lowassa siyo candidate mzuri kwa 2015, unamwambia akutajie a better candidate, inakuwa mgogoro.
 
Wengi wetu tuliokaa mkao wa kula toka jana na kudhani kiranja wa Monduli atamwaga ugali baada ya mpangaji wetu wa Magogoni kumwaga mboga miezi kadhaa ilopita tumepigwa na butwaa baada ya EL kuongelea ajira ya vijana hahaha!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
INVISIBLE nimekukubali 100%,
ila sioni kama kulikuwa na haja ya kuita waandishi wa habari wakati huna majibu ya maswali ambayo kila siku watanzania wamekuwa wakimlalamikia yeye. Kwanini waandishi wasingeamua kuondoka! Ninachokiona mimi aliitisha mkutano kuwatetea UVCCM, badala ya kujitetea yeye.
 
Hutafanikiwa kwa kuwatisha waandishi wa habari. Fanikio lako ni kukiri na kutubu kwa wananchi wa Tanzania kwa madhambi uliyoifanyia nchi hii. Tuanze pale alipoishia marehemu Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere. Hakusita kukwambia ukweli kuwa wewe HUFAI kuwa Kiongozi wa nchi hii. Alikupa sababu za kusema vile. Bado hadi leo sijasikia au kuona sehemu au wakati wowote ukiomba radhi, badala yake umekuwa ukiendelea kujilimbikizia mali na kutafuta uongozi kwa gharama zozote. Lowasa mambo haya uwe unaongea na wajinga wanaoshindwa kukwambia ukweli juu ya taswira yako kisiasa nchini. UNANUKA ndugu yangu. Heba siku moja jaribu kupita Kariakoo mchana uone wananchi watakavyokupokea.
 
KGBtz, hivi ni kweli unataka kutuambia kuwa hujui wizi wa EL au unatania? Uliishawahi kumuuliza Marehemu Baba wa Taifa kwanini alimwambia EL kuwa HAFAI kuwa kiongozi wa nchi hii? Hivi unalijuaje suala la RICHMOND/DOWANS? Better candidates wataonekana baada ya kuchukua fomu za kugombea, wazuri ni wengi sana lakini kama hawatachukua fomu haitatusaidia kujadili sasa hivi.
 
Kuwa na nyumba London sio utajiri ni rahisi sana, kule nyumba zinauzwa kama magari na thamani ya nyumba iliyotumika ni ndogo sana, mahesabu huwa yanapigwa kutokea nyumba ilipojengwa. Kutokana na muda ambao amefanya kazi EL hata kama ni wewe kama ungekuwa na akili za maendeleo ungeweza kuwa na zaidi ya hata alivyonavyo EL pamoja na kuwa mengi ni maneno wala sio kweli. Ukiulizwa nyumba iko London mtaa gani na ni plot namba ngapi huwezi kujibu.
Bwn Exaud Minja wacha kukurupuka mitaa zilipo hizo nyumba inafahamika, tena iliwekwa wazi hapa jamvini toka kwa kitengo cha uchunguzi wa uchumi SFC cha UK!!!!!!!! Mpaka acct za Bank zilizopeleka fedha na CO zilizotoa fedha!!!!!!!!! Hiyo ni cha mtoto je USD $300million zilizoko Swizz Bank vipi unayo majibu???????????????
 
Kweli Magamba wanasiasa wote ni CRAP!!!!!!!! Unaita watu Monduli kuongea hayo, bora hilo la kujenga viwanda mengine yote ni pumbaaa:shock:

Hivi kumbe Mkutano ulikuwa Monduli??? Duh, sasa nani amelipa hizo gharama..??? Kwa Bongo inawezekana hata nauli amewalipia waandishi wa habari kuhudhuria!!!!
 
Back
Top Bottom