Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizi lugha za kusema hatujafika ndo akili mgando zinazotumiwa na CCM kuwakandamiza. Kwa nchi yenye Bandari 3, madini ya kila aina kila kona, vivutio vya utalii vinavyotambulika kidunia, nishati ya gas, sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba na rasilimali chungu nzima kuona elimu tu haiwezekani ni kutijusi mwenyewe. Kwangu mie elimu bure inawezekana kama kiongozi ana nia thabiti.
Nakumbuka wale vijana waliojaza uwanja wa taifa wenye degree na masters wakifanyiwa usahili na wengine wanalalamika wanamiaka 2-5 hawajapata kazi wanazunguka na bahasha huku wakiwa na degrees zao leo hii wanaambiwa elimu yao haitoshi!!
Ni ubabaishaji wa sera ya ajira tu mkuu, mshaurini mgombea huyu akimaliza kampeni aitishe mkutano na watu waliosomea fani zinazohusiana na viwanda kuanzia technicians mpaka managers halafu mjadala utaanzia hapo. . . . ..
Kama kweli nia ipo. . . . .
Acha kujichanganya kijana, elimu bora haipimwi kwa wingi wa majengo(vyuo) wala kwa idadi ya wahitimu. First priority ni kuimarisha elimu. Hivyo viwanda si vitakufa tu kama vilivyokufa awali!?. Elimu bora inahitajika, tupate graduate wengi wenye ubora wa kusimamia viwanda vyetu na kuweza kushindana ktk soko la ajira la kimataifa. EL yuko sahihi, hata ccm wanalijua hili.huyo jamaa anazungumzia elimu gan? JK kajenga vyuo vikuu vipya vinne, vyenye uwezo wa kutoa graduates 30000, means kila mwaka kuna graduate wapya 100,000~120,000 ss hao vijana unawapeleka wapi? kwa ss n uimarishaj tu wa elimu unaotakiwa ila viwanda ndo first priority ili nguvu kazi ya taifa itumike kuzalisha
mkuu nakubaliana na wewe,,, ila ngoja nikwambie kitu, ktk nchi za east and central Africa moja ya nchi ambazo ni vigumu kupata kibali cha kufanya kazi kwa mgeni ni Tanzania
lakn currently, viwanda vya Tanzania especially vinavyomilikiwa na wahind au wenye asili hiyo vimejaza wahind kuanzia store,jikon mpk mgt yote wabongo tumebaki kuosha vyombo na kaz za kufagia (km huamin nenda rhino cement tanga).
hawa wahind wanakuja km tourist, uhamiaji wanajua kila kitu na wanawapa vibali vya kuja kutembea ambavyo vinakua renewed kila baada ya miezi mi3! wakuu wa wilaya ukiwambia wanakwambia mkubwa ndo amesema tufanye hivo hatuna jinsi zaid ya kutii amri!!
kuna mengi sana mkuu ambayo nikiongea hapa ntakuchosha, kifupi hawa CCM bora wapumzike tu......JK kawapa nchi hii wahind na wachina wanafanya wanachotaka!!
ndo mana mimi sina imani na mtu yeyote aliepo CCM kwasabb hawez kumkaripia JK, hivi viwanda vingi ana hisa ndo wana wanavunja sheria wanaangaliwa tu
Kusema lazima tusome kwanza wakati wahitimu kibao ambao ni wasomi..mana yake wamekwisha soma wanatafuta kazi na eti tuanze kusoma kama vile hakukuwa na shule ndio tujenge viwanda naona ni "Mtindio" wa akili!!! Watanzania waliokwisasoma na wanaotafuta kazi/ au wajasiriamali tayari wapo wanachohitaji ni kuwezeshwa..Lowassa na sio kupelekwa tena shule! Lkini kiwanda kikijengwa waajiriwa watafunzwa namna ya kuendesha hivyo viwanda!!!
So, the current plants/factories we do have now, how are we operating them? The dude is a fool and dumb.
Waajiriwa kufunzwa namna ya kuendesha viwanda umerudi pale pale, ELIMU ELIMU ELIMU. Jisikilize unavyojichanganya mwenyewe. Kwa maana rahisi wasomi wetu sio competent. Mitaala ya Elimu inatakiwa kufumuliwa na kusukwa upya. Zitaanzishwa elimu maalumu kwa waliohitimu Ku brush walipopungukiwa, waziri wetu wa Elimu Mh Mbatia aliahidi Arusha atalishughulikia hilo.
Tatizo lake anashindwa kutambua kuwa ELIMU YA BURE VIDUDU HADI CHUO kuanzia januari kwa Tz bado hatujafika huko, linaweza likafanyika hilo kama watafosi ila 'wasomi' wataotoka hapo ni MAJANGA. Hivi jamaa anashirikisja timu yake kufikiri au anasema tu kufurahisha 'nyomi' zake?
Lowasa ana vision, maamuzi, ufuatiliaji na ni mzuri kutoa maelekezo kuliko Magufuri, Magufuri si kiongozi bali ni mtendaji.
Suala la kutoa elimu bure kama anavyosema Lowasa linawezekana kabisa. Libya iliweza kutoa elimu, huduma za afya nzuri, huduma za bima na nyinginezo bure kwa miaka mingi kwa ajili ya mafuta tu waliyokuwa nayo. Kwanini Tanzania ishindwe wakati ina gesi, mafuta, dhahabu, almasi, Tanzanite na mbuga za wanyama?. Kinachokosekana katika Tanzania ni Uongozi bora pamoja na mfumo sahihi. Lowasa ni kiongozi bora wala si bora kiongozi, na Chadema wana mfumo mzuri si kama wa CCM. Lowasa ndani ya Chadema ataleta mabadiliko chanya kwa Tanzania na kwa faida ya Watanzania wote.
Lowasa ana qualities za uongozi. Watanzania tusifanye makosa 25th October 2015. Chagua Lowasa, chagua mabadiliko ya kuelekea kwenye maendeleo tuliyonyimwa na CCM kwa miaka 50 iliyopita.
Sijasema HAIWEZEKANI, nimesema bado hatuko tayari kwa hilo na DEFINATELY kwa Januari ndo hatuko tayari kabisaaaaa. Inaweza fosiwa ila tutazalisha vilaza.
Kula Like Mkuu, tuwakumbushe Ajali ya Mv. Bukoba wazamiaji tu ilibidi watoke A. Kusini.
Maeneo mbalimbali tu ambapo zinatumika Mashine za kisasa kufanyia shughuli yoyote kitu kikiharibika kazi zinasimama mpaka fundi wa kurekebisha atoke A. Kusini.
Lowassa yuko sahihi kabisa kwani CCM imetupatia elimu ya kufaulu mitihani tu wala si kutenda na ndio maana anasema atabadili Mitaala yote ili kuiboresha Elimu Nchini.