Luhaga Mpina alikuwa Waziri Kigeugeu. Je, vigeugeu wanatufaa kama Taifa?

Mpina ana hoja au hana hoja? Matrilioni ya watanzania yameibiwa hayajaibiwa? Haya ndio ya kujadili, mambo ya huko nyuma yana faida gani?
 
Jibu hoja wapi mlipoficha fedha mlizowaibia watanzania?
 
Kakatwa sababu ya unafiki, mbona Gwajima hajakatwa licha ya kupinga sera za mama. Tatizo hiyo Mpina ni unafiki, Kuna mambo alifumbia macho awamu ya Tano mfano katiba mpya kivipi imekua ya muhimu Sasa kuliko mwaka juzi JPM alipokua hai? Kivipi sio unafiki huo
inaonekana naongea na mtu Ambaye hamjui Luhaga Mpina. Mpina alikuwa Waziri wakati wa Kikwete na JPM, (maybe na Mkapa), uwaziri ulimwishia mwisho mwisho wa JPM. Muda wote alikuwa Member wa Cabinet; angewezaje kuanza ku-debate mambo ambayo Cabinet inakubaliana nayo? Ni wakati wa ubunge tu wakati wewe siyo Member wa Cabinet unaweza kuchallenge serikali. Sasa unafiki wake hapo upo wapi? You are lacking information Sir.

Hata kama kweli hakuraise issue ya Katiba mpya wakati wa JPM, sasa wakati wa Samia ame-raise - what's wrong? Hiyo ndiyo inamfanya awe mnafiki?
 
Ukweli upi anaongea, Huyu baada ya kugundua hatarudi bungeni tena sasa anahangaika kupiga domo

Alikuwa Waziri kamili wakati wa JPM tukashuhudia Wanapima samaki kwa kutumia rula kwenye migawa
Kwani alivunja sheria?
 
Mimi ni mwana ccm Siamini Katika watu wajinga wanaomsagia mwana ccm mwenzao kunguni ili wapate cheo

CCM ni mfumo na taasisi, Tatizo hawa akina Mpina, Makonda, Sabaya, Ally happi na mnyeti waliamini Katika kuligawa Taifa hili

Hawa watu walilazimisha kuwa ndugu zetu wa upinzani ni maadui wa Taifa hivyo tusishiriki hata Katika ndoa, misiba au harusi

Walisahau Taifa hili tumeshaoana na kuzaliana hakuna Chadema wala ccm, Hakuna simba wala Yanga, Tumeshazaliana

Chuki za akina Mpina must stop
Kwani wewe unapenda Chadema wachukue inch?
 
Jibu hojazake
 
Hatuwezi kujidumaza kifikra kwa kudharau hoja za wengine kwasababu ya yale waliyofanya siku za nyuma, huko ni sawa na kuliangamiza taifa.

Kama unaamini Mpina hana sifa za kusema kile asemacho sasa kwasababu ya past, basi nioneshe yule aliye mtakatifu ili niwe namsikiliza yeye.
Anatafuta ugali, na akiupata atakaa kimya!!
 
inaonekana naongea na mtu Ambaye hamjui Luhaga Mpina. Mpina alikuwa Waziri wakati wa Kikwete na JPM, (maybe na Mkapa), uwaziri ulimwishia mwisho mwisho wa JPM. Muda wote alikuwa Member wa Cabinet; angewezaje kuanza ku-debate mambo ambayo Cabinet inakubaliana nayo? Ni wakati wa ubunge tu wakati wewe siyo Member wa Cabinet unaweza kuchallenge serikali. Sasa unafiki wake hapo upo wapi? You are lacking information Sir.

Hata kama kweli hakuraise issue ya Katiba mpya wakati wa JPM, sasa wakati wa Samia ame-raise - what's wrong? Hiyo ndiyo inamfanya awe mnafiki?
Mpina namjua vizuri sana tokea akiwa mwenyekiti wa kamati ya viwanda na biashara alikua machachari sana bunge la 10 kwenye kuisimamia serikali ila kuanzia 2015 ndio alikua waziri sio kabla ya hapo.

Sasa kivipi akiwa mbunge adai katiba mpya akiwa waziri akapotezea katiba alafu akiwa Tena mbunge wa kawaida adai katiba mpya kama sio unafiki ni Nini?

Okay alikua waziri so baraza la mawaziri huwezi pinga and blah blah. Kama anajua waliafikiana kusamehe deni la ACACIA la trillion 300+ je kwanini alipopoteza huo uwaziri ndio alalamike ilihali mwenyewe umekiri hawezi kwenda kinyume na makubaliano ya baraza la mawaziri?
 
Kwani huo ubunge alionao haumpi ugali?!

Jibuni hoja za Mpina, acheni kuhangaika.
Mkuu usiingiie huu mtego kuwaamini hawa Wana CCM Membe yukowapi? Lowassa Yuko wapi? Mpina ni Yale Yale huwa wanakuwa "wazalendo" pale tu maslahi Yao yakiguswa ila huyo Mpina akipewa uwaziri utasikia ghafla anageuka. Hivi mara hii umesahau Bashe alivyotaka Hadi TISS ivunjwe kwa kuteka watu, ila ghafla kawa waziri na hatujasikia kokote akimuomba Rais kufanya reforms huko TISS!!
 
Kuukataa huo mtego maana yake unanitaka nikae kimya pia nitazame tu "tunavyochakazwa" kwenye ripoti ya CAG..
 
Atoe ushahidi gani zaidi ya huo aliyotoa!
Sasa bajeti ya nchi haifiki trillion 45 alafu mtu anasema ufisadi uliofanyika ni Trillion 30!! Ina make sense kweli? Kingine unasema Kuna ushahidi? upi huo maana mie naona anasoma tu ripoti ya CAG ambayo ni audit query pekee na hakuna sehemu inasema trillion 30 imefanyiwa ufisadi!!
 
Pumbavu kwani kila siku ni jumatano?
We tukana tu ila Jibu hoja? Kwanini mnapenda unafiki mkikosa cheo ndio mnajifanya wazalendo, mkipata mnasahau wenye shida. WaTanzania tumeamka hatutaki Tena unafiki wenu, na nilichofurahi Mama kamng'oa NEC na hiyo 2025 ubunge asahau.
 
Kuukataa huo mtego maana yake unanitaka nikae kimya pia nitazame tu "tunavyochakazwa" kwenye ripoti ya CAG..
Yeah usikae kimya maana platform za kupinga ufisadi ni nyingi ila kamwe haiwezekani platform hiyo ikatokea CCM. hao ni wasaka vyeo tu ni mara 10 tutumie lobby groups na wanaharakati sio mbunge wa CCM
 
Sasa bajeti ya nchi haifiki trillion 45 alafu mtu anasema ufisadi uliofanyika ni Trillion 30!! Ina make sense kweli? Kingine unasema Kuna ushahidi? upi huo maana mie naona anasoma tu ripoti ya CAG ambayo ni audit query pekee na hakuna sehemu inasema trillion 30 imefanyiwa ufisadi!!
Trillion 30 ni cumulative kwa sababu miradi haikuanza mwaka ambao CAG amefanya ukaguzi.

Kuwepo kwa audit query ni udhaifu katika utekelezaji wa miradi na usimamizi mbovu wa fedha za umma, wote huo ni ufisadi na kama hujui kuwa ni ufisadi basi jitathimini mwenyewe!
 
We tukana tu ila Jibu hoja? Kwanini mnapenda unafiki mkikosa cheo ndio mnajifanya wazalendo, mkipata mnasahau wenye shida. WaTanzania tumeamka hatutaki Tena unafiki wenu, na nilichofurahi Mama kamng'oa NEC na hiyo 2025 ubunge asahau.
Kwani wabunge wenu wote ni wajumbe wa NEC? Au wajumbe wote wa NEC ni wabunge?
 
Back
Top Bottom