Elections 2015 Lowassa: Viwanda bila elimu ni sawa na kazi bure

Nakumbuka wale vijana waliojaza uwanja wa taifa wenye degree na masters wakifanyiwa usahili na wengine wanalalamika wanamiaka 2-5 hawajapata kazi wanazunguka na bahasha huku wakiwa na degrees zao leo hii wanaambiwa elimu yao haitoshi!!
 

Usirudie tena hii maneno iko kamili sana asiyetaka kuelewa achana naye kabisa Kingmairo
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka wale vijana waliojaza uwanja wa taifa wenye degree na masters wakifanyiwa usahili na wengine wanalalamika wanamiaka 2-5 hawajapata kazi wanazunguka na bahasha huku wakiwa na degrees zao leo hii wanaambiwa elimu yao haitoshi!!

Achana na siasa. . . . wapo wenye uwezo weeengi sana, wapo wanaohitaji rescucitation kidogo na wapo wabovu ila wooote kuambiwa hawafai si kweli hata kidogo. . . .
 

mkuu nakubaliana na wewe,,, ila ngoja nikwambie kitu, ktk nchi za east and central Africa moja ya nchi ambazo ni vigumu kupata kibali cha kufanya kazi kwa mgeni ni Tanzania

lakn currently, viwanda vya Tanzania especially vinavyomilikiwa na wahind au wenye asili hiyo vimejaza wahind kuanzia store,jikon mpk mgt yote wabongo tumebaki kuosha vyombo na kaz za kufagia (km huamin nenda rhino cement tanga).

hawa wahind wanakuja km tourist, uhamiaji wanajua kila kitu na wanawapa vibali vya kuja kutembea ambavyo vinakua renewed kila baada ya miezi mi3! wakuu wa wilaya ukiwambia wanakwambia mkubwa ndo amesema tufanye hivo hatuna jinsi zaid ya kutii amri!!

kuna mengi sana mkuu ambayo nikiongea hapa ntakuchosha, kifupi hawa CCM bora wapumzike tu......JK kawapa nchi hii wahind na wachina wanafanya wanachotaka!!

ndo mana mimi sina imani na mtu yeyote aliepo CCM kwasabb hawez kumkaripia JK, hivi viwanda vingi ana hisa ndo wana wanavunja sheria wanaangaliwa tu
 
Acha kujichanganya kijana, elimu bora haipimwi kwa wingi wa majengo(vyuo) wala kwa idadi ya wahitimu. First priority ni kuimarisha elimu. Hivyo viwanda si vitakufa tu kama vilivyokufa awali!?. Elimu bora inahitajika, tupate graduate wengi wenye ubora wa kusimamia viwanda vyetu na kuweza kushindana ktk soko la ajira la kimataifa. EL yuko sahihi, hata ccm wanalijua hili.
 

Nimekuelewa sana ila kiu ya mabadiliko isichukuliwe kama room ya kuambiwa kila jambo hata ambayo hayana ukweli au usahihi wa kutosha. . . . .

Tunataka viwanda sababu zipo na uwezo upo mambo ya kupewa sababu nyepesi ili baadaye uambiwe bado tunaandaa wasomi tuyakatae tangu mwanzo kabisa. . . . . Unahitaji miaka minne kuoata engineer, mitatu au minne kupata muhasibu, miwili kupata technician, mitatu kupata mtu wa manunuzi, masoko na boharia hapo wawe wamefika form six bado uzoefu kazini hapo si miaka kumi imeisha mnaachwa kama mlivyokutwa???!!!!

Hapana wagombea lazima wawe precise kwenye wanachokisema.. . . . .
 
CCM inaitawala Tanzania sababu watanzania wengi ni wajinga sana.... na hao wajinga ndio wanaipa mamlaka ya kututawala sote.....
Wanajua kabisa watu wakpata elimu watahoji kila kinachofanyika hivyo kusababisha viongozi kutokuwa miungu mtu...
Elimu iliyopo haifai na haitoshi, ni Lowasa pekee mwenye maono ya Tanzania mpya
 
dist111 we kwel bogus tatzo c kua na vyuo vingi tatzo n elim gn wanaipata we hujiulz kwa nn wakenya wanatuzd kete na kngine elim ya sasa inatakiwa ikisaidie kua mbunifu na co kutegemea kuajiriwa shtuka ww
 
Last edited by a moderator:
Kwenye ilani ya CCM elimu imepewa kipaumbele! Sasa huyo fisadi anazungumzia elimu ya aina gani?

Niandike kwa ufupi tu, duniani hakuna nchi inayotaka kuendelea ikakosa viwanda!
 

Waajiriwa kufunzwa namna ya kuendesha viwanda umerudi pale pale, ELIMU ELIMU ELIMU. Jisikilize unavyojichanganya mwenyewe. Kwa maana rahisi wasomi wetu sio competent. Mitaala ya Elimu inatakiwa kufumuliwa na kusukwa upya. Zitaanzishwa elimu maalumu kwa waliohitimu Ku brush walipopungukiwa, waziri wetu wa Elimu Mh Mbatia aliahidi Arusha atalishughulikia hilo.
 
So, the current plants/factories we do have now, how are we operating them? The dude is a fool and dumb.

Wewe Chin Current Factories unazozisema ziko wapi? Viwanda vichache ni vya wahindi,ambapo Watanzania ni HR,madereva, wahudumu, na kazi za chini kabisa kimaslahi. Kama uko Dar, nakupa Changamoto nenda Kule Temeke Mbozi Road au nenda Mwenge kule karibu na ITV utapata jibu kuwa hatuna viwanda na vilivyopo vya ndugu zetu wenye asili ya Asia(siyo kwa ubaguz hapa) wataalam wengi wameagizwa kutoka India, Bangladesh na Pakistan!
Hata kama u kipofu, uwe mkweli, Tanzania hii ni yetu sote, hata kama u mnufaika kwenye mfumo, lakini kama siyo wewe, basi ndugu, jamaa, marafiki wanapigika kijijini kwenu, uwaonee huruma na wenzako, cake ya Taifa angalau nao waionje!
 

HAPANA. . . . .kufunzwa jinsi ya kufanya kitu inatokana na version ya mashine na technolojia iliyotumika sio suala la ukosefu wa elimu. . . . Short course au on job training ni sehemu ya kuongeza ufanisi. . .

Kufumua na kuboresha mitaala tuko pamoja mkuu
 

Usione kushindwa kwenu CCM kwa miaka yote mliyokuwa madarakani msidhani ndio kushindwa kwa Watanzania wote ndio maana tunawapumzisha mwaka huu muone mawazo mapya
 


Ndugu Msolwa, kwanza ukweli ni kuwa mtu ambaye kawa waziri na PM, hatuwezi kusema hana vision, lakini nataka kukufahamisha ya kuwa hiyo issue ya elimu bure sio issue mbaya lakini lazima iangaliwe vizuri, kwani linaweza kutuharibia elimu ya watoto wetu, na kama halikuwekwa vizuri basi tutapa two different categories of Education:

Leo huku Uingereza kuna matatizo ya elimu, utaona watoto wanosoma private schools wanapata elimu bora kuliko wale wanaosomea public schools, which affects their admissions to the best Universities.

Ndugu Msolwa, Huwezi Fananisha na Tanzania, Kwanza Libya lina idadi ya watu 6,244174, Tanzania Approx:50,000,000,
Libya has the 10th largest Oil Reserves on earth, Tanzania bado hatuja gundua Oil na hatutoi Mafuta, na ndio kwanza mikakati ya kutoa Gesi inafanywa huenda ikachukua miaka mitano ijayo (Export Quantity).

GDP ya Libya ni $70 Billion, ukilinganisha na idadi ya wananchi wao kila mmoja wao anawezakupata $11210/- kwa mwaka. Infact Gadafi alistahili kuwapatia wananchi wake maendeleo zaidi ya hayo. Gadafi na wanae wamechukua mabillion of Dollars na kuziweka USWIS, hivi leo hizo pesa ni Frozen na zinawajenga waswiss.

Ukipata Fursa naomba umuulize huyo Mgombea Uraisi wako, 1974 alikuwa hana hata kibanda, na miaka yote hiyo alikuwa mfanyi kazi wa serekali, |Jee alipataje shares 15% za Vodacom, majumba ya Gorofa, Ranchi za serekali , Ng'ombe zaidi ya 20,000, Ardhi kibao za ufugaji na kilimo. Na pia mwanae akiwa na umri wa miaka 21 alishakuwa millionier ten kwa $ za kimarekani na sio millionier wa shillingi zetu.

For your Information, Rafiki yake na mshiriki wake kwenye biashara ROSTOM, amenunua vila PALM JUMEIRA - DUBAI AMBAYO ILIMGHARIMU $5,500,000/- MILLIONS NI SAWA NA BILLION 14 ZA TANZANIA.

Jee huo ndio Uongozi wa Quality wa Lowasa, Kutuibia mali zetu?
 
Sijasema HAIWEZEKANI, nimesema bado hatuko tayari kwa hilo na DEFINATELY kwa Januari ndo hatuko tayari kabisaaaaa. Inaweza fosiwa ila tutazalisha vilaza.

Kwani hadi sasa ELIMU yetu inazalisha wasomi waaina gani? Tafsiri ya DR anaeikana Paper yake iliyompa uDR kisa NJAA utasema kaelimika huyo? Nyie tangu mpate UHURU tumeshaona uwezo wenu ulipoishia na kwakuwa hamna hatimiliki nahii NCHI mwaka huu tumeamua kuwapeleka kwenye Jumba la Makumbusho kwa Miaka 5 UKAWA ikiwafunza namna yakuongoza NCH
 
HatamBui hao wanaojaza mikutano take no watu ambao wamekosa ajira cyo Elimu, hivyo viwanda ni muhimu ma'am ndivyo vitakavyoendesha ghalama ya Elimu
 

Siwatukani wasomi wa Tanzania na ninawapenda sana. Ninachojua wanasoma kwa bidii lakini elimu wanayoipata ni mbovu. Ninamfahamu msomi wa geology fani ya mining engineering aliyeajiriwa Mirerani kama Mining engineer alikuwa hajui chochote kwa kukiona. Ukimwambia aelezee utampenda mwambie washa machine ya monorope hajui mwoga kuingia mgodini hajui jinsi ya kuseti vilipuzi kwasababu alikuwa mshikaji poa tulimfundisha na digrii yake . Sasa mtu kama huyo akifanyiwa usahili na mtu siriazi atatoboa? Si itabidi atafute ajira ya Bodaboda? Ndio idadi kubwa ya wasomi tulionao. Ukimkabidhi mgodi angeweza kiuuendesha kwa theories tu bila practical? Uliza kwenye makampuni wahasibu wanaokuja na degree zao bila utu wasingepewa kazi maana wanaanza kufundishwa upya. Wasomi wetu wamekuwa wa kukariri tu wafaulu mitihani. Inatakiwa ELIMU itakayotolewa ibadili mind set zetu isiwe ya kukariri kwaajili ya kufaulu mitihani tu Bali iwe ya kuelewa na iwe practical. Magufuli kanitia aibu kuwaambia wakazi wa bagamoyo atafufua kiwanda cha tanalec cha magunia. TANALEKI NI KIWANDA CHA VIFAA VYA UMEME NA KIKO Arusha. Raisi wa Libya ni Sadam no ni wa Kuwait. Mambo ya kukariri tu.

Nasema kwa sauti kubwa. ELIMU ELIMU ELIMU BORA. Wasomi tulio nao isipokuwa waliosoma nje hawawezi kuendesha viwanda. Elimu kwanza. Naunga mkono hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…