Ndugu zangu wana JF. Kwanza kabisa napenda kumshukuru na kumpongeza sana "INVISIBLE" kwa kutuhabarisha juu ya kilichokuwa kinaendelea Monduli, kabla na baada ya mkutano wake Mh. Edward Lowasa na waandishi wa habari leo.
Nimeipitia kwa umakini sana hotuba ya Mh. Edward Lowasa aliyoisoma leo mbele ya waandishi wa habari jimboni kwake Monduli. IENISIKITISHA SANA. Sikutegemea kama Mh. Lowasa baada ya misukosuko yote hii, aendelee kuwa "muongo" kiasi hiki. Hili linanipa tabu kichwani mwangu na, hasa pale anaposema na kuonekana akiombewa na TB Joshua.
Sio kweli kama Mh. Lowasa hukuwahi kupanga kugombea Urais mwaka 2010. Mipango hii ulikuwa nayo na uliwashirikisha baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa kadhaa, wabunge na makatibu wa CCM wa mikoa kadhaa. (Majina na vituo vyao vya kazi tunahifadhi kwa sasa). Mipango yako hii ilikuwa inajulikana kwa viongozi mbali mbali ikiwa ni pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM.
Baada ya kuona maji ni marefu ktk kutekeleza mipango yako hiyo, ulimshawishi Waziri Mkuu mmoja mstaafu agombee na wewe ulikuwa tayari kumsaidia, tumshukuru mke wa Mheshimiwa huyo, kwani alimkatalia mume wake kata kata, na hata kutishia kuvunjika ndoa. Mama huyo alimwambia mumewe kuwa amtizame mbunge mmoja toka kanda ya ziwa aliyejiuzuru kwa kushawishiwa na kundi lako, na sasa anavyoteseka, maana hata nauli inamshinda.
Kumekuwa na mipango ya kupeleka ktk Halmashauri Kuu ya Chama ijayo hoja ya kutenganisha kofia ya Uenyekiti na Urais, HOJA hii inatoka kwako, na watu wako ndio wanayoiuza kwa wajumbe. Je, hizi sio hujuma kwa Mwenyekiti unayedai kuwa hamkukutana mitaani? Kuipeleka hoja hii ktk vikao vya Chama kunamsaidia nini Mwenyekiti wa Chama?
Hivi karibuni tumemshuhudia Kiongozi mmoja wa UVCCM akiwakemea VIONGOZI wake akiwa Arusha. Siku chache baadae ulimwita na kumpongeza kwa utumbo aliousema. Leo hii unatuambia kuwa eti huhusiki na mgogoro wa kisiasa mkoani Arusha, maneno hayo kawaambie wajinga, welevu wanajua nini kinachoondelea. Halafu umejichanganya ktk maelezo yako kwa kutoa rai kuwa UVCCM waachwe wafanye mambo yao Hivi hiki kinachoendelea UVCCM unaona kinafaa hata waachwe? Wote wanaeleta fujo ndani ya Chama na Jumuiya zake ni watu wako wa karibu, utakaaje kuwa nawe huhusiki? Mbona hatujasikia ukiwakemea waache ujinga wanaoufanya?
Mh. Lowasa, hivi ni kweli kuna kundi la watu wanaotaka kukugombanisha wewe na Rais au wewe na tamaa zako ndio unajigombanisha na Rais? Hivi utaacha lini uongo wa namna hii? Nilidhani ulipoenda kwa TB Joshua basi utaenda kuungama, kumbe sio vile hata kidogo. Tutamwambia Rev. Joshua azidi kukuombea angalau uache tabia ya kusema uongo.
Kusema ukweli hotuba yako ya leo imekera saana na hasa pale unapotumia nafasi zako mbali mbali ulizoshika na unazoshika kukinga maovu yako. Ulishindwa kujirekebisha tabia yako ulipopewa Uwaziri Mkuu na JK, ukatuingiza ktk RICHMOND. Baada ya kushinikizwa UJIUZURU ukadai bungeni kuwa umeonewa. Waziri Mkuu anaonewa na nani????? Nenda kawadanganye hao hao wenye njaa na walio tayari kuona Taifa lao linaingia ktk matatizo kwa ajili ya kukutetea.
Nakushauri ukae kimya au la, utaumbuka kuliko unavyodhani. Utashinda mahakamani kuwashitaki waandishi wote wa habari, maana hata hao wanaokutetea itafika wakati watazidiwa nguvu na Umma. Mh. Lowasa, kubali tu kuwa tamaa zako ndio zimekufikisha hapo. Usichokonoe mengine ambayo watu walikuwa wameamua kukusitiri.