Luhaga Mpina alikuwa Waziri Kigeugeu. Je, vigeugeu wanatufaa kama Taifa?

Umesahau dk Mvungi kuuawa, umesahau watu kumwagiwa tindikali, umesahau David Mwangosi aliuawa kipindi gani ili wanashadadia kipindi cha Magufuli hata mtu angeokotwa vichaka alisingiziwa Magufuli kisa aliwatumbua vyeti feki, wakwepa kodi, wadhulumaji, mafisadi,na aliwazuia wapinzani kula asali
 
Hatukai tulipojikwaa!

Kwa akili yako mleta uzi, unataka watu wawe 2020 huko wakati tupo 2023

Bushike boko!!
 
Kwani anachosema leo ni uongo? Even a madman may say a true word.
 
We naye umekazana na quantitative hivi unajua maana yake? Yeye kasema ufisadi kwenye ripoti ya CAG umefika trillion 30 mwaka huu je hiyo trillion 30 ameielezea quantitatively imekujaje? Alafu akiambiwa atoe ushahidi aseme anaonewa.

Atoe ushahidi gani zaidi ya huo aliyotoa!
 
Pumbavu kwani kila siku ni jumatano?
 
 
Thanks brother !!Stay blessed for a nice memory.
 
Wewe mwenyewe ni kigeugeu huna hiki ama kile. Kiongozi thabiti lazima awe (Flexible and firm) ndicho anachokifanya kwa kuzingatia maslahi ya wananchi. Kwa sasa wananchi wananyanyswa sana kuliko wakati wowote na hakuna media zozote zinazosema chochote maana wote wamenunuliwa ili wasifu tu hilo kwa mbunge huyu hawezi kulikubali na msimlazimishe nyie wezi ndio maana kutwa kucha mnamshambulia huyu mwamba wa kuchambua kwa data 'realistic' sio siasa uchwara
 
Kama Samia alikuwa hapendi matendo ya Magufuli angejiuzulu, hebu punguza hii mambo ya kichawa.
 
Wewe una lako jambo na huyo bwana yako mpya aliyeanza kukutumia upya!
 
Wapi wanasema watu wameiba, Unafahamu maana ya Auditing

Mahakama ndio yenye mamlaka ya kuthibitisha wezi
Huu usomi wenu wa "Auditing" ndio unatumiwa kama kichaka na wezi, halafu mnadhani kila mtu ni mjinga atawaamini.

Iko hivi, Zitto jana akizungumza kulitaka bunge liwaruhusu wabunge waijadili ripoti ya CAG kwa uhuru, alisema hao makatibu wakuu na maafisa wengine wana mchezo wa kuwakwepa maafisa wa CAG wakienda kwenye ofisi zao kwa ajili ya kufanya ukaguzi, ajabu ikitoka ripoti chafu ya matumizi mabaya ndio wanaanza kuhangaika kutaka kujisafisha..

Hujiulizi huwa wanaficha kitu gani mpaka wamkwepe CAG akiwatembelea ofisini? huoni kuna mchezo wa kijinga hapo bila kujali mambo yako ya Auditing unayoniandikia hapa? kwani yule Zitto aliyezungumza vile sio mchumi mwenzenu?!

Na hizo mahakama zipi unazozungumzia za kuwatia hatiani hao wezi? hizi zilizowekwa mfukoni na watawala wa CCM au kuna nyingine tofauti?

Muwe mnatulia watu tukiandika mambo yetu, huo usomi wenu wa "Auditing" kaeni nao kwenye vitabu vyenu kwenye makabati yenu.
 
Who the h
ell wants to know about job description? Watu wanataka chakula mezani, siyo porojo. Pesa zinapotea na sisi tunahangaika hii ndiyo issue yetu, tunajua nchi ina Rais na lazima awe responsible.

Kama unakubali kuwa Samia alikuwa hana mamlaka wakati wa JPM kwa nini uoni kuwa hata Mpina hakuwa na hiyo privilege? Wote walikuwa under dictator kama wewe unavyotaka kusema, nakubali, sasa unamtetea Samia wakati unaona ati Mpina kigeugeu huoni hapo hiyo ni double standard?

Acha ya JPM; tujikite sasa, Mama Samia and the Team wameboronga lazima wajibu, na Mpina kwa sasa is right!
 
Alikuwa anakamata wavuvi anawaomba rushwa, wakikata, anaenda kuchoma nyavu zao na mitumbwi.

Pia alidhulumu n'gombe nyingi sana, akaenda kuzificha katavi kwa kisingizio kwamba zimetaifishwa.

Mkoa wa Morogoro amedhulumu ekari zaidi ya 1000, wanakijiji hawana mahala pa kulima, ardhi ya kilimo kachukua yote
 
Ushahidi wako uko wapi?

Kama hauna wacha kelele unatuumiza masikio.
 
Jibu hoja za Mpina acha mbambamba....
 
CCM hamna mfumo wowote. CCM, Chadema, ACT na wengine wote wa upuuzi. Tunahitaji wagombea binafsi tupate watu wenye akili zao.
 
Tatizo sio kusema ukweli , bali huyo anayesema huo ukweli anaweza kuusimamia huo ukweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…