Uchaguzi 2020 Lowassa: Huko kina Lissu wameanza kujipambanua kwa sera, fujofujo mpaka matv mengine yanatisha. Rais wetu usitishike

Uchaguzi 2020 Lowassa: Huko kina Lissu wameanza kujipambanua kwa sera, fujofujo mpaka matv mengine yanatisha. Rais wetu usitishike

Uzee unakuja na mambo Mengi. Mungu amsamehe huyu Babu kwa kweli
 
Huyu mzee nimemuelewa kuwa Chadema ni wapenda fujo.
 
Tulikuwa tunamsanifu tu. Tulijua lazima arudi nyumbani kwa mafisadi wenzake. Si unaona alivyopokelewa kwa bashasha na fisadi mwenzake pale Lumumba na dereva wake alikuwa fisadi mwandamizi RA
Hilo ndio tatizo lenu hamueleweki mnasimamia wapi. Nina imani hata huyu chotara wa kibelgiji mnaemuabudu leo kesho mtasema hawafai mlikua mnamsanifu tu ili asijisikie vibaya kuachishwa posho za ubunge na kugombea kitu ambacho anajua hakiwezekani kwake.
 
Waziri mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiwa Monduli kwenye kikao cha chama cha mapinduzi ambapo mwanae Fred Lowassa anawania jimbo hilo, alipata fursa ya kuongea na kumuelezea Dkt. Magufuli aliyoyafanya katika vita dhidi ya Korona. Pia kwenye kikao hicho alikuwepo Mizengo Pinda.

Lowassa: Mimi sina mashaka juu ya kushinda, mashaka yangu atapita kwa kura ngapi. Huko kwa kina Lissu wameanza kujipambanua sana, maneno mengi, fujo zile, wanaonekana kwenye mamitaa, matv, matv mengine yanatisha tisha lakini tulimwambia Rais wetu usitishike hata kidogo.

Umma wa watanzania uko nyuma yako na dunia inajua kwamba kuna mwanaume Tanzania. Nasema hivyo kwa sababu, Australia kama ulisikiliza BBC leo, Rais anajiuzulu, kule Bolivia Rais anajiuzulu yote kwa sababu ya hii kitu, Corona si mchezo.

Nyinyi mtu wenu tena mtu mweusi hana nguvu za kimitume anakwenda anawaambia Taifa lake, jamani tumuendee mwenyezi, tumuombe atusaidie tuondokane na hili janga. Watu wa ajabu, wakasema huyu anababaisha tu. Anababaisha? Imepita wiki mbili, tatu hamna korona.

Huyu mzee naye anaongea upumbavu gani huu? Ni ma-TV gani ameyaona yanaonesha kampeni za Lissu? TV zote si kamiliki mzee Walwa?
 
Back
Top Bottom